Athanas Myonga aibuka Mshindi wa kwanza wa Shindano la Stories of Change 2023

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,014
HALFA.jpg

Baada ya miezi mitano (5) tangu Msimu wa Tatu wa Stories of Change 2023 ulipotangazwa, kuanza na baadaye kufuatiwa mchakato wa Majaji kufanya uhakiki wa Vigezo vilivyowekwa, hatimaye usiku wa leo Oktoba 7, 2023, Washiriki waliofanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali watafahamika/julikana.

Kuhusu Shindano la Stories of Change
Huu ni msimu wa Tatu wa Shindano ambapo Msimu wa kwanza ulikuwa mwaka 2021 na Msimu wa pili mwaka ulikuwa mwaka 2022. Katika msimu huu wa tatu wa Shindano la Stories of Change 2023 Jamii Forums (JF) iliendelea kutoa nafasi kwa wadau wake na Wananchi wote kuwa sehemu ya watu wanaoleta mabadiliko chanya kwenye jamii kwa kushiriki katika shindano la uandishi wa maudhui mtandaoni wenye kuleta tija.

Mwaka huu 2023 Washiriki walishindana kuandika maandiko yanayochochea mabadiliko katika nyanja za Uwajibikaji na Utawala bora. Awamu ya Tatu (2023) ya Shindani hii ilianza Mei 15 na jumla ya Machapisho 1,214 yaliwekwa katika Jukwaa la JamiiForums.com na kupita kwenye Mchujo wa Majaji ambapo leo, Oktoba 7, 2023 tutayafahamu Maandiko yaliyoibuka kidedea.

Shindano hili lilianza Mei 15 hadi Julai 31.

Zaidi soma: Uzinduzi wa awamu ya 3 wa Shindano la Stories of Change


Kaa nasi katika uzi huu ili kufahamu Washindi na zawadi watakazozipata:

---
- Mgeni rasmi Balozi wa Sweden Nchini Tanzania, Charlotta Ozaki na Wageni Waalikwa wamewasili Ukumbini.

Meneja Programu wa JamiiForums atoa neno la ukaribisho

Ziada.jpg

Ziada Omary (Meneja Programu JamiiForums)
Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru sana kwa kuungana nasi katika tukio letu la kutoa tuzo kwa washindi wa shindano la Stories of Change mwaka 2023.

Washindi hawa wameandika makala zenye viwango vya hali ya juu zinazochochea Utawala Bora na Uwajibikaji na usiku huu ni maalum kwa kuwatambua wao na mchango wao katika kujenga taifa lenye tija kupitia maudhui ya mtandaoni.

Ikiwa ni msimu wa tatu wa Stories of Change tulipata jumla ya maandiko 1,778 na yaliyokidhi kuchapishwa ni 1,214 na ingawa leo tunatoa tuzo kwa washindi bora watano, tunapenda kutambua mchango wa kila aliyeshiriki na kupendekeza mabadiliko chanya na kuongeza idadi ya maudhui ya kiswahili yenye tija mtandaoni.

Kwa niaba ya Sekretariet ya JamiiForums ninawakaribisha sana kuwa sehemu ya tukio letu kubwa zaidi la mwaka na zaidi niwashukuru kwani kila mmoja wenu kwa namna moja au nyingine amekuwa mdau wa JamiiForums.

Karibuni tuburudike, tuelimike na tutengeneze marafiki wapya.

Mwenyekiti wa Bodi ya JamiiForums atoa neno la kufungua hafla hii

mwenyekiti.jpg

Joseph Ngwegwe (Mwenyekiti wa Bodi JamiiForums)

Kwa niaba ya Bodi ya JamiiForums, ningependa kuwakaribisha kwenye usiku wa tuzo za shindano la Stories of Change 2023.

Bodi inaipongeza timu ya JamiiForums ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Maxence Melo kwa kazi nzuri ambayo licha ya ugumu wake wameendelea kuifanya kwa ubora wa hali ya juu.

Kama Bodi tumetoa baraka zetu kupitia mpango mkakati wa taasisi huku tukiangalia kwa karibu shughuli za taasisi ili kuwapa watanzania uwanja bora na salama kuweza kupata haki yao ya kikatiba ya uhuru wa maoni.

Ningependa kutambua uwepo wa Wanachama waanzilishi wa JamiiForums ambao wametuamini kama Bodi kusimamia Taasisi hii. Tunawashukuru sana.

Ninatambua pia uwepo wa uwakilishi wa Serikali ambayo imekuwa ikishirikiana na JamiiForums katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye kulenga kumpa Mwananchi taarifa sahihi ili kumuwezesha afanye maamuzi sahihi.

Stories of Change 2023 ni moja ya programu ambazo zimekuwa na mafanikio sana kutoka kwetu na tunashukuru kila aliyeshiriki kutoa ushauri, kuandika, kutoa tuzo na Serikali kwa kufanyia kazi mawazo ya wananchi kwa mwaka 2021 na 2022 na tunatarajia mawazo ya 2023 yatafanyiwa kazi pia ili kuimarisha Utawala Bora na Uwajibikaji.

Nashukuru sana na niwatakie tafrija njema.

Balozi wa Denmark nchini Tanzania apata nafasi ya kutoa neno

Denmark.jpg

Mette Norgaard (Balozi wa Denmark)

JamiiForums imefanya mapinduzi ya kile ambacho kimekuwa kikifanyika katika Sekta ya Habari, imekua sauti ya watu wengi, imeongoza njia ya watu wanaotaka kuujua ukweli.

Tumeona umuhimu wa kile ambacho kinafanywa na JamiiForums kwa kuwaweka Wananchi pamoja na kufanya mapinduzi kwenye habari.

Katika kufanikisha Utawala Bora JamiiForums imefanya kazi na Taasisi mbalimbali za Serikali na Zisizo za Kiserikali, mfano mmoja wapo ni Taasisi ya TAKUKURU Suala la Utawala Bora ni jambo gumu na imekuwa changamoto kwa mataifa mengiTunapozungumzia Utawala Bora, tunazungumzia Uwazi, kuboresha mazingira ya kuwa na usawa.

Balozi wa Marekani nchini Tanzania atoa neno

Marekani.jpg

Dkt. Michael Battle Sr (Balozi wa Marekani)

Waandishi wa Mtaani ni jicho la jamii, wana mchango mkubwa kwenye jamii. Majukumu ya Waandishi wa Habari yanawafanya Wanasiasa kuwa makini na taarifa zao na kuwakumbusha suala la uwajibikaji.

Uandishi wa Habari unachangia uwajibikaji wa mamlaka kwa kiwango kikubwaTanzania kuna mazingira ambayo yanaruhusu uhuru wa Vyombo vya Habari.

Ripoti ya kinachofanyika kwenye Mitandao ya Kijamii inawakilisha kilichopo mtaani

Msemaji wa Serikali Mobhare Matinyi amepata atoa neno

Mobhare.jpg

Mobhare Matinyi (Msemaji Mkuu wa Serikali)

Nawashukuru JamiiForums, kwani mmeona tusiishie kusoma tu, bali mmetushirikisha tena tukio hili muhimu ili tupate kuelewa zaidi jinsi mnavyowashirikisha wananchi katika kuimarisha uhuru wa kujieleza na demokrasia nchini.

Aidha, niwashukuru kwa kuja na shindano hili la Stories of Change, ambalo linachangia wananchi kuja na suluhu ya changamoto kadhaa wanazoona katika Taifa letu huku tukichangia kuongeza maudhui chanya ya lugha ya Kiswahili mtandaoni. Najua, hii ni mara ya tatu (3) JamiiForums imetushirikisha kwenye tuzo hizi; mwaka jana mlipotoa tuzo Novemba 8, 2022, mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Mawasiliano, Mhe. Nape Nnauye, ambaye pamoja na mengine, alizindua jukwaa jipya la JamiiCheck ambalo kwakweli ni la kipekee na shirikishi la wananchi. Ni ubunifu wa kipekee toka Tanzania.

Uandishi wa Stories of Change, umenifanya nibaini namna ambavyo watanzania hasa watumiaji wa JamiiForums wana uelewa mpana wa mambo na wana mawazo ya namna bora ya kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu. Natoa wito muendelee hivi kwa miaka ijayo ili tuweze kupata mawazo zaidi ya wadau kuhusu masuala mbalimbali, tutaendelea kufuatilia kwa karibu na yale yanayowezekana kufanyiwa kazi yatazingatiwa na Serikali.

Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu wa kushirikisha wananchi katika kuimarisha utawala bora nchini hivyo tunatambua mchango huu wa JamiiForums kupitia shindano la Stories of Change. Ni sehemu ya mkakati wa Serikali na imebainishwa katika Mkakati wa kuboresha Uchumi wa Kidijitali 2023-2033 na hata kwenye Rasimu ya Sera ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari ya 2023. Uwepo wa wenzetu toka TAKUKURU ni ishara ya utayari wa Serikali katika ushirikishwaji wa wananchi na Asasi za Kiraia katika mapambano dhidi ya rushwa.

Nimepata pia kuangalia namna Fichua Uovu inavyotumiwa na wananchi na kuona MADOKEZO kadhaa yaliyowekwa na wananchi; inafurahisha kuwa mengi yamefanyiwa kazi na mengine yanaendelea kufanyiwa kazi. Nitoe wito kwa wananchi kuitumia JamiiForums kwa kutumia teknolojia hii kwani ni rahisi na ya kipekee. Mhe. Rais hivi karibuni akiwaapisha wateule wake aliwataka wamjulishe yanayoendelea katika vituo vyao. Taarifa sio lazima itoke kwa wateule tu bali hata kwa wananchi ambao wanaathirika moja kwa moja.

Kwa mara nyingine tena, niwashukuru kwa nafasi hii. Nimefurahi kuwaona washindi wa mwaka huu na nimeyapitia maandiko yao, kweli wanastahili. Hongereni sana.

Asanteni sana, JamiiForums mnafanya kazi nzuri sana - basi Kazi Iendelee!

Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums Maxence Melo akielezea zaidi kuhusu kazi za JamiiForums

Maxence jpg.jpg

Maxence Melo (Mkurugenzi Mtendaji JamiiForums)
Nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukusanyika hapa siku ya leo. Kwa niaba ya JamiiForums, napenda kutoa shukrani kwa kutenga muda wenu na kujumuika nasi siku ya leo. Nimefurahia uwepo wenu, hakika mmetuheshimisha! Leo, tumekusanyika kwa ajili ya hafla muhimu, ikiwa ni awamu ya 3 ya utoaji tuzo kwa washindi wa Stories of Change 2023. Shindano la mwaka huu, tumeshirikiana na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza (SAUT) na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) na Ushirikiano huu umekuwa nguzo katika kufanikisha shindano hili, tunakushukuru sana kwa utayari wenu wa kushirikiana nasi awamu hii.

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wetu wa miaka 5 (2020-2024), JamiiForums tumedhamiria kuinua sauti za Wananchi na kuimarisha Upatikanaji wa Taarifa kama moja ya maeneo yetu muhimu ya kimkakati. Tunafanya hivyo kwa mashirikiano na wadau wenye nia sawia ili kuongeza ubora wa maudhui mtandaoni hasa katika jukwaa la JamiiForums. Uwepo wetu hapa leo ni uthibitisho wa mafanikio ya mkakati huu.

Mwaka huu, shindano la Stories of Change limezingatia vipengele viwili muhimu kwa
maendeleo katika nchi: Uwajibikaji na Utawala Bora.

Kwa miaka yote 3, tumepata zaidi ya maandiko 4,500 kutoka kwa wananchi, waandishi wa habari, makundi maalumu, na wadau kutoka wa Asasi za Kiraia (yaliyofikia viwango na kuruhusiwa kuwa sehemu ya shindano) yenye maudhui bora kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Natoa shukrani nyingi kwa jopo letu la majaji, waliojitenga muda na utaalamu wao kutathmini kwa umakini mawasilisho na kupata washindi 5 bora zaidi. Mchango wao ni wa thamani sana, tunashukuru kwa kujitolea kwao. Uamuzi wao ulibeba 60% ya maamuzi ya kupata washindi wakati kura za mtandaoni zikibeba 40%.

Nakushukuru Mgeni Rasmi kwa utayari wako kujumuika nasi leo na kuwatuza washindi wetu. Si jambo dogo kwetu. Ni heshima kubwa umetupatia.

Nawapongeza wadau wa JamiiForums walioshiriki katika shindano la mwaka huu na kipekee pongezi nyingi kwa washindi wetu wa Stories of Change 2023.

Team JamiiForums, asanteni sana kwa kazi nzuri katika maandalizi ya shughuli ya leo pamoja na kazi nzuri mnayoendelea kuifanya katika kuwahudumia watanzania. Mnatambua kuwa daima nawapa maua yenu, ila leo HONGERENI SANA kwa maandalizi mazuri. Kazi haikuwa ndogo, lakini mmefanikisha!

Mabibi na mabwana, Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu wote mlioungana nasi jioni ya leo kwa hafla hii. Uwepo wenu hapa ni thamani kubwa kwetu kama JamiiForums. Asanteni sana kwa kujali kwenu; Mwenyezi Mungu azidi kuwabariki.

Balozi wa Sweden nchini Tanzania Charlotta Ozaki atoa Hotuba
Balozi Sweden.jpg

Charlotta Ozaki (Balozi wa Sweden)

Shindano la Stories of Change ni sehemu nzuri ya kutangaza uhuru wa kujieleza na ni sehemu sahihi ya kuonesha Demokrasia.

Uhuru wa kujieleza unahusisha uwazi, unahusisha Wananchi kuwa huru kuchagua viongozi wao

Inafurahisha kuona katika Shindano la Stories of Change jinsi Wananchi wanavyopata nafasi ya kujieleza na kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko katika Jamii.

Uhuru wa kujieleza unahusisha Uwazi kwa Wananchi kuwa huru kuchagua Viongozi wao

Inafurahisha kuona katika Shindano la Stories of Change jinsi Wananchi wanavyopata nafasi ya kujieleza na kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko katika Jamii.

Kinachofanywa na JamiiForums ni kuonesha nguvu ya maudhui kwa njia ya Digitali.

Inatia moyo kuona namna ambavyo shindano hili (Stories Of Change) linavyotoa nafasi kwa Wananchi kushiriki katika kutoa maoni yao kwa uhuru kupitia uandishi wa kidijitali

Tunaposema kuhusu uwajibikaji, mfano mzuri ni ushirikiano kati ya JamiiForums na TAKUKURU, pia kupitia jukwaa la FichuaUovu ambalo linatoa nafasi ya Wananchi kuibua masuala yanayopaswa kuzingatiwa.

Kinachofanywa na JamiiForums ni kuonesha nguvu ya Maudhui kwa njia ya Dijitali.

* Washindi wa Stories of change 2023 *
Mshindi wa Tano ni Nick Rusule (Objection)

Mshindi 1.jpg
Andiko lililoelezea na kufafanua Nafasi na Umuhimu wa Teknolojia katika kukuza Utawala Bora na Uwajibikaji katika Sekta za Umma Nchini Tanzania, limefanikiwa kumwezesha Nick Rusule kuwa Mshindi wa Tano.

Andiko hilo linaitwa, “Jukumu la Teknolojia katika Kukuza Utawala Bora na Uwajibikaji katika Sekta Za Umma" na linapatikana ndani ya JamiiForums.com katika Jukwaa la Stories of Change 2023.

Kutokana na andiko hili, Nick ameweza kujishindia zawadi ya fedha ya Tsh. Milioni 1.

Andiko lake lililoshinda:
SoC03 - Jukumu la Teknolojia katika kukuza Utawala Bora na Uwajibikaji katika Sekta za Umma
***
Mshindi wa NNE katika Shindano la STORIES OF CHANGE 2023 ni BASHARI N. KIDAYA wa Nne (Kidaya)

1696704750249.jpeg
Kutokana na changamoto ya upatikanaji wa Maji Safi na Salama katika maeneo mengi, Bashari aliwasilisha andiko linalohamasisha Mamlaka kujumuisha Miradi ya Maji kwenye Miradi ya Ujenzi ikiwemo Shule, Vituo vya Afya, Masoko au Vituo vya Mabasi ili inapokamilika itoe huduma kwa kuzingatia wingi wa Watu.

Bashari ameshinda Tsh. Milioni 2.

Andiko lake lililoshinda:
SoC03 - Tutumie maji chini ya ardhi kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji

***
Mshindi wa TATU katika Shindano la STORIES OF CHANGE 2023 ni Nathaniel Atanas Mpasi (Aimenter)

1696705134534.jpeg
Andiko la Nathaniel linahusu kuongezeka kwa matukio ya Ukatili dhidi ya Watoto ambayo yamekuwa yakifanywa na Watu wa Karibu wakiwemo Ndugu, Walimu, Majirani au kwenye Vyombo Usafiri bila kuwepo njia rafiki za kudhibiti matukio hayo.

Nathaniel amehamasisha matumizi ya Teknolojia inayowezesha Ufuatiliaji Usalama wa Mtoto anapokuwa mbali na Wazazi au Wazazi ili kumwepusha na Vitendo vya Ukatili.

Kupitia andiko hili Nathaniel ameshinda Tsh. Milioni 3.

Andiko lake lililoshinda:
SoC03 - Mfumo wa kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya ukatili-KIDGUS

***
Mshindi wa pili ni Respick Tairo Hugolini (Rs MI)

1696705257321.jpeg
Andiko alilolitambulisha kwa kuandika “Kitambulisho cha Taifa kiboreshwe ili kuendana na ulimwengu wa Kidigitali” limemfanya Respick Tairo Hugolini kuwa mshindi wa Shindano la Stories of Change 2023.

Katika andiko hili amebainisha changamoto kadhaa kuhusu Kitambulisho cha Taifa, vitu vya kuongezwa kwa lengo la kuboresha, jinsi ya kutumika Kidigitali zaidi, Sheria za Kulinda

Kwa andiko hili Respick Tairo Hugolini amejishindia Tsh. Milioni 4.

Andiko lake lililoshinda: SoC03 - Kitambulisho cha Taifa kiboreshwe ili kuendana na ulimwengu wa kidigitali

***
Mshindi wa Kwanza ni Athanas Myonga (Research Solution TZ)

1696705193928.jpeg
Andilo lililolenga kutoa ushauri kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu kupanga Malengo ya Fedha zinazokusanywa limempa Athanas Myonga nafasi ya kuwa Mshindi wa Kwanza

Andiko lake linapatikana ndani ya JamiiForums.com ambapo alilitambulisha kwa kuandika “Namna ya kupanga malengo ya fedha za kukusanya TRA ili kuwe na uwajibikaji, sio kila Mwaka wanatuambia wamevuka lengo, kwa kujiwekea malengo madogo”

Kwa andiko hili Athanas Myoga ameshinda Tsh. Milioni 7

Andiko lake lililoshinda:
SoC03 - Namna ya kupanga malengo ya fedha za kukusanya TRA ili kuwe na uwajibikaji, sio kila mwaka wanatuambia wamevuka lengo, kwa kujiwekea malengo madogo

 
Hao wanachaguana wao kwa wao huko huko mkuu,wala hili hupaswi kuliwaza
hopeless ukiambiwa utoe ushahidi utaweza? acha wivu na chuki kwa washindi na huu mtandao wa jamiiforums sawa? halafu unaonekana una stress sana na maisha magumu kwani muda mwingi nakuona ni mtu mwenye makasiriko mengi na una wivu usio na sababu kwa members maarufu hapa JamiiForums. badilika kwani unaboa sawa?
 
Back
Top Bottom