Hii jeuri Mkurugenzi wa Kilimo Uyole anaipata wapi?

kimpe

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
911
861
Jana niliona kwenye mitandao ya kijamii wananchi wakilalamika kuchukuliwa eneo lao na Taasisi ya Kilimo Uyole. nilipofuatilia hili suala ni kwamba lilishafanyiwa maamuzi miaka mitatu iliyopita na waziri wa Ardhi wa kipindi hicho Mh Lukuvi kwa kuwarudishia wananchi hekari zao 67 ambazo kilimo walizihitaji lakini wakashindwa kuzilipia fidia kwa miaka takribani ishirini.

Mbele ya Mbunge wa Mbeya ambaye ni spika wa Bunge ambaye aliwaombea wananchi hao na mgogoro huo ukatatuliwa lakini siku tatu zilizopita Mkurugenzi wa Kilimo kawapa tenda Suma JKT Uyole wajenge ukuta ndani ya makazi ya watu ambao wameshahamia kwa nia ya kutaka kulitwaa upya

Taharuki hii anaypianzisha mkurugenzi haijulikani ni nani yupo nyuma yake lakini kwa anayoyafanya ndo yale Miaka ya unanijua mimi nani wapeni haki zao wananchi kuwafidia hamuwezi
 
Wana eneo kubwa sana lakini bado wanataka maeneo ya wananchi, nashauri hii taasisi ipo katikati ya mji ihamishwe ilo eneo wauziwe wananchi ili wajenge
 
Wana eneo kubwa sana lakini bado wanataka maeneo ya wananchi, nashauri hii taasisi ipo katikati ya mji ihamishwe ilo eneo wauziwe wananchi ili wajenge
Ni kweli kabisa katikati ya jiji Alizeti zinafanya nini unganisha Uyole na Sae kwa majumba makali waende Inyala huko mapori kibao
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom