Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,893
- 3,200
Habari wana jamvi wa JF,
Sisi kama binadamu, tumeumbwa kufuata miongozo.
Miongozo hiyo imo katika vitabu vitakatifu kama vile Biblia na Msahafu kwa upande wa dini na Katiba kwa upande wa kisiasa.
Bila miongozo hii, tusingekuwa hapa tulipo na dunia pasingekuwa mahali salama pa kuishi.
Hivyo, hata kama mtu hufuati kile kilichomo kwenye hivyo vitabu, ni hatari sana kusimama na kusema huyafuati maana uovu uambukiza hasa pale unapofanywa au kuhamasishwa na kiongozi.
Hivyo Rai yangu kwetu sote, kwa maana ya viongozi na raia, tuweke msisitizo wa kufuata miongozo yetu ile tuliyowekewa (Biblia kwa Wayahudi na Wakristo na Msahafu/Qoran kwa Umma wa Kiislam) na ile tuliyojiwekea (Katiba kwa wote wenye dini na wasio na dini).
Vinginevyo tukifanya tofauti na hivyo, basi tutakiona cha mtema kuni!
Hakuna dharau mbaya sana kama ile ya kudharau au kuonesha kudharau Miongiozo.
Ahsanteni sana.