Hesabu za Membe hazipo sawa sawa

kali KENYATTA

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
288
166
Hesabu za Membe hazipo sawa sawa. Lowassa alifanya timing muhimu mno. Mwaka pekee ambao tungeshudia Upinzani ukishika dola ulikua ni 2015. CCM ni chama kinachobadilika kulingana na mazingira. Kinajikosoa na kubadilika.

1. CCM ilikua imechukiwa na raia. Hivyo 2015 ilikua ni karata muhimu kuiondoa CCM madarakani.

2. Lowassa alikua na umaarufu na uwekezaji mkubwa kwenye safari yake kuelekea IKULU. Sioni Membe akifika hata nusu za harakati za Lowassa.

3. Membe anakwenda kupambana na CCM iliyorudisha imani kwa raia. Anakwenda kukutana na siasa za Upinzani zilizogawanyika. Sitegemei ile spirit ya UKAWA kuwa live. Mwaka 2015 kulitokea kusalitiana. Vyama vya upinzani haviaminiani kirahisi.
 
Hesabu za Membe hazipo sawa sawa. Lowassa alifanya timing muhimu mno. Mwaka pekee ambao tungeshudia upinzani ukishika dola ulikua ni 2015. CCM ni chama kinachobadilika kulingana na mazingira. Kinajikosoa na kubadilika.

1. CCM ilikua imechukiwa na raia. Hivyo 2015 ilikua ni karata muhimu kuiondoa CCM madarakani...
Alishindwa kujenga hoja ya watanzania kuwa na dual citizenship, hata kwa masharti fulani bali kuruhusu watanzania walioko nje watumie mianya yote huko bila kupoteza haki zao nyumbani.
 
Naungana na wewe MEMBE HAKUBARIKI KIASI ANACHODHANI
Yule mnayemwita kachero sijui mbobezi nadhani hata hatumii akili.Sijui hata huo ukachero wake unamsaidia nini Membe kwa sababu anatajwa tu katika mikoa ya Dar,Pwani ,Lindi ,Mtwara labda na Ruvuma.Nikuhakikishie kwamba mikoa iliyobaki hata hilo jina hawajawahi kulisikia.

Nenda Kilimanajro,Simiyu ,Shinyanga ,Geita ,Mara nk.ukilitaji jina la Membe watalishangaa.Hawajawahi hata kumsikia. labda kuna lingine analitafuta lakini siyo Urais.
 
Yule mnayemwita kachero sijui mbobezi nadhani hata hatumii akili.Sijui hata huo ukachero wake unamsaidia nini Membe kwa sababu anatajwa tu katika mikoa ya Dar,Pwani ,Lindi ,Mtwara labda na Ruvuma.Nikuhakikishie kwamba mikoa iliyobaki hata hilo jina hawajawahi kulisikia.Nenda Kilimanajro,Simiyu ,Shinyanga ,Geita ,Mara nk.ukilitaji jina la Membe watalishangaa.Hawajawahi hata kumsikia .labda kuna lingine analitafuta lakini siyo Urais.
Umenena vyema. Lowassa ametoa fundisho. Tena kwa gharama kubwa. Halafu Membe anataka kufanya mambo kirahisi rahisi kiasi hiki? Halafu wakati huu?
 
Mimi CCM damu damu. Napenda tume huru, napenda mihimili huru inayofanya kazi kwa weledi.

Kwa sasa ni ngumu sana upinzani kutoboa, nasema kushinda hata iwepo tume huru bado ni ndoto.

Hizi siasa zetu za mitandaoni zinazofanywa na wenye mtazamo chanya wanaoweza kung'amua mambo ni sehemu ndogo sana ya wapiga, na mbaya zaidi asilimia kubwa ya hawa waelewa huwa siku kupiga kura hawajitokezi kupiga kura.

Hata kama chama changu tawala kina kasoro zake kitapita tu maana wanaopiga kura ni watu wa kawaida, japo wengi wana maisha magumu ila wataenda kupiga kura kutokana na sifa wanazosikia bila ya hata kufahamu uhalisia wa sifa husika.
 
Hakuna haja ya kuweweseka au kupiga ramli tusubiri october mbichi na mbivu zitajulikana... huenda kura zikagawika mara tatu sitoshangaa hili na mshindi akawa chini ya 48% sijui katiba itasemaje... vinginevyo zipikwe kura za ziada!!
 
Hakuna haja ya kuweweseka au kupiga ramli tusubiri october mbichi na mbivu zitajulikana... huenda kura zikagawika mara tatu sitoshangaa hili na mshindi akawa chini ya 48% sijui katiba itasemaje... vinginevyo zipikwe kura za ziada!!
Fact check on the ground, JPM anaenda kushinda kwa kishindo. Wakati mgumu kwake ulikua 2015.
 
Atakuwa rais wa mitandao. Kama kurudisha kadi ilikuwa dili kisiasa, jama nchi ingezizima kwa wanaorudisha kadi. Aangalie tofauti yake na Seif Sharif Hamad alipohama chama.
Amekosea aana mahesabu yake.
 
Membe ni amepiga hesabu kali kuliko Lowassa. Amesimama kama mbadala wa JPM (alternative to) Amejiseti kwenye mteremko.
 
Atakuwa rais wa mitandao. Kama kurudisha kadi ilikuwa dili kisiasa, jama nchi ingezizima kwa wanaorudisha kadi. Aangalie tofauti yake na Seif Sharif Hamad alipohama chama.
Amekosea aana mahesabu yake.
Wana CCM wa sasa ni CCM kazi aka wahemeaji. Unarudisha kitambulishon ha kaxi kumsaport mwanasiasa????
 
Back
Top Bottom