Buriani Benard Membe, Umepigana Vita Vilivyo Vitakatifu, Mwendo Umeumaliza, Imani Umeitunza, Madeni Yako Yaliyobakia Karma Itakulipia!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,499
113,608
Screen Shot 2023-05-14 at 8.08.55 AM.png
Screen Shot 2023-05-14 at 8.09.22 AM.png

Wanabodi, leo katika viwanja vya Karimjee, Watanzania tunamuaga aliyekuwa Waziri wetu kwa kipindi chote cha miaka 10 ya utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete, Mwana Diplomasia nguli, Bernard Cammilus Membe, aliyefariki dunia ghafla, juzi Ijumaa asubuhi.

Nilivyomfahamu Membe.
Fani yetu ya uandishi wa habari, inatukutanisha sisi waandishi wa habari na watu mbalimbali, hivyo japo sikumbuki nilikutana vipi kwa mara ya kwanza na Benard Membe, ila nilikuja kupata nafasi ya kuzungumza nae kwa nafasi, wakati wa safari za UNGA, ambapo enzi za Mkapa, mimi ndio mwandishi wa kwanza wa vyombo vya habari binafsi kusafiri na ujumbe wa Tanzania, kwenda kuripoti Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, ndiko nilikokutana na JK kwa nafasi.

Hivyo baada ya JK kuingia Ikulu, niliendelea kuripoti UNGA na kukutana na Membe akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Kufuatia Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Nje, wa Rais Mwinyi Mwinyi, kisha akaja kuwa rais wa JMT, kwa kumpokea Mwinyi, na Jakaya Kikwete akawa Waziri wa Nje wa Mkapa, akaja kumpokea Mkapa kwenye urais wa Tanzania, hivyo Benard Membe akiwa ndiye Waziri wa Nje wa Kikwete akitegemewa ndiye angempokea Kikwete ile 2015 ila haikuwa hivyo.

Ni kufuatia trends hiyo, Waziri Benard Membe akawa anaongea kwa confidence kubwa sana kwa mamlaka kama rais mtarajiwa.

Kuna wakati kupitia kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV, alitutishia sisi waandishi wa habari kwa kutuambia tuombe asioteshwe kugombea urais mwaka 2015, ikitokea akaoteshwa, kuna maadui zake 11, itawabidi watafute pa kuhamia, kwa kuihama nchi, na akataja, miongoni mwa hao maadui zake 11, wamo waandishi wa habari wawili! Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya!

Kwa vile na mimi ni mwandishi wa habari, na niliwahi kuwa very critical kumhusu Membe kwa kumuona kama mtu pompous tuu with nothing of substance, hivyo nilitofautiana nae kwenye mambo mbalimbali ikiwemo Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi na issue hii
Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane!
hivyo kuelekea mwaka 2015 ili nisije kuwemo kwenye ili list ya kuihama nchi, nikajitolea kumsaidia Membe.

Alikuwa mtu wa watu, very social and easy to talk to!
Kuna siku kwenye sherehe fulani ya Send Off ya mdogo wake mwandishi wa habari mwenzetu, Usia Nkhoma Lendama, nilikutana face to face na Benard Membe na nikashusha bandiko humu JF Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"

Economic Diplomacy
Ni kipindi cha Membe ndipo Tanzania ikabadili diplosia yetu kutoka vita baridi, kuwa ni diplomasia ya kiuchumi, economic diplomacy, nilipokutana na Membe, nikampondea, tunafuata vipi diplosia ya kiuchumi wakati kwenye Balozi zetu, bado tunajaza waambata wa kijeshi na wale 'jamaa zetu' wa 'kazi mbili mbili' badala ya kupeleka waambata wa kiuchumi?!. Membe alicheka tuu! Maendeleo ya kweli Tanzania yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

2015 Ilikuwa Awe Membe, Ilikuwaje Hakuwa?
You can never be sure with politics, ndio maana kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, kwanza nilianza na Membe ile 2013 Nitamuunga mkono Benard Membe 2015 kama akioteshwa kugombea urais wa Tanzania
ndipo 2014 nikaja kupenyeshewa hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli toka ile August 2014, but you can't be sure until it happens, hivyo kuelekea 2015 japo nili bank na Edward Lowassa, Benard Membe pia niliweka akiba nikijua pia anaweza kuwa ni Membe, nikamuandalia a video documentary nzuri kumfagilia njia ya 2015, na baada ya kuikamilisha nikawapelekea wadau muhimu wa kutoa mpunga wa maana kuidhamini irushwe ili Membe apae!, wadhamini wakagoma!, ndipo nikaanza kuusoma mchezo wa 2015 kuwa kumbe sio Membe!

Na kweli Membe akaja kutoswa. Japo Mkapa alishindana na Kikwete na Lowassa, baada ya ushindi aliwachukua, na Kikwete akashindana na Prof. Mwandosya na Dr. Salim Salim, baada ya kushinda aliwachukua, ila Membe baada ya kutoswa, alitoswa jumla! Membe be careful, adui yako wa kweli humjui!

Hivyo kuelekea 2020, Membe akaamua kutingisha kibiriti, kuna mwandishi mmoja wa habari kichaa akaamua kumchafua, Membe akaibuka na niguse ninuke, na kweli akakinukisha na kufukuzwa CCM.

Niliandika kitu kumhusu Membe nikamshauri japoameonewa lakini asifanye maamuzi ya hasira Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!.

Nilimpa ushauri kuwa asihame CCM kwa hasira, haikusaidia, alihama CCM na kuhamia ACT Wazalendo na kuwa mgombea wake wa urais. Niliendelea kumtetea Membe Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity kumhusu Membe, nilisema
Wanabodi

8. Benard Membe
Sauti inayodaiwa ni ya Membe na Katibu Kata kijiji cha Rondo video ...
Tangu kuanza kuvuja kwa hizi sauti, hakuna mwingine yoyote ni bold enough kukiri kuwa ni sauti yake, Membe tuu pekee ndio lijitu bold lenye ma confidence ya ajabu, limekiri sauti iliyodukuliwa ni yake na anajua sauti hiyo imedukuliwa na TISS, anajua kudukuliwa ni kosa la jinai hivyo anashangaa rais anatumiaje data zilizopatikana kujinai kuadhibu watu?. Kwa vile Membe bado ana kinyongo cha kushindwa na Magufuli, halafu Magu amemshiti jumla na kumtelekeza, hivyo kwa vile Membe aligombea na Magufuli, anajiona yeye ni bora kuliko Magufuli, hivyo Magufuli kwake japo ni rais wa nchi, lakini Magufuli hajawahi kuwa kachero, kutokana na ukachezo mbobezi anayejua sheria, taratibu na kanuni, anajua kudukua ni kosa la jinai lakini rais anaitumia jinai hiyo kuwatisha watu wanaomkosoa, hivyo kwake, Magufuli sii lolote sii chochote, ana pride fulani, ni kiburi na jeuri ya ukachero. Huyu hataomba msamaha wowote kwa yeyote na popote na yuko tayari kwa lolote, liwalo na liwe!.
Baada ya uchaguzi, alijirudi na kurejea nyumbani na akapokelewa, akamfungulia kesi yule mwandishi kichaa, akashinda na mwandishi anatakiwa kumlipa Membe mabilioni ambayo hana.

Mwandishi kichaa akawatumia baadhi ya maaskofu kumuombea msamaha kwa Membe, Membe akawagomea, sisi watu wa ushauri wa bure pia tukashauri. Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani mwenzetu, wakati alipokuwa akiyatenda hayo na kufanya makosa yale, hakuwa yeye, he was insane and possessed by demons hivyo kuwa kama kichaa kabisa! ni shetani alikuwa akimiliki na akimtumia!, hivyo baada ya kuombewa, mapepo yamemtoka, ametambua makosa yake, ametubu, ameomba msamaha, as a human being, hata kichaa anastahili msamaha Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo
Kwenye ushauri huo, kuna mistari Mikhail niliweka
Wanabodi,

Kitendo cha Membe kutowatii maaskofu kitamgharimu sana!. Kuna kiongozi fulani aliwahi kuwadharau maaskofu, najua ni nini kilikuja kumtokea, hivyo sitaki Membe yamkute ya kumkuta!. Amsamehe tuu huyu kichaa, ameishajirudi, akili zimemrudia!, amekubali kosa, ametubu dhambi zake kwa viongozi wake wa dini, wanamuomba Membe amsamehe, Membe asamehe tuu.

Paskali
Hatimaye kabla ya kulipwa mabilioni yake, ndio sasa Membe ameitwa mbele ya haki, na leo ndio tunamuaga ukumbi wa Karimjee.

Kitu cha kwanza ninachosema, kuna uwezekano Membe ndani ya moyo wake aliisha samehe zamani tuu, hivyo kama alisamehe, then wadeni wake wako salama, lakini kama hajasamehe amekufa na kinyongo, namshauri yule kichaa, mwandishi mwenzetu wa habari, atafute muda, kwa muda wake, aende kwenye kaburi la Membe, kumlilia na kumuomba msamaha hata kifoni ili amsamehe, asipofanya hivyo, Membe atafidiwa kupitia kitu kinachoitwa fidia za karma, na kiukweli gharama zake huwa ni kubwa kuliko kitu chochote!.

Benard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Mwendo umeumaliza,
Imani umeitunza,

Sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi,
Bwana alileta, Bwana ametwaa.
Jina lake Lihimidiwe

Rafiki Mwana Diplosia Nguli, Benard Camilus Membe, Buriani na Kwaheri ya Kuonana...

Paskali
 
In 2015, this ship started sailing unchartared waters. In 2021, the sea gets murky, a potential storm, a catastrophy of biblical proportions struck the ship.

And like the gloomy analogy from the Book of Jonah, the cabin crew cast a vote and it befell on the Captain who is then tossed into the sea as a sacrificial lamb .

This Captain is the one who took a major detour, and instead of going to Nineveh he chose Tarshish, the unchartered waters much at the displeasure of his cabin crew and many passengers who were seasick.

In 2023, a stranded cabin crew starts to jostle over the control of the ship and some are tossed into the sea as the previous Captain.

And as a hedonistic Roman citizenry hysterically cheered at bloodstains and gore of the Colosseum, the demented, and short-sighted passengers cheer at the spectacle made by the cabin crew.

With great enthusiasm and fanfare, the yell and wave their placards, some place their bets on the spectacle to gain fortune or be in good graces of the Cabin Crew. It's a sick mob indeed.
 
........Mwandishi kichaa akawatumia baadhi ya maaskofu kumuombea msamaha kwa Membe, Membe akawagomea, sisi watu wa ushauri wa bure pia tukashauri. Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani mwenzetu, wakati alipokuwa akiyatenda hayo na kufanya makosa yale, hakuwa yeye, he was insane and possessed by demons hivyo kuwa kama kichaa kabisa! ni shetani alikuwa akimiliki na akimtumia!, hivyo baada ya kuombewa, mapepo yamemtoka, ametambua makosa yake, ametubu, ameomba msamaha, as a human being, hata kichaa anastahili msamaha Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo
Kwenye ushauri huo, kuna mistari Mikhail niliweka

Hatimaye kabla ya kulipwa mabilioni yake, ndio sasa Membe ameitwa mbele ya haki, na leo ndio tunamuaga ukumbi wa Karimjee.

Kitu cha kwanza ninachosema, kuna uwezekano Membe ndani ya moyo wake aliisha samehe zamani tuu, hivyo kama alisamehe, then wadeni wake wako salama, lakini kama hajasamehe amekufa na kinyongo, namshauri yule kichaa, mwandishi mwenzetu wa habari, atafute muda, kwa muda wake, aende kwenye kaburi la Membe, kumlilia na kumuomba msamaha hata kifoni ili amsamehe, asipofanya hivyo, Membe atafidiwa kupitia kitu kinachoitwa fidia za karma, na kiukweli gharama zake huwa ni kubwa kuliko kitu chochote!.

Benard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Mwendo umeumaliza,
Imani umeitunza,

Sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi,
Bwana alileta, Bwana ametwaa.
Jina lake Lihimidiwe

Rafiki Mwana Diplosia Nguli, Benard Camilus Membe, Buriani na Kwaheri ya Kuonana...

Paskali
mkuu Paskali umefanya vyema sana kuandika hii butiani.

Nilikuwa nasubiri sana kusoma andiko lako la kumuaga marehemu Membe.

Niseme kwamba, ukomavu wa kifikra mara nyingine ni prediction ya near future. Nani alijua kuwa Mzee Membe angeliondoka mapema hivi?

Mimi nilisimama kukupinga kwenye andiko nililoliquote hapo juu. Lakini nahisi kama napaswa kuyameza maneno yangu. Ulimshauri kusamehe na sisi wapenda haki tulisimama kidete kutetea msimamo wa marehemu. Hatukufanya hivyo kwa sababu tunamchukia sana Musiba bali tulipima madhara makubwa yaliyojiri awamu ile na ili kuzuia yasije yakajirudia tena kwa kupata mfano unaoishi.

Ushauri kwa Musiba ni ushauri wa kiungwana sana.

Naamini Membe hakuwahi kulisaliti Taifa kwa sababu sisi wa vijiweni tunajua adhabu ya jasusi anayesaliti nchi ipoje.

Tuungane sote kumtakia mapumziko mema ndugu na mzee wetu Membe. Tukatae kufarakanishwa na mashabiki wa kambi zinazofurahia vifo vya watu wasiowapenda.

Amen
 
View attachment 2620991View attachment 2620992
Wanabodi, leo katika viwanja vya Karimjee, Watanzania tunamuaga aliyekuwa Waziri wetu kwa kipindi chote cha miaka 10 ya utawala wa Jakaya Mrisho Kikwete, Mwana Diplomasia nguli, Bernard Cammilus Membe, aliyefariki dunia ghafla, juzi Ijumaa asubuhi.

Nilivyomfahamu Membe.
Fani yetu ya uandishi wa habari, inatukutanisha sisi waandishi wa habari na watu mbalimbali, hivyo japo sikumbuki nilikutana vipi kwa mara ya kwanza na Benard Membe, ila nilikuja kupata nafasi ya kuzungumza nae kwa nafasi, wakati wa safari za UNGA, ambapo enzi za Mkapa, mimi ndio mwandishi wa kwanza wa vyombo vya habari binafsi kusafiri na ujumbe wa Tanzania, kwenda kuripoti Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York, ndiko nilikokutana na JK kwa nafasi.

Hivyo baada ya JK kuingia Ikulu, niliendelea kuripoti UNGA na kukutana na Membe akiwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Kufuatia Benjamin Mkapa kuwa Waziri wa Nje, wa Rais Mwinyi Mwinyi, kisha akaja kuwa rais wa JMT, kwa kumpokea Mwinyi, na Jakaya Kikwete akawa Waziri wa Nje wa Mkapa, akaja kumpokea Mkapa kwenye urais wa Tanzania, hivyo Benard Membe akiwa ndiye Waziri wa Nje wa Kikwete akitegemewa ndiye angempokea Kikwete ile 2015 ila haikuwa hivyo.

Ni kufuatia trends hiyo, Waziri Benard Membe akawa anaongea kwa confidence kubwa sana kwa mamlaka kama rais mtarajiwa.

Kuna wakati kupitia kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na ITV, alitutishia sisi waandishi wa habari kwa kutuambia tuombe asioteshwe kugombea urais mwaka 2015, ikitokea akaoteshwa, kuna maadui zake 11, itawabidi watafute pa kuhamia, kwa kuihama nchi, na akataja, miongoni mwa hao maadui zake 11, wamo waandishi wa habari wawili! Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya!

Kwa vile na mimi ni mwandishi wa habari, na niliwahi kuwa very critical kumhusu Membe kwa kumuona kama mtu pompous tuu with nothing of substance, hivyo nilitofautiana nae kwenye mambo mbalimbali ikiwemo Serikali ya Tanzania yatoa tamko, yamlilia Gaddafi na issue hii
Membe amejuaje Contents za 'Diplomatic Bag'? Uwezo kukanusha kaupata wapi? - Tusidanganyane!
hivyo kuelekea mwaka 2015 ili nisije kuwemo kwenye ili list ya kuihama nchi, nikajitolea kumsaidia Membe.

Alikuwa mtu wa watu, very social and easy to talk to!.
Kuna siku kwenye sherehe fulani ya Send Off ya mdogo wake mwandishi wa habari mwenzetu, Usia Nkhoma Lendama, nilikutana face to face na Benard Membe na nikashusha bandiko humu JF Face To Face With Mhe. Benard Camilius Membe!. "Sipati Usingizi!"

Economic Diplomacy
Ni kipindi cha Membe ndipo Tanzania ikabadili diplosia yetu kutoka vita baridi, kuwa ni diplomasia ya kiuchumi, economic diplomacy, nilipokutana na Membe, nikampondea, tunafuata vipi diplosia ya kiuchumi wakati kwenye Balozi zetu, bado tunajaza waambata wa kijeshi na wale 'jamaa zetu' wa 'kazi mbili mbili' badala ya kupeleka waambata wa kiuchumi?!. Membe alicheka tuu! Maendeleo ya kweli Tanzania yataletwa na Elimu na Ukweli. Tusidanganye, Tusidanganywe, Tusidanganyike!

2015 Ilikuwa Awe Membe!, Ilikuwaje Hakuwa?!
You can never be sure with politics, ndio maana kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, kwanza nilianza na Membe ile 2013 Nitamuunga mkono Benard Membe 2015 kama akioteshwa kugombea urais wa Tanzania
ndipo 2014 nikaja kupenyeshewa hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli toka ile August 2014, but you can't be sure until it happens, hivyo kuelekea 2015 japo nili bank na Edward Lowassa, Benard Membe pia niliweka akiba nikijua pia anaweza kuwa ni Membe, nikamuandalia a video documentary nzuri kumfagilia njia ya 2015, na baada ya kuikamilisha nikawapelekea wadau muhimu wa kutoa mpunga wa maana kuidhamini irushwe ili Membe apae!, wadhamini wakagoma!, ndipo nikaanza kuusoma mchezo wa 2015 kuwa kumbe sio Membe!.

Na kweli Membe akaja kutoswa. Japo Mkapa alishindana na Kikwete na Lowassa, baada ya ushindi aliwachukua, na Kikwete akashindana na Prof. Mwandosya na Dr. Salim Salim, baada ya kushinda aliwachukua, ila Membe baada ya kutoswa, alitoswa jumla! Membe be careful, adui yako wa kweli humjui!

Hivyo kuelekea 2020, Membe akaamua kutingisha kibiriti, kuna mwandishi mmoja wa habari kichaa akaamua kumchafua, Membe akaibuka na niguse ninuke, na kweli akakinukisha na kufukuzwa CCM.

Niliandika kitu kumhusu Membe nikamshauri japoameonewa lakini asifanye maamuzi ya hasira Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!.

Nilimpa ushauri kuwa asihame CCM kwa hasira, haikusaidia, alihama CCM na kuhamia ACT Wazalendo na kuwa mgombea wake wa urais. Niliendelea kumtetea Membe Psychoanalysis ya Waomba Msamaha Kwa Rais, Makamba Snr is the Next, Membe Will Never for Pride, Kiburi na Jeuri, Kinana Will Never for Integrity kumhusu Membe, nilisema

Baada ya uchaguzi, alijirudi na kurejea nyumbani na akapokelewa, akamfungulia kesi yule mwandishi kichaa, akashinda na mwandishi anatakiwa kumlipa Membe mabilioni ambayo hana.

Mwandishi kichaa akawatumia baadhi ya maaskofu kumuombea msamaha kwa Membe, Membe akawagomea, sisi watu wa ushauri wa bure pia tukashauri. Huu ni wito wangu na ushauri wangu wa bure kwa Bernard Membe, asibishane na Maaskofu, amsamehe tuu huyu mwana fani mwenzetu, wakati alipokuwa akiyatenda hayo na kufanya makosa yale, hakuwa yeye, he was insane and possessed by demons hivyo kuwa kama kichaa kabisa! ni shetani alikuwa akimiliki na akimtumia!, hivyo baada ya kuombewa, mapepo yamemtoka, ametambua makosa yake, ametubu, ameomba msamaha, as a human being, hata kichaa anastahili msamaha Bernard Membe usibishane na Maaskofu, samehe tu. Yule ni kichaa anastahili msamaha, hakujua atendalo
Kwenye ushauri huo, kuna mistari Mikhail niliweka

Hatimaye kabla ya kulipwa mabilioni yake, ndio sasa Membe ameitwa mbele ya haki, na leo ndio tunamuaga ukumbi wa Karimjee.

Kitu cha kwanza ninachosema, kuna uwezekano Membe ndani ya moyo wake aliisha samehe zamani tuu, hivyo kama alisamehe, then wadeni wake wako salama, lakini kama hajasamehe amekufa na kinyongo, namshauri yule kichaa, mwandishi mwenzetu wa habari, atafute muda, kwa muda wake, aende kwenye kaburi la Membe, kumlilia na kumuomba msamaha hata kifoni ili amsamehe, asipofanya hivyo, Membe atafidiwa kupitia kitu kinachoitwa fidia za karma, na kiukweli gharama zake huwa ni kubwa kuliko kitu chochote!.

Benard Camilus Membe,
Umepigana vita vilivyo vitakatifu,
Mwendo umeumaliza,
Imani umeitunza,

Sisi tulikupenda, lakini Bwana amekupenda zaidi,
Bwana alileta, Bwana ametwaa.
Jina lake Lihimidiwe

Rafiki Mwana Diplosia Nguli, Benard Camilus Membe, Buriani na Kwaheri ya Kuonana...

Paskali
Duh Paskali!
 
Nimekusoma kirefu, paliponivutia ni pale ambapo Membe alionekana kujiamini 2015 itakuwa zamu yake, mpaka akawataja maadui zake 11 aliodai angeanza nao, wajiandae kukimbilia Kenya.

Wewe kwa kuiona fursa ukamuandalia documentary ya kumsafishia njia, ukawapelekea ulioamini wangeipenda waisogeze mbele, bahati mbaya ikatoswa, hapo ndipo akili ikakukaa sawa na kujua kumbe 2015 isingekuwa ya Membe ingekuwa ya Magufuli.

Baada ya kuyasoma hayo, nimetambua inawezekana ule mchezo wa kulikata jina la Lowassa uliandaliwa vizuri na JK, na kwa kujua kuwa supporters wa Lowassa wangekasirika baada ya pale, akamuacha Membe asogee hatua moja zaidi mbele kwenye ule mchakato wa uchujaji, ili hasira ziwapande vizuri wale wajumbe wa Lowassa.

Baada ya hapo, ndipo JK akamchinja na Membe ili kumaliza hasira zao, na kwa kufanya vile alifanikiwa sana, wao kwa kudhani JK alitaka kumbeba Membe, kumbe inawezekana hata hakuwa na mpango huo, ule ulikuwa ni mchezo tu.

Mbele ulipoandika kumkumbusha Membe kwamba adui yake sio yule anayemdhania, hapo ndipo akili yangu ikafunguka zaidi, kuwa inawezekana adui wa Membe alitokana na ule msemo wa kiswahili "kikulacho ki nguoni mwako" jamaa alitumiwa bila kufahamu, kama Lowassa pamoja na urafiki wao alitoswa, kwanini isiwe kwa Membe!.
 
Interesting Obituaries....
Kama amekufa Kwa mipango ya Mungu ...the chapter is closed .
Kama kuna faulo...let's see the retaliation...itakuja tu...
 
Uchambuzi mzuri sn!
Kwa membe tuenzi mema alofanya - kwa Musiba tuchukie kutumikishwa na njaa na watawala
 
Mkuu uandishi wako ni ishara tosha kuwa wewe ni zaidi ya mwandishi wa habari. Umegusa kila angle ya maisha membe kwa namna nzuri na ya ajabu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom