Hesabu ya dereva wa daladala Baada ya nauli kupanda

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Naomba kujua kama hesabu ya siku ya dereva wa daladala has Dar, inatakiwa ipande kwa kiasi gani ?

Kwa sababu vipuri vimepanda bei sana .

Nina daladala 3 zinatoka buza hadi mnazi mmoja na kwa siku nakusanya 75000 kwa kila daladala, Niongeze kiasi gani kwa haya mabadiriko ya nauli yalitangazwa .
 
Nauli kutoka 500 hadi 700 ni ongezeko la 40%

Kama na wewe unataka kuongeza unaweza kuongeza kwa hizohizo 40% za pato la awali au chini ya hapo kulingana na bei ya za mafuta kupanda

Mfano ongezeko la nauli kwa %
(new value − original value) ÷ original value × 100 = Percentage increase

(700-500)
°°°°°°°°°°°° × 100 = 40%
500

Mfano ongezeko la mapato kwa 40%
75,000 + (75,000 ×40%)
75,000 + 30,000
105,000 pato jipya baada ya kuongeza 40%

Niwewe tu Unaweza kuongeza 20% au 30% kwa kuzingatia gharama za mafuta au 40% ambayo ni sawa na ongezeko la nauli bila kuzingatia Gharama za mafuta

Nimejaribu kwa elimu yangu ya QT
 
700-550=150

150/550 x 100%= 27%

Ongezeko la asilimia 27 %
27% ya 75000 ni 20000

So 75000+20000=95,000/-

Makadirio ni 95,000/-

Mbona hujaweka (hujatoa) fuel inflation au mwenye gari ndiye anaweka mafuta?
Kwa kipindi kifupi tu nimeona mafuta yakipanda bei karibia kila mwezi
 
Back
Top Bottom