Heko kwa Kufuzu, ila kwa Mpira 'mbovu' tuliocheza na kwa Timu tunayoenda Kukutana nayo, tukifuzu Nusu Fainali mnizamishe Baharini na Jiwe

Watu kama nyie ndo mnafanya nisiiamini JF

Inawezekana kukosea kwa ulichokiandika ila unavyozidi kubisha napata shaka na lengo la mabandiko yako hapa JF
 
Simba atatinga robo fainal iwapo tu hawa wachezaji watatu wakipewa onyo na ushauri wa kisaikolojia .
1.Morrison aambiwe aache ubinafsi ,yule jamaa ni mchezaji mzuri Sana na mpira anaujua haswa shida yake ubinafsi na kutaka kuzungumziwa yeye na kutaka ufalame, aambiwe timu kwanza alafu yeye afuate ,mfano Jana matokeo liyashikilia yeye ,kipindi cha kwanza tu kazi ilikua inaisha ila nadhan aliambiwa kwenye changing room na kipindi cha pili kweli aliacha uchoyo na hatimae kupata matokeo ,narudia tena uongozi wa Simba ukae nae huyu mtu na kumchana ukweli.

2.Sacko .
Huyu maelezo ya bm3 yote yanaangukia hapa.

3.Kanoute .
Huyu dogo niseme tu ukweli mm sijawah mwelewa ni mtu anayepoteza Sana mipira na Jana ilikua bahat tu kwa upande wetu lasivyo angetugharimu ,pmaoja na kwamba alifunga kwa kutoa bikra ila sio wa kumwamini Sana huyu.

Nyongeza ni Onyango huyu nae sio wa kumwamini pass mbovu ,na Jana kidogo atukost ni bahat adebayo alimkwepa lile lingekua tuta ,jamaa Ana making mbovu Sana pale anapozidiwa na opponent wake .
Onyango atafutiwe mbadala msimu ujao
 
Kama Simba Ni mbovu, hao waliotolewa tunawaitaje. Kuna timu mbovu inashinda goli nne bila?

Kimpira kila mfungaji Ni mchoyo, na kilichokosekana KWA simba jana hasa kipindi Cha kwanza Ni utulivu tu . Simba waliweza kuumiliki mchezo vilivyo. Ndiyo maana kipindi cha pili walirudi wakiwa wameshusha presha na kumaliza mechi.

Duniani kila timu huwa bonasi zipo, si dhambi, Ni moja ya njia ya kuchochea ari na kujituma.

Ni ushamba, upumbavu, kutojielewa kudhani kwamba Kuna uchawi, kuhonga waamuzi ndiyo maana Simba inashinda. Simba wanapambana kwa jasho na damu kupata matokeo mazuri.

Kwakweli Ni kukosa heshima, shukrani na uchawi kusema jana simba ilicheza mpira mbovu. MPIRA MBOVU DHIDI YA UPI MZURI WA GENDARMARIE?

Labda useme SIMBA Ni mbovu kwa kutinga robo fainali na akina Asec Mimosas Ni bora ndiyo maana walitolewa.

Hakuna mtu anayeujua mpira atamsajili Mayele kwamba atakusaidia kwa mechi za kimataifa. Kwa NBC premier league hapo sawa na tena anastruggle sana kufunga goli.

Hakuna timu ya kuitisha simba kati ya hao Pirate's, Mazembe nk ishu ni kujipanga, kujifunza na kujua wanataka Nini. Uamuzi wa kupata matokeo bora robo fainali uko mikononni kwa Simba.

Wachache Walio bora kati ya wengi ndiyo wamefuzu kwa robo fainali , hivi ndivyo watu positive hufikiri. Zaidi sasa ukishafuzu Ni kujipanga,kucheza kwa Ari na mipango madhubuti.Naamini kabisa hao unaowaogopa hata wao wanaogopa kukutana na Simba.
Hivi mtu mwenye akili timamu anayeujua mpira anawezaje kusema Simba Ni MBOVU? Kuna lugha nyingine mtu anaweza kuitumia lkn si kusema Simba Ni mbovu.

Ukiondoa timu ya Orlando Pirates,Mazembe HAKUNA timu nyingine yyte ya East Africa, Central and South of Sahara iliyobaki KTK mashindano haya shirikisho km so simba.Yanga ,Azam,Biashara,Kenya wako wapi.

Simba ipewe heshima yake. Mwakani tunapeleka timu nne Tena,sababu Ni Simba Hii inaitwa mbovu. Yanga wana Cha kujifunza.Yanga wanafanya vzr ktk ligi lkn nikuhakikishie kile kikosi kikienda kimataifa km kilivyo hawatafurukuta wanahitaji usajili mzito Sana.

SIMBA ingetolewa Jana sijui leo ungeleta bandiko la aina gani km wamefuzu na umekuwa MCHAWI kiasi hiki.

Nakumbuka tangu mechi na RED ARROWS umekuwa ukipost uchawi tu, yaani huna jema wakishinda huna jema wakifungwa. Mliombea Sana Simba ifungwe KTK kila mechi,mkaomba Jana wasifuzu Bado mkaumbuka.

Angalia jinsi ulivyoanza bandiko lako kwa kupongeza halafu ukanza uchawi. TUNAJUA NI JINSI GANI MNAUMIA KWA MAFANIKIO HAYA SIMBA. TUNAJUA NI JINSI GANI DUA ZENU MBAYA ZINAFELI.

HAKUNA timu isiyo na weakness ktk eneo Fulani, ndiyo maana Kuna kusajili Kuna kuacha. Ila kwa wakati huu ni kushauri kwa mechi zinazokuja nini lifanyike kupata ushindi. Hao Mazembe siyo kwamba Ni bora Sana, Kuna wakati ubora haukusaidii bali mbinu na kujua unataka Nini.

SIMBA ikitolewa Ni matokeo tu ya mpira lkn si kwamba Ni timu mbovu. Hakuna timu mbovu inaweza kucheza makundi sembuse robo fainali.
Maelezo marefu yenye Pumba na Takataka tupu tu.
 
Hakuna mechi Simba imeshinda, watu wakakubali. Majungu kibao, lakini inasonga mbele tu!
 
Maelezo marefu yenye Pumba na Takataka tupu tu.
wanaelewa wenye ubongo. Popoma km wewe utaelewa nn nje ya box

Huna akili dadangu, hauko smart km unavyojidhania. Kuna watu smart humu. Wewe umekalia uchawi na ulozi tu.
 
Sijaona Mpira wa kutilia shaka kiasi hicho, sijajua wewe umeangalia kwa mtazamo upi.

Timu ipo..huyo Morrison angekuwa wa Genda Marie na jana wangetugalagaza leo hii ndio angekuwa wimbo hapa Bongo...sasa kama Watu kama hao tunao sisi wewe unaogopa nini?.
Huyu mtu ana matatizo ya akili mpira wote bado linalalamika tu.
 
Tusheherekee zetu tu kwa Kushinda jana na Kufuzu huko Robo Fainali ya CAFCC na kupata hicho Kitita cha Shilingi Milioni Mia Nane ( 800,000,000/= Tsh)

Ila kwa Mpira mbovu niliouona Jana huku Beki Onyango, Beki Tshabalala, Viungo Mkude na Kanoute na Washambuliaji Morrison na Sakho wakionyesha Utoto mwingi na Kunyimana Pasi na kutaka Sifa Binafsi za Kufunga GENTAMYCINE nakuwa wa Kwanza kusema kuwa Safari yetu ndiyo imeishia hapa.

Simba SC inaenda Kukutana na Moja ya Vigogo hivi viifuatavyo Barani Afrika hivyo ninaposema kuwa tunaishia hapa Robo Fainali kutokana na kuwa na Timu mbovu kwa sasa na yenye Kiwango kibovu hasa kwa Mechi za Kimataifa ninamaanisha.....

1. TP Mazembe ( Congo DR )
2. Orlando Pirates ( South Africa )
3. Al Ahly Tripoli ( Libya )

Najua kwa huu Uzi wangu msiotaka Ukweli, wapenda Unafiki na msio na Jicho la Kiufundi la Kimpira hapa mtanitukana na Kunidhihaki kwa kila namna na mpo pia ambao mtasema Mimi ni Yanga SC ila nasisitiza tena kuwa Mafanikio yetu yameishia Jana tu kwa kufika hapa Robo Fainali ya CAFCC lakini nina uhakika wa 100% kwa Simba SC hii ya sasa 'hatutoboi' kamwe hatua ya Nusu Fainali.

Na nakumbusha tu kuwa hizi Mechi za hatua Robo Fainali kati ya moja ya hizo Timu nilizozitaja hapo juu zitachezwa / tutacheza kati ya tarehe 15 hadi 17 Mwezi huu wa April na kurudiana tena kati ya tarehe 22 hadi 24 Mwezi April, 2022.

Timu inashinda kwa Morali tu ya Pesa kwa Ahadi za Mwekezaji na Rais wa Heshima Mohammed Dewji na Mambo yetu ya 'Kienyeji' hasa ya Nje ya Uwanja ila siyo kwa Kiwango cha Mpira kinachotakiwa na hata Kocha wa Simba SC hana Ubora na Uzuri huo na hatuna Wachezaji wa Kiushindani isipokuwa tunao tu hawa wa Kubahatisha ambao leo Moja wanatufurahisha lakini Mechi zaidi ya Tano ( 5 ) za Ligi au za ASFC au za Kimataifa Wanaharibu na Kurukaruka tu Viwanjani

Ushauri wangu wa mwisho kwakuwa nina uhakika kuwa Simba SC tunaenda kuishia tu hapa Robo Fainali nashauri tujikite tu zaidi huku katika NBC Premier League na kule ASFC ili tubebe Ubingwa ( japo katika Ligi Kuu ya NBC nina wasiwasi kama tutabeba ) na tukifanikiwa basi Uongozi wa Simba SC ufanye Maamuzi Magumu ya Kuachana ( Kuwatema ) Wachezaji wengi Wazawa na hata Wageni ( wasio na Hadhi ya Kuchezea Simba SC kwa sasa ) kisha Tusajili Wachezaji mahiri na wa uhakika kweli kama ambao baadhi yao wapo kwa Watani zetu Yanga SC mfano wa akina Beki Kiraka Yanick Bangala, Kiungo Fundi Khalid Aucho na Mshambuliaji hatari Fiston Mayele ( wa Nje ) na akina Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Feisal Salum Fei Toto ( wa Ndani )

Kila Ia Kheri Mechi yetu na Coast Union FC katika Ligi Kuu ya NBC tarehe 7 April, 2022 na Mechi ya Police Tanzania Wikiendi hii ijayo na tugangamale kweli katika Mechi zetu zote za Ligi Kuu na hata Kombe la ASFC kwani kwa hatua za sasa hakuna Kulala wala Mzaha tena kwani kwa Upinzani mkubwa uliopo na jinsi Yanga SC ilivyo na Kiwango kikubwa na cha Hatari ( huku wakiwa wamejipanga vyema ndani na nje ya Uwanja ) kuna uwezekano pia ambao GENTAMYCINE nauona wa Wao ( Yanga SC ) kubeba Ubingwa ( Makombe ) yote haya na Simba SC yetu ( yangu ) kwa Msimu huu tukabaki na Mafanikio ya Kubeba Kombe la kuishia tu Robo Fainali ya CAFCC.

'Ukweli' huuma, ila ni 'Dawa' inayotibu!!!

Cc: Mzizi wa Mbuyu
Mechi za ligi ni tofauti sana na mtoano (knock out), kwenye knockout stage kinachotakiwa sio mpira sambusa bali mbinu za kumzuia mpinzani asikufunge. Mfano mzuri no Atletico Madrid ya Diego Simone, hubadilika kulingana na mahitaji ya mchezo husika.

Kwenye hatua ya knockout, Atletico Madrid hufanya kazi ya kuziui zaidi kuliko kushambulia.

Vv
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom