hivi kweli hakuna uwezekano wa kuvichapisha hivyo vitaabu hivyo, ? maana nakumbuka sana vitabu hivyo,kwa sisi tuliosoma hapa Dar es salaam, kama hukuweza kukariri maneno aliyoyasema Umslopagasi wakati analinda ngazi kuu , wewe ulikuwa unahesabiwa kama wakuja, maneno yenyewe ni kama yafuatayo naomba mutanisamehe kwani kipindi kirefu kimepita na baadhi yake nimeyasahau, Alisema hivi, ''mimi gota gota,mimi muuaji,mimi mwenya mbio, mimi mwenye damu ya mfalme Chaka,nasikia harufu ya damu, nani anataka kulibusu shoka langu?''' SASA MANENO MENGI NIMEYASAHAU MWENYE KUKUMBUKA TUKUMBUSHANE, pia palikuwa na vitabu vinginevyo kama safari za Gulliver, Elisi katika nchi ya ajabu, Alfu lela u lela, Animal Farm,nk:redfaces::redfaces::redfaces::redfaces::redfaces::redfaces::redfaces: