companero na kile cha Juma na Roza kama unacho, niazime kiongozi
Bila shaka kiongozi.Hicho sina mkuu, ukikipata nimuvuzishie.
Bila shaka kiongozi.
Kuna kijitabu kingine nakumbuka kilikuwa na shairi moja hivi:
Mgeni siku ya kwanza mpe chele na.....(nimesahau mboga), siku pili...., siku ya tatu mpe jembe akalime
Ewaaaa, ni Bulicheka na mkewe, ngoja niingie mtandaoni, shukrani mkuu!Nadhani hicho ni cha kina Bulicheka na Mkewe Lizabeta pamoja na Makari Hodari, ila hilo shairi lipo mtandaoni - ligugo.
Ewaaaa, ni Bulicheka na mkewe, ngoja niingie mtandaoni, shukrani mkuu!
wewe ni mtoto mtukufuuuuuuu aliposema neno mtukufu akapulizia chai fuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. wazazi wako wanakusifuuuuuuuuuu waliposema wanakusifu akapulizia chai fuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!Wakuu posts zote hapa zimenisisimua sana. Watoto siku hizi hawafaidi. Darasa la sita kama sijasahau kitabu cha Kiswahili kilikuwa na sura "Kutembelea Uwanja wa Ndege." Tulipata nafasi ya kutembelea uwanja wa ndege kutokana na juhudi binafsi za Mwalimu wetu Emmanuel Mbelele. Napenda kuonesha shukrani zangu kwake. Naamini nimekuwa na wakati mzuri sana katika maisha ya utotoni. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa ofa hii.
Asante mkuu, hata sisi wa miaka ya mwanzo ya 2000 tuna ruhusiwa?Poa, karibu kwenye tukio hili la kujikumbushia hayo:
For those who lived in and around Chuo (Mlimani) in the 80s and 90S karibu kukutana na marafiki wa zamani. Nyama choma, drinks, football, music, kids corner etc
inaitwa msindi kubong'oaMichezo mingine bana daaaah.....mtu unainama kuokota kitu jamaa anakuja anakupiga bonge la teke kwenye makalio.....
ilikuwa inaitwa dabali (kutokana na neno double)unavaa kaptula 3 kukwepa bakora zisikuingie mwilini tena za jeans au unaweka maboksi na makaratasi kwenye makalio duh!zamani bakola zilikuwa zinatembea sana!
nakumbuka kuna jamaa lipewa adhabu na mwl ya kumwagilia maua hadi palie vyura kwa siku hiyo hiyoukiwahi unakimbilia kuchota maji mtoni then kumwagilia mchicha na maua mwalimu anapima kwa kuchomeka fimbo kama kimelowa sasa ole wako aone hakijaloana maji hayajafika chini pia tulikuwa tunaagizwa mbolea ya mavi ya ngombe,kuku na mbuzi pia udongo uliooza na miradi ya shule kuuza mapera ya shule dah!enzi hzo ilikuwa raha sana!