Hebu jikumbushie 'Siku ya Gulio Katerero'

Hilo somo la siasa nililichukia sana hata walipoliremba kule sekondari wakaliita civics na high school GS....

Wewe sasa ni wa Juzi tu! Wala huwezi jiringanisha na hao jamaa wanaoleta hadithi za kina Manenge na Mandawa, Wazazi wako wankusifuuuuuuuuuuuuuuu! Angalia hao Siafuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!! Kila Kazee kakisema fuuuuuuuu kanapoza chai wewe!!!!!! Maana jina la Civics limekuja juzi tu jamaa yangu enzi zile tulikuwa tunaita Siasa tu hata Sekondari.
 
Sizitaki mbichi hizi
Kambi ya Kaboya
Mpiga filimbi wa Hamelini
Hadithi za Kiingereza: The story of Mkisi; The Scout master's camera;

Du acha tu enzi hizo.
Jamani kuna mtu aliyesoma Boma Primary School Korogwe, miaka ya 1983-1986.Kuna mwalimu mmoja alikuwa anaitwa Mwl Kimushu natamani sana kumwona nimpe shukrani zangu kwa kazi yake nzuri kipindi hicho, nategemea kwenda huko mwezi December mwishoni na nitapita Korogwe kwa nia ya kumtafuta, kama kuna mtu anamjua alipo au contact zake ani PM tafadhali.
 
ama kweli. leo nimeamini kwamba humu ndani ni watu wakubwa. kama mnakumbuka enzi hizo za themanini na...duh jamani. hebu sikia hii, "karudi baba mmoja, toka safari ya mbali, kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili, watoto wake wakaja ili kumtaka hali.........au wakati wa mchakamchaka, ' alisema, alisema, alisema nyerere alisema, vijana wangu sasa mmeregea, sharti tuanze mchakamachaka......
 
mchaka mchaka , binti seleman wa kongo e kapika ugali na ngogwe kala na mwanaye seleman katubakizia makombo ee mwambie eee eee ajue basi hapo mnaaza kumnanga mwalimu na kiongozi wa zamu du marshal ya skonga si mchezo
 
Kwa wale ambao hawajafika huko siku ya gulio Katerero inakuwa kama inavyoonekana kwenye picha.

KATERERO.JPG
 
[/COLOR]



1. Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja
2. Sitapokea wala kutoa rushwa
3. Nitajitolea nafsi yangu....................
4. ............
5. ............
6. ............
7. .............
8. ............
9. ............
10. ...........

Jamani anayezikumbuka atuwekeeeeeeeeeeeeee hapa!!!!!!!!
4. Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko.
5. Nitashilikiana na wenzangu wote-kujenga nchi yetu.
6. Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa rushwa.
7..............
 
Shule za Msingi ( UPE )Category:Common Interest - HistoryDescription:
Ushawahi kusoma shule za kukimbia mchakamchaka, kwenda na kidumu cha maji na mfagio mkononi? Kama ndio basi kundi (Group) hili linakufaa.

Hebu jikumbushie haya:

1. Bulicheka na nduguze
2. Mr. & Mrs. Daudi
3. Fikiri na Sadiki
4. Linda amwokoa Kapilima
5. Siku ya gulio katerero
6. Tola anakula gizani
7. Twende tukawinde Ngedere
8. Kibanga ampiga mkoloni
9. Nanzoge anapika.
10. Mafuriko ya mto Rufiji
11. Pazi na jogoo

Waweza ongezea na wewe.

Kama ulisoma academy school, huambulii...
Lazima ujifunze:

1. Sayansi Kimu
2. Uraia
3. Sanaa

Wakati wa mapumziko lazima ucheze,

1. Mpira (Chandimu, one touchi, mputo)
2. Netboli na rede
3. Mdako
4. Bong'oa
5. Kula m'bakishie baba
6. Kubanjua Gololi

Msosi wakati wa mapumziko.

1. Mihogo ya kukaanga na chachandu
2. Aishiklimu
3. Barafu
4. Kashata
5. Bagia (za walimu)

mkuuuuu! wewe ni jembe, umenisisimuaaaa

matete na mpapai
mbu na tembo
pazi na jogooo
musa na neema aiseeee ilikua raha iliyoje
 
Nimekumbuka mbali sana,sijui kwanini licha ya kusoma vitabu vizuri na vyenye mafundisho kama haya kizazi hicho kimezalisha mafisadi wengi!
 
Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
Wakataka na kauli iwafae maishani

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa, kifo kinanikabili,
Kama mnataka mali, mtayapata shambani

Wakazidi kumbana , baba mwenye homa kali
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili
Akili yetu nyembamba, haijajua methali
Sema ipo wapi mali, itufae maishani.

Ninakufa masikini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, mwisho mtapata mali
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali.

..............................
................................
..............................



ZILIPENDWA HIZI WAJAMENI SIZIKUMBUKI VIZURI KWANI NI ZAIDI YA MIAKA 30 IMEPITA TOKA NILIPOZISOMA PALE SHULE YA MSINGI TANGANYIKA PACKERS KAWE DSM; LEO WANAIITA S/ M KAWE "B"!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Hapo kuna kuwahi number asubuhi,ukaguzi siku ya alkhamisi na band ya shule.

Unankumbusha mbali sana coz kuna watu tulikuwa hatuwezi kuwahi number;so tunasubili mpaka kipind cha kwanza kinaisha then tunapisha madaflali kupitia dilishan then unaingia as if umetokea toilet (ilikuwa late 1990's,Nyamagana shule ya msingi)
 
Musa na Neema drs la tatu hadi la saba ule mwendelezo ulikuwa bomba sana,

Jiografia dar la nne, kilimo cha karanga Dodoma, kilimo cha mhogo mtwara, unaisoma Tanzania nzima unajua kila mkoa inalima nini,

Kuwahi namba saa moja kamili asbh, hapo una jembe, mfagio, kidumu cha maji, maua, mbolea

Watoto wa siku hizi gari linamfuata mlangoni

Kiuweli nimekumbuka mbali sana...... Brown ashika tama
 
JAMANI NILIKUA NAOGOPA ADHABU YA KUSHIKA MASIKIO. YAANI ILIKUA NI AFADHALI NICHAPWE TUU MBAKOLA, LAKINI SIO HIYO ADHABU. JE ILE YA KUNYANYUA MIKONO JUU HUKU UMEPIGA MAGOTI KWENYE KOKOTO...YAANI TULIKOMAGA ENZI ZETU..LOOOO!:A S cry:
 
mkuuuuu! wewe ni jembe, umenisisimuaaaa

matete na mpapai
mbu na tembo
pazi na jogooo
musa na neema aiseeee ilikua raha iliyoje

samahani mkuu, hapo kwenye pazi na jogoo ni Jogoo aliyesema- kitabu hicho kilinifanya niogope majogoo hadi leo!
 
Back
Top Bottom