Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,183
- 10,913
Iran kupitia kwa wizara yake ya mambo ya nje imesema Marekani imefanya kosa kubwa sana la kimkakati kwa kushambulia maeneo ya Iraq na Syria.
Kwa upande wa Iraq imesema haitaki nchi yake iwe ni uwanja wa kujibizana mahasimu na kwamba inataka majeshi ya Marekani yaliyobaki yaondoke haraka nchini humo.Zaidi ya hapo waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo amesema kupiga maeneo ya nchi hiyo ni kukiuka haki na mamlaka ya kiinchi.Papo hapo Iraq kupitia waziri huyo imekanusha madai ya Marekani kwamba walitoa taarifa kabla ya kuanza kushambulia vituo inavyodai vina wapiganaji wanaofadhiliwa na Iran.
Syria kufuatia mashambulio hayo imesema hali ya Marekani kuikalia nchi yao haitoachwa iendelee.
Ama kwa upande wa Houth wa Yemen wamesema hasira zitajibiwa na hasira zaidi na kwamba hawataacha kushambulia meli za wachokozi mpaka hapo Israel itakaposimamisha vita huko Gaza.