Marekani imeshaamua kupiga Syria na Iraq. Inasubiri hali ya hewa tu iwe safi ianze kazi

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,183
10,921
Raisi Biden wa Marekani na wasaidizi wake wametangaza kuwa mipango yote ya kupiga vituo vya Iran ndani ya Syria na Iraq imekamilika.Kinachosubiriwa ni hali ya hewa tu iwe rafiki kwa kile walichodai kukwepa kusababisha madhara kwa raia.
Na sisi walimwengu tunasubiri tuone athari ya vita hivyo na kwamba jee Iran itakaa kimya tena kwa kushambuliwa maslahi yake kwenye nchi hizo.
Tunachosubiri tena ni kuona iwapo Syria itatumia ile mitambo yake ya S400 kujilinda na mashambulizi ya anaga kutungua angalau ndege moja ya Marekani itakayoingia kwa jeuri nchini mwake.

US approves plan to strike Iranian targets in Syria and Iraq, officials say

1706848365060.png
 
Ngoja tuone....nini kitajiri huko mashariki ya kati..
Ni muendelezo wa vita vitakavyosambaa bila kutarajiwa.
Uamuzi huu wa Marekani na serikali ya Biden ni wa kisiasa zaidi kuelekea uchaguzi mkuu.
Kwa sababu Marekani imeshambuliwa mara nyingi na kufa askari wake zaidi ya hao watatu kule Iraq na haikufanya kitu.
Kwa upande mwengine muda inaochagua kuanza kujibu mapigo si rafiki kutokana na hali ya vita vinavyoendelea Gaza.Kunaweza kukatibua hali vibaya dhidi ya Israel na waliokuwa wamekaa kimya kama Misri na Jordan wakapata maeneo ya kuanza kuingilia kati.
 
Hayo mataifa mawili hayawezi ingia kabisa.....
 
Misiri haiwezi kujiingiza kwenye vita ambayo USA yupo tayari....USA itafanya kama alivyoplan hakuna vi nchi vya kutibuliwa bali nchi kama RUSSIA inaweza kupeleka askari wake kisiri sana huko Syria.
 
Raisi Biden wa Marekani na wasaidizi wake wametangaza kuwa mipango yote ya kupiga vituo vya Iran ndani ya Syria na Iraq imekamilika
Na sisi walimwengu tunasubiri tuone athari ya vita hivyo na kwamba jee Iran itakaa kimya tena kwa kushambuliwa maslahi yake kwenye nchi hizo.
Mbona maslahi yake yanashambuliwa kila siku? Hamna vita hapo, hakuna anayetaka vita kwa sasa.Hapo ni mchezo wa kuigiza kuridhisha wapiga kura na kujivua aibu.

Kinachokuja ni kilekile kama alivyouawa yule kamanda wa Iran! Yaani ni maigizo!
 
Ni maigizo kweli.
Kama kuna siku Marekani ilipigwa ni pale kambi nzima iliposambaratishwe kule Iraq baada ya kifo cha kamanda Sleyman mwaka juzi.Na wala hakujibu chochote.
 
Raisi Biden wa Marekani na wasaidizi wake wametangaza kuwa mipango yote ya kupiga vituo vya Iran ndani ya Syria na Iraq imekamilika.Kinachosubiriwa ni hali ya hewa tu iwe rafiki kwa kile walichodai kukwepa kusababisha madhara kwa raia.
Na sisi walimwengu tunasubiri tuone athari ya vita hivyo na kwamba jee Iran itakaa kimya tena kwa kushambuliwa maslahi yake kwenye nchi hizo.
Tunachosubiri tena ni kuona iwapo Syria itatumia ile mitambo yake ya S400 kujilinda na mashambulizi ya anaga kutungua angalau ndege moja ya Marekani itakayoingia kwa jeuri nchini mwake.

US approves plan to strike Iranian targets in Syria and Iraq, officials say

View attachment 2891375
Mara ngapi? Waliimpiga Sadam hussein hivi sasa wanajuta. Waislam hawana silaha lkn dua zinawaangamiza maadui
 
Raisi Biden wa Marekani na wasaidizi wake wametangaza kuwa mipango yote ya kupiga vituo vya Iran ndani ya Syria na Iraq imekamilika.Kinachosubiriwa ni hali ya hewa tu iwe rafiki kwa kile walichodai kukwepa kusababisha madhara kwa raia.
Na sisi walimwengu tunasubiri tuone athari ya vita hivyo na kwamba jee Iran itakaa kimya tena kwa kushambuliwa maslahi yake kwenye nchi hizo.
Tunachosubiri tena ni kuona iwapo Syria itatumia ile mitambo yake ya S400 kujilinda na mashambulizi ya anaga kutungua angalau ndege moja ya Marekani itakayoingia kwa jeuri nchini mwake.

US approves plan to strike Iranian targets in Syria and Iraq, officials say

View attachment 2891375
Mbona wanazunguka sana waogopa kuingia moja kwa moja

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ni muendelezo wa vita vitakavyosambaa bila kutarajiwa.
Uamuzi huu wa Marekani na serikali ya Biden ni wa kisiasa zaidi kuelekea uchaguzi mkuu.
Kwa sababu Marekani imeshambuliwa mara nyingi na kufa askari wake zaidi ya hao watatu kule Iraq na haikufanya kitu.
Kwa upande mwengine muda inaochagua kuanza kujibu mapigo si rafiki kutokana na hali ya vita vinavyoendelea Gaza.Kunaweza kukatibua hali vibaya dhidi ya Israel na waliokuwa wamekaa kimya kama Misri na Jordan wakapata maeneo ya kuanza kuingilia kati.
vita vitakavyo sambaa unamaanisha kusambaa mitandaoni aka kutrend au kasambaaje ?
 
Watapigwa tu na hakuna kitu Iran atafanya kwa sababu Iran, sawa na nchi yoyote duniani, haina ubavu wa kufunga virago na kwenda karibu na pwani ya Marekani na kisha kuishambulia Marekani.

That will never happen till the end of the world.
Hilo la kuwa mbali ndio sababu ya kiburi cha Marekani.Hata hivyo watu wameshajua dawa yake na imeanza kutumika.
Moja ya dawa hiyo ni kupambana na meli zake za kibiashara na za kivita zinazopita karibu yao.Hilo lina athari kubwa kwa uchumi wa Marekani na ikiendelea kwa muda kule Marekani hakutokalika wala kutawalika.
 
vita vitakavyo sambaa unamaanisha kusambaa mitandaoni aka kutrend au kasambaaje ?
Kusambaa kutokana na uchokozi.
Huyu atachokozwa kwa namna moja na mwengine kwa namna tofauti mpaka kila mmoja ataanza kuingia vitani ili kujitetea au kulinda maslahi yake.
 
waarabu hawasapotian mkuu iraq anapigwa majirani zake wanatoa military base kiufupi nilichojifunza saivi ukiingia matatizoni ni lazima ujue uko peke yako ukrain anapigwa nato wanatoa support ya mchongo
 
Back
Top Bottom