6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 1,827
- 4,084
Wakuu vipi, kwema.
Nimefuatilia kwa makini mambo yanayoendelea duniani, nikagundua kwamba Marekani na Tanzania yetu kuna baadhi ya mambo huwa tunafanana haswa kwa upande wa mambo ya kufukia mashimo.
1) Nikianza na Taifa kubwa Marekani:
Hawa jamaa baada ya kusikia kuwa kuna mzozo mkubwa umezuka huko Mashariki ya kati, kati ya vikosi vya Israel na Palestina. Marekani wakaamua kuja na scandal la uvujishwaji wa nyaraka za siri ili kuwatoa watu kwenye mood ya kutaka kujua ni hatua gani taifa hilo lenye nguvu, na ushawishi mkubwa duniani litachukua dhidi ya yale yanayoendelea huko Mashariki ya kati.
Ikumbukwe Marekani ndio hujifanya kiranja wa kila kinachoendelea hapa duniani. Kwahiyo kitendo chake cha kukaa kimya without to say anything, or to do something kitafanya watu waone kuwa USA inaunga mkono yanayoendelea huko Mashariki ya kati. Sasa ili kufunika kombe ili mwanaharam apite, ndo likaanzishwa zengwe la nyaraka za siri na mpango sijui wa kumuua Putin, nyaraka za kijeshi nk ili watu waanze kuwa busy kuzijadili nyaraka za kumuua Putin badala ya kile kinachoendelea huko Mashariki ya kati.
2) Nikimalizia na nchi yetu Tanzania:
Nayo iko vizuri katika medani ya ufukiaji wa mashimo, haswa linapokuja swala la kuikaba koo serikali au chama tawala (ccm)
Ndo maana baada ya mh CAG kuja na kile kinachoonesha kuwa kuna ufisadi mkubwa umefanywa na watumishi ambao waliaminiwa na serikali, hadi kupelekea hali ya hewa kuchafuka nchini. Sasa game limegeuzwa ambapo sasa hivi mada zinazojadiliwa kwa nguvu zote ni zile zinazohusu ushoga, huku hili la waliochota mabilioni ya shilingi likionekana kufifishwa kwa nguvu kubwa kutoka kusikojulikana. Pia na hii lengo lao ni lile lile la kufunika kombe ili mwanaharam apite.
Haya ngoja tuone mwisho wa haya yanayoendelea kwa Marekani na Tanzania yetu.