Haya ndio maisha halisi ya familia zetu hasa msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka

Mkyamise

JF-Expert Member
Apr 14, 2014
454
555
Jinsi ya kujitambua kuwa wewe ni paratrooper msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya

1. Ni pale vikao vya familia vitakapoanza bila kujali uwepo wako na vikaweza kuendelea hata ukisusa.

2. Ni pale utakuwa mtu pekee atakayehitajika wakitaka kuchinja mbuzi au kufanya shughuli yoyote inayohitaji nguvu bila akili .

3. Endapo meno yako ndio yatageuzwa kuwa official family soda/ beer opener.

4. Pale utakapotafutwa endapo chizi atavamia makazi yenu

5. Endapo hutajulishwa ukiendeshwa mchago wowote wa dharura kwa kuwa huna cha kuchangia.

6. Endapo wageni wote wanatoka mjini kuja kijijini likizo na kukukuta wewe upo tu kijijini siku zote permanently on holiday. Everyday is your holiday. In fact you badly need a holiday from the endless holidays.

7. Endapo wewe ndiye utakayetakiwa kupanda mti wa mparachichi kuwatungulia maparachichi watoto wa ndugu zako waliotoka mjini.

8. Endapo utapewa ufunguo wa gari na mdogo wako akikuambia braza katuletee kreti tatu za bia mchanganyiko, konyagi ndogo nne bila kusahau K-Vant kubwa. Uwe makini usigonge migomba

Msimu mwema wa sikukuu Paratroopers
 
Tuseme tu ukweli hizi sikukuu za mwisho wa mwaka ni maneno tu wanaozifaidi ni wachache.....

Mimi naona za waislamu ndo zinabamba zaidi(ni mtazamo tu, sio kwamba naleta udini)
 
Nashindwa kuelezea,

Za waislamu hazijakaa kipesa pesa sijui kutoka out, kula beer....

Ndo maana kuna wakristo wanapata stress mda wa sikukuu mambo ni mengi.....

Afu misosi yao ni mizuri

Mimi ni mkristo ila sijawahi kufurahia christmas

Sahihi, ubepari unashika usukani siku baada ya siku hata waislamu nao wamesha ingiwa na hiyo mifumo.

Siku hizi hata kushare vyakula mwezi mtukufu sio sana kama miaka ya nyuma
 
Back
Top Bottom