Kwako Mheshimiwa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan
Kwa Heshima na taadhima, na kwa unyenyekevu mkubwa, naleta ombi kwako wewe Mheshimiwa Rais, utusaidie kuondoa ukali ya mgao na ukosefu wa umeme angalau katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka. Baada ya kuteseka sana na mgao mkali wa umeme karibu mwaka mzima nadhani zawadi bora kabisa ya sikukuu unayoweza kuwapatia wananchi wako ni upatikanaji wa uhakika wa umeme angalau katika kipindi hiki sikukuu za Xmas na Mwaka mpya.
Wanachi wako wengi hawako kazini katika kipindi hiki, wengi pamoja na familia zao wako mapumzikoni hivyo ni muda mzuri kwa wao kuwa pamoja na familia zao wakifurahia mapumziko yao, lakini ukosefu wa umeme unawafanya wawe wanyonge, wawe na huzuni na wajikute wakiwa hawana kitu cha kufanya kutokana na kukosa umeme.
Ukosefu wa umeme umeanza kujenga chuki na hasira kutoka kwa wananchi dhidi ya serikali yao na hali hiyo huenda ikazidi kama hali ya umeme itaendelea kuwa hivi.
Mengi yameshasemwa kuhusu sababu, mikakati upembuzi yakinifu ya kuboresha umeme lakini kwa sasa watu hawataki kusikia maneno hayo tena, wamechoka wanachotaka ni umeme uwepo majumbani mwao
Nawasilisha.