seemz una uelewa na hayo mambo hebu nielekeze Jellyfish anaweza kutokuwa na ubongo akasurvive!?..
Nikimaanisha kujikinga na maadui, kuemploy flight technics kuwakimbia, kujua strategy gan aitumie na kwa wakati gani as naamini hivyo vitu vinachakatwa kwenye ubongo kwanza!.
Swali lako lina jibu refu mno ili tuelewane, ila nitajitahidi kufupisha kwa kadri ya nitakavyoweza ili mradi tu uelewe ama upate japo mwanga.
Kibaiolojia viumbe hai tuna kazi au majukumu "matatu tu ya msingi";
1. kula (feeding)
2. Kutokuliwa / kutogeuzwa chakula cha mwingine. (defense)
3. Kuhakikisha kizazi chenu mnazidi kuwepo duniani/kuzaliana (reproducing)
katika kuyatimiza hayo, kazi ya mfumo wa fahamu/neva (nervous system) ni kusaidia mwili wa kiumbe kujitambua wenyewe na kuyatambua mazingira yake, yaani kuhisi adui yako yuko wapi ili umuepuke, kuhisi mwenza wako yuko wapi ili umfikie mzaliane na pia kuhisi chakula chako kiko wapi ili ule.
Mazingira unayoishi ndio yataamua aina ya chakula na aina ya maadui zako na hivyo kuamua utata wa mfumo wako wa fahamu (complexity of your nervous system). Mfumo wa fahamu wa kiumbe unaweza kuwa rahisi ukihusisha neva chache pekee au ukawa tata ukihusisha mamilioni ya neva, "ubongo" na "uti wa mgongo".
Ubongo ni nini ?
Kwa kifupi, ubongo ni mkusanyiko wa neva za fahamu zinazofanya kazi pamoja kama kiungo kinachoratibu mambo yote ya utambuzi na maamuzi katika mwili wa kiumbe. Mkusanyiko huo hufanyika sehemu ya juu au ya mbele ya kiumbe hali ambayo inapelekea sehemu hiyo kuitwa "kichwani". Kitendo cha neva kukusanyika (concentration of nervous ganglia) upande wa mbele/juu wa kiumbe (tunakokuita kichwani) na kutengeneza kitu kinachoitwa "ubongo" kwa lugha ya kiingereza kitendo hicho kinaitwa "Cephalization".
Jellyfishes are not cephalized. Kwahiyo hii ni kusema kwamba hao viumbe wanao mfumo wa fahamu, lakini hawana "ubongo". Mfumo wao wa fahamu una neva zilizo tandaa (kama nyuzi za chandarua vile/net like nerves) na hizo ndizo zinamsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku.
Sababu za kuwa na mfumo rahisi wa fahamu ni kwamba kwa mujibu wa maisha yake na mazingira yake huo mfumo ndio unaomfaa. Hii ni kwa maana ya kwamba, anaweza kuzaliana kwa njia zote mbili "sexually" na "asexually", anaweza kuishi katika njia mbili za vizazi (two alteration of generations) kati ya "medusa" na "polyp", ana uwezo wa kutoa sumu kwa ajili ya kuwashughulikia maadui zake, namna ya ulaji wake ni kula kwa kufyonza (filter feeder) hakumtaki ahangaike sana kukimbizana na "vitoweo" na mengineyo mengi.
Ninadhani kwa kiwango fulani nimejibu swali lako.