Hawa ndio wanyama 10 wenye akili duniani

Hawa ndio wanyama 10 wenye akili duniani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,672
1.SOKWE

Great-Ape.jpg

Sokwe ni viumbe wa pili kwa kuwa na akili zaidi baada ya binadamu. Kwa mujibu wa uchunguzi wa kisayansi, binadamu alitoka katia familia ya sokwe ambao ni pamoja na nyani, kima, tumbili, na kadhalika.
Sokwe wana uwezo mkubwa wa kuwasiliana, kufahamu mazingira waliyomo, kujenga makazi yao na kutumia zana katika kutafuta chakula chao, wanaweza kujifunza maneno na lugha ya binadamu na hujilinda kwa kutumia zana mbalimbali.

2. POMBOO

dolphin-playing-ball_1600.jpg

Pomboo ndiyo wanafuatia. Ni wanyama ambao binadamu huwatumia kutatua matatizo mengi hususan ya baharini. Akili ya pomboo ni kubwa kama miili yao, huonyesha hisia mbalimbali, hujifunza vyema mazingira yao, nusu tu ya akili yake hulala, nusu nyingine ikiwa macho kukabiliana na tishio lolote

3. TEMBO

Elephant.jpg

Tembo wana akili kubwa kuliko mnyama yeyote wa ardhi kavu. Huonyesha akili nyingi kijamii na ni moja ya marafiki wakubwa wa binadamu. Hujifunza mazingira yao, hutambua milio mbalimbali, huonyesha furaha, hucheza na kusikitika. Huigiza pia sauti mbalimbali na hutafuta chakula kwa kutumia zana.

4. NYANGUMI

Whale.jpg

Wana uwezo mkubwa wa kutumia akili zao katika kuwasiliana na kuigiza sauti mbalimbali, mambo yanayowafanya kuwa wanyama wenye akili zaidi. Ni watulivu, wanapenda kusafiri na kuwinda.

5. MBWA

Dog.jpg

Ni marafiki wakubwa wa binadamu, ambapo mbwa wa kawaida ana akili kama mtoto wa binadamu mwenye umri wa miaka miwili. Wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu, kujilinda, na kujifunza kutoka kwa binadamu.

6. PWEZA

Octopus.jpg

Pweza ni viumbe wenye akili zaidi miongoni mwa wale wasio na auti wa mgongo. Wana uwezo mkubwa wa kujua maadui, mnyama pekee wa kundi hilo kutumia zana, hujibadili kukwepa maadui.
Mfano mzuri ni Pweza Paulo aliyetabiri Hispania kuchukua kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

7. NGURUWE

PIG.jpg

Mmoja wa wanyama wenye akili nyingi, hupenda kucheza na kushirikiana na viumbe wengine, wana uwezo mkubwa wa utambuzi kuliko mbwa, huenda kuishi pamoja, ana uwezo wa kurejea nyumbani hata akiwa mbali, hutambua sauti za viumbe wengine kiurahisi.

8. FISIMAJI

Fischotter_Lutra_Lutra.jpg

Ni wanyama wadogo zaidi wa majini wanaoishi majini na nchi kavu, hutumia mawe kutafutia chakula na kuondoa sehemu za samaki na kaa wakati wa kuwala, wana uwezo wa kutambua sauti za adui.

9. KUNGURU

Crow.jpg

Hawa wamezagaa duniani kote, hawawapendi binadamu na huwafanyia fujo wanapoweza, wana akili kubwa ya kutafutia chakula, miongoni mwa ndege wenye akili zaidi, wanatambua kirahisi mavi ya binadamu, wanaweza kuvunja nazi kwa kuiangusha kwenye mawe, hutumia mawe kushambulia maadui na kushambulia ndege wengine.

10. MCHWA

Ant.jpg

Hawa hawana akili kubwa, wamekuwepo tangu enzi za wanyama ‘dinosaur’ walipokuwa wanaishi, wana akili ndogo zaidi miongoni mwa viumbe mbalimbali. Walianzisha mfumo wa kilimo miaka milioni 50 kabla ya binadamu kwa kupandikiza na kukusanya chakula. Mchwa anaweza kubeba kitu kikubwa mara 50 zaidi ya mwili wake kutokana na misuli ya nguvu aliyo nayo.
 
Mkuu asante kwa uzi mzuri. Ila majina ya Kiswahili sio ya mchezo , Bora ungeweka na kiingereza kwenye mabano kidogo maana huyo Fisi maji na huyo Pomboo kweli sijawahi kusikia hilo jina.
Pomboo kwa kizungu anaitwa DOLPHIN
 
Miaka milioni 6000 imefika na kuisha lini? Duh

Mkuu, umri wa dunia ni miaka bilioni kadhaa, umri wa "maisha" hapa duniani ni mamilioni mengi sana ya miaka, hivyo, japokuwa sina hakika na idadi ya miaka ya kuishi kwa hao viumbe kama alivyotanabaisha mdau hapo juu, nakuhakikishia uwezekano wa kuishi miaka hiyo upo maana maisha yamekuwapo kwa miaka mingi sana.

Hii unaambiwa huu ni mwaka 2018, ni mfumo tu wa kuhesabu miaka kikalenda lakini ukweli ni kwamba kumekuwapo na maisha kwa miaka mingi sana zaidi ya ''hutu tumiaka buku mbili"
 
Back
Top Bottom