Hawa ndio wanyama 10 wenye akili duniani

Hawa ndio wanyama 10 wenye akili duniani

Mnyama = Animal.
Animal is any member of kingdom Animalia.

Mchwa anapatikana Kingdom Animalia, phylum arthropododa, class insecta.

Kwa maelezo hayo mafupi, ya juujuu na ya jumla jumla, ninayo furaha kubwa kukujibu mbele ya hadhara hii, kwamba hakika Mchwa ni mnyama.
Hahaaa
 
Viumbe hai viko vya aina mbili, wanyama na mimea kama mchwa siyo mnyama ni mmea?

Kwa ''lugha ya kumuelewesha" mtu kuhusu mchwa uko sahihi, lakini kwa uhalisia wa dhana ya viumbe hai, hauko sahihi, ni zaidi ya hayo makundi mawili (wanyama na mimea) kama ulivyoeleza hapo juu. Kwa sasa tunaweza kusema yapo makundi matano ya viumbe hai. Pamoja na hayo mawili uliyoyataja pia kuna kundi "Monera, fungi na protoctista.'' Makundi hayo Matatu yanahusisha zaidi "vijidudu'' ndio maana kwa hali ya kawaida yanakua yanasahaulika kwenye stori za haraka haraka za viumbe hai.
 
Na wakati leo tuko 2018[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Mfumo wa kuhesabu miaka kwa kuongezeka yaani mwaka 1,2,3,.......2017,2018 umeanza mara baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kabla ya hapo kulikua na mfumo tofauti wa kuhesabu miaka na ulikua ni wa kupungua yaani ....10,9,8,7.....

Kimsingi miaka tunayoitumia sasa ni miaka ya Yesu (angekuwapo anaishi Duniani hadi leo, angekua ni mzee mwenye umri wa miaka 2018).

Kufikiria hakukua na maisha kabla ya mwaka 0 (mwaka aliozaliwa Yesu Kristo) ni kusema kwamba hakuna bikira Maria, hakuna Joseph Hakuna...... Yaani unakua unajiaminisha kwamba Yesu alijizaa mwenyewe au alizaliwa na Maria ambaye walizaliwa siku moja/mwaka mmoja na pia unajiaminisha kwamba Yesu ndiye mwanadamu wa kwanza kuishi hapa Duniani.

Na hata kama ingekuwa hayo hapo juu ni kweli, bado ushahidi wa kibailojia, kijiografia na pengine kibiblia vyote vinaonyesha kwamba binadamu ni moja kati ya viumbe wa mwisho mwisho kuikalia dunia.

Baina ya viumbe, "Wenyeji wetu" ni wengi mno kuliko wageni wetu.
 
Kwa ''lugha ya kumuelewesha" mtu kuhusu mchwa uko sahihi, lakini kwa uhalisia wa dhana ya viumbe hai, hauko sahihi, ni zaidi ya hayo makundi mawili (wanyama na mimea) kama ulivyoeleza hapo juu. Kwa sasa tunaweza kusema yapo makundi matano ya viumbe hai. Pamoja na hayo mawili uliyoyataja pia kuna kundi "Monera, fungi na protoctista.'' Makundi hayo Matatu yanahusisha zaidi "vijidudu'' ndio maana kwa hali ya kawaida yanakua yanasahaulika kwenye stori za haraka haraka za viumbe hai.
Ninavyojua hayo makundi hua unayafuata ndani kadri unavyozidi kuzama kwenye kundi husika.

Hivyo mchwa ni mnyama, ila utaipata classification yake ukizidi kwenda ndani.
 
Kwahiyo kitimoto anamzidi akili nyau?

Halafu hao kunguru wanarushaje hayo mawe hadi wamdunde mlengwa?
 
QUOTE="srinavas, post: 27505983, member: 45365"]Mkuu asante kwa uzi mzuri. Ila majina ya Kiswahili sio ya mchezo , Bora ungeweka na kiingereza kwenye mabano kidogo maana huyo Fisi maji na huyo Pomboo kweli sijawahi kusikia hilo jina.[/QUOTE]
Pombo




Pomboo atakua ni dolphin.
 
Kunguru naye mnyama
Mchawa naye vp?

Kwahyo binadamu siyo mnyama?

Sikuamini tena.
 
Jelly fish yeye ndie kiumbe asie akili maana hana ubongo pia hana moyo wala macho hapa Duniani lakini ameweza kuishi Duniani kwa miaka zaidi ya milion 6000.

Hii itakuwa habari nzuri kwa wale vichwa maji wa humu JF. [emoji23] View attachment 804082View attachment 804083
Bila shaka huyu anakamilisha usemi wa jifanye fala siku ipite....naona ujinga wake ndio unamfanya asipotee duniani.
 
1.SOKWE

Great-Ape.jpg

Sokwe ni viumbe wa pili kwa kuwa na akili zaidi baada ya binadamu. Kwa mujibu wa uchunguzi wa kisayansi, binadamu alitoka katia familia ya sokwe ambao ni pamoja na nyani, kima, tumbili, na kadhalika.
Sokwe wana uwezo mkubwa wa kuwasiliana, kufahamu mazingira waliyomo, kujenga makazi yao na kutumia zana katika kutafuta chakula chao, wanaweza kujifunza maneno na lugha ya binadamu na hujilinda kwa kutumia zana mbalimbali.

2. POMBOO

dolphin-playing-ball_1600.jpg

Pomboo ndiyo wanafuatia. Ni wanyama ambao binadamu huwatumia kutatua matatizo mengi hususan ya baharini. Akili ya pomboo ni kubwa kama miili yao, huonyesha hisia mbalimbali, hujifunza vyema mazingira yao, nusu tu ya akili yake hulala, nusu nyingine ikiwa macho kukabiliana na tishio lolote

3. TEMBO

Elephant.jpg

Tembo wana akili kubwa kuliko mnyama yeyote wa ardhi kavu. Huonyesha akili nyingi kijamii na ni moja ya marafiki wakubwa wa binadamu. Hujifunza mazingira yao, hutambua milio mbalimbali, huonyesha furaha, hucheza na kusikitika. Huigiza pia sauti mbalimbali na hutafuta chakula kwa kutumia zana.

4. NYANGUMI

Whale.jpg

Wana uwezo mkubwa wa kutumia akili zao katika kuwasiliana na kuigiza sauti mbalimbali, mambo yanayowafanya kuwa wanyama wenye akili zaidi. Ni watulivu, wanapenda kusafiri na kuwinda.

5. MBWA

Dog.jpg

Ni marafiki wakubwa wa binadamu, ambapo mbwa wa kawaida ana akili kama mtoto wa binadamu mwenye umri wa miaka miwili. Wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu, kujilinda, na kujifunza kutoka kwa binadamu.

6. PWEZA

Octopus.jpg

Pweza ni viumbe wenye akili zaidi miongoni mwa wale wasio na auti wa mgongo. Wana uwezo mkubwa wa kujua maadui, mnyama pekee wa kundi hilo kutumia zana, hujibadili kukwepa maadui.
Mfano mzuri ni Pweza Paulo aliyetabiri Hispania kuchukua kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini.

7. NGURUWE

PIG.jpg

Mmoja wa wanyama wenye akili nyingi, hupenda kucheza na kushirikiana na viumbe wengine, wana uwezo mkubwa wa utambuzi kuliko mbwa, huenda kuishi pamoja, ana uwezo wa kurejea nyumbani hata akiwa mbali, hutambua sauti za viumbe wengine kiurahisi.

8. FISIMAJI

Fischotter_Lutra_Lutra.jpg

Ni wanyama wadogo zaidi wa majini wanaoishi majini na nchi kavu, hutumia mawe kutafutia chakula na kuondoa sehemu za samaki na kaa wakati wa kuwala, wana uwezo wa kutambua sauti za adui.

9. KUNGURU

Crow.jpg

Hawa wamezagaa duniani kote, hawawapendi binadamu na huwafanyia fujo wanapoweza, wana akili kubwa ya kutafutia chakula, miongoni mwa ndege wenye akili zaidi, wanatambua kirahisi mavi ya binadamu, wanaweza kuvunja nazi kwa kuiangusha kwenye mawe, hutumia mawe kushambulia maadui na kushambulia ndege wengine.

10. MCHWA

Ant.jpg

Hawa hawana akili kubwa, wamekuwepo tangu enzi za wanyama ‘dinosaur’ walipokuwa wanaishi, wana akili ndogo zaidi miongoni mwa viumbe mbalimbali. Walianzisha mfumo wa kilimo miaka milioni 50 kabla ya binadamu kwa kupandikiza na kukusanya chakula. Mchwa anaweza kubeba kitu kikubwa mara 50 zaidi ya mwili wake kutokana na misuli ya nguvu aliyo nayo.
Umesahau panya. Huwezi kuongelea wantama 10 wenye akili ukaacha panya. Hata 5 bora anaweza kuwepo.
 
kwahiyo nguruwa anamzidi paka akili? acha uzuzu!
 
Mkuu asante kwa uzi mzuri. Ila majina ya Kiswahili sio ya mchezo , Bora ungeweka na kiingereza kwenye mabano kidogo maana huyo Fisi maji na huyo Pomboo kweli sijawahi kusikia hilo jina.
fisimaji otter pomboo dolphin
 
Mnyama = Animal.
Animal is any member of kingdom Animalia.

Mchwa anapatikana Kingdom Animalia, phylum arthropododa, class insecta.

Kwa maelezo hayo mafupi, ya juujuu na ya jumla jumla, ninayo furaha kubwa kukujibu mbele ya hadhara hii, kwamba hakika Mchwa ni mnyama.
jamaa mgumu kuelewa huyo, ni wazee wa viswahili na history
 
Back
Top Bottom