Hatimaye Rais Samia atimiza ndoto za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,230
9,667
Ndugu zangu zilikuwa ni ndoto za baba wa Taifa kuijenga Tanzania yenye usawa na haki kwa watu wote, Tanzania ambayo kila mtu alikuwa ana nafas sawa katika kuijenga na kunufaika na matunda yake, Tanzania iliyokuwa inaheshimika na mataifa yote bila kujali uchumi wetu.

Katika kuifikia azima hiyo baba wa Taifa alihakikisha anaijenga misingi imara ya kutuungaanisha, alijuwa nyumba Bora inatokana na msingi ulio imara, hivyo alijenga msingi imara wa umoja, mshikamano na upendo, kwa kuvunjilia mbali ukabila, udini na hata ukanda.

Alipinga kila aina ya ubaguzi kila alipopita Hadi mbegu hiyo ya kuepuka ubaguzi ikamea na kukomaa katika akili zetu, vizazi na vizazi tukalijuwa Hilo kuwa sisi sote ni watanzania, tukawa hatuulizani habari za makabila au dini hata wakati wa kuoa au kuolewa

Tulikuwa wamoja kwelikweli, ungeweza kwenda ugenini ukapewa mahali pa kulala na kula chakula na siku ya kuondoka Kuendelea na safari yako ukashikiwa kuku wa kwenda Naye uendako, mtu ungeweza kuwa kiongozi hata eneo ambalo hujazaliwa maana hatukuangalia kabila Wala dini Wala ukoo wakati wa kumpa mtu uongozi ikiwa anavigezo na sifa.

Hata mfumo wa mwanafunzi kutoka mkoa mmoja kwenda kujiunga kidato Cha kwanza au tano mkoa mwingine kiliendeleza dhana hiyo ya kuujenga umoja wetu, kiukweli ilikuwa ni ngumu Sana kwa adui kupenya katikati yetu au kutugawa, Na ilikuwa Rahisi Sana kwetu kumkabili adui na kumshinda kwa namna tulivyo kuwa wamoja Kama Tulivyo mkabili na kumshinda nduli idd amini Dada mwaka 1978-1979.

Ndugu zangu mpaka kifo chake Baba Wa Taifa aliendelea kuhubiri dhana hiyo katika kulijenga Taifa letu kuwa moja, Alipeleka maendeleo kila eneo la nchi hii bila ubaguzi, alisomesha watanzania wote wenye sifa ndani na nje ya nchi bila ubaguzi ili wakirudi waje waitumikie Tanzania.

Alipambana kuhakikisha kuwa maendeleo yanayopatikana yanamgusa mwananchi mnyonge, alisisistiza kuwa maendeleo yanapaswa kuwa ya watu na siyo vitu tu pekee, alihakikisha uchumi unakuwa shirikishi wa kumgusa Mtanzania.

Hii ndio sababu Mwalimu nyerere anakumbukwa na kuliliwa mpaka kesho siyo tu na watanzania Bali bara Zima la Afrika na dunia yote kwa ujumla wake, kwa namna alivyookuwa akiwajali watu.

Asante mungu wakati watanzania wakiwa na mawazo hayo ya unyerere akilini mwao anaibuka Rais ambaye Ni Kama Nyerere amezaliwa ndani yake kwa kurudi katika ndoto na fikra za mwalimu Nyerere, kwa kuunganisha Tanzania kuwa Taifa moja, lenye umoja mshikamano na upendo.

Huyu sio mwingine Bali Ni mh Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Alie amua kuijenga Tanzania iliyo moja, Tanzania yenye umoja mshikamano na upendo, anaijenga Tanzania ambayo adui akijitokeza tutamkabili kwa pamoja bila kujari itikadi za vyama vyetu, Tanzania ambayo kila mtu Yupo huru kutoa mawazo na akasikilizwa

Kazi hii aliianza Mara tu alipoapishwa na kuwa Rais hasa pale aliposeama siyo wakati wa kuangalia mbele kwa mashaka Bali kuangalia mbele kwa matumaini na kukuamini, siyo wakati wa kuangalia yaliyo pita Bali Ni wakati wa kuangalia yajayo, siyo wakati wa kunyoosheana vidole Bali Ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbelee.

Aliendelea kusema kuwa huu ni wakati wa kufarijiana na kufutana machozi, kiukweli yote aliyo yasema mh Rais hakika yalitoka ndani ya moyo wake, maana kwa Sasa unaona namna nchi inavyi jengwa kila Kona ya nchi unakuta miradi ya maendeleo ikiendelea.

Ile dhana ya baba wa Taifa kuwa maendeleo ni lazima yawe ya watu kwa Sasa mh Rais anaitekeleza vyema Sana, ndio maana unaona namna anavyofanya vitu vinavyo mgusa mwananchi moja kwa moja,

Anajenga uchumi shirikishi na unaomgusa mwananchi, ametambua kuwa karibu 80% ya watanzania Ni wakulima, hivyo Ni lazima juhudi zote za kuujenga uchumi uhakikishe kuwa unatoa kipaombele katika kilimo, ndio maana unaona hata kauli mbiu ya mwaka huu kuwa kilimo Ni biashara.

Anatimiza Hilo kwa serikali yake kutoa Ruzuku ya billioni Mia moja hamsini ili kupunguza Bei ya mbolea itakayosaidia wananchi wengi kumudu bei, soko la uhakika kwa Sasa lipo maana ameimarisha vizuri mahusiano yetu na majirani na hivyo kurahisishia biashara na majirani zetu,

Kwa Sasa pia huduma za kijamii zinaendelea kuboreshwa kila mkoa ambako utaona vituo vya Afya, shule, umeme, maji Miundombinu ikijengwa kila eneo,

Kwa Sasa utaona pia namna Mh Rais anavyopambana na suala la mfumuko wa Bei unaoitesa Dunia kwa kutoa Ruzuku ya karibu billion Mia moja kila mwezi katika mafuta ambayo ni injini katika uendeshaji wa uchumi, maana mafuta yakipanda kila kitu lazima lipande.

Kwa Sasa keki ya Taifa inagawiwa kwa usawa na haki, hakuna anayeachwa nyuma kwa Sasa, hakuna anayesahaulika kwa Sasa, wote tunanufaika na kile kipatikanancho.

Ndio maana unaona hata wakina Mh Mbowe wakisimama mahali wanahuburi Aman umoja mshikamano na upendo maana mama anaeleweka dira yake kwa Sasa.

Tuendelee kumuunga mkono Mh Rais wetu katika juhudi zake za kuijenga Tanzania mpya kwa kizazi hiki na kile kijacho, Tanzania ya kesho iliyo Bora inategemea na ubora wa mawazo na maamuzi yetu ya leo, Tuamue sote kwa pamoja kuijenga Tanzania ya kesho iliyo Bora kwa kuiandaa vyema leo.
 
Duh mambo yakuandika hapa nimengi muda hautoshi,tozo zimetukakamaza viungo hata kuandika inakua tabu.

Siwezi sema umelamba asali lakini najiuliza kwani hujaona changamoto zetu nazo ukaziweka hapa?

Hiyo elimu bila walim wakutosha unamaanisha nini? Walimu wapo mtaani na wanafunzi wapo shuleni serikali nayo ipo ofisini.

Nasema hivi hili nalo mkaliangalie
 
Hapa ulikuwa hujaanza upuuzi wa kuweka namba za simu.
JamiiForums3817054.jpg
 
Back
Top Bottom