Rais Samia kuongoza uzinduzi wa Sanamu ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Addis Ababa Ethiopia

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,274
9,717
Ndugu zangu Watanzania,

Baada ya hapo jana Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hasssan kipenzi cha watanzania mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge kuongoza watanzania katika mazishi ya waziri Mkuu mstaafu hayati Edward lowassa,hii leo anafanya kazi nyingine tena ya kimataifa kuwaongoza makumi ya viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika katika uzinduzi wa Sanamu ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage Nyerere Addis Ababa Ethiopia.

Sanamu hiyo inakuja kama sehemu ya kutambua mchango mkubwa sana wa Mwalimu Nyerere na Tanzania katika ukombozi wa bara la Afrika.huwezi ukaiandika vyema historia ya bara la Afrika pasipo kuitaja kwa uzito na kuizungumzia kwa heshima kubwa nchi ya Tanzania. Ni Tanzania ndio iliyoongoza ukombozi wa nchi nyingi sana barani Afrika kutoka katika makucha ya wakoloni hususani nchi za kusini mwa Afrika. lakini pia Tanzania imewahi kutoa katibu mkuu wa OAU iliyokuwepo awali kabla ya hii ya sasa.

huyu si mwingine bali ni Salimu Ahmed Salim kuanzia mwaka 1989-2001,ambaye kama siyo kura ya VETO ya marekani alikuwa anakwenda kuwa mtanzania wa kwanza kuwa katibu mkuu wa umoja wa Mataifa yaani UN.kwa kuwa alikuwa amekidhi kila kitu na kila sifa na uwezo wa kutosha, lakini kutokana na itikadi na siasa za ujamaa na ubepari ambazo zilikuwa zimeota mizizi na kutawala kwa wakati huo ikawapa hofu Marekani walioamua kumpiga vita asitwae kiti hicho.

Kwa hiyo leo Rais wetu mchapa kazi ametua huko kwa kishindo na kwa kujivunia historia ya kutukuka na mchango wa kipekee wa baba yetu wa Taifa na Taifa letu kwa ujumla .lakini pia ikumbukwe ya kuwa hata lugha yetu ya Taifa yaani kiswahili ni miongoni mwa lugha zinazotambulika katika umoja huo, lugha ambayo baba wa Taifa aliitumia kwa nguvu zake zote kuliunganisha Pamoja Taifa letu na kujenga umoja wa kitaifa.

Rai yangu ni kuwa tumuenzi baba wa Taifa kwa kufanya yale mazuri yote aliyokuwa anayahubiri,tupinge vita rushwa,wizi,ufisadi,ubaguzi na unyonyaji wa aina yoyote ile. Ni lazima viongozi wetu wamuenzi kwa kudumisha uadilifu na uzalendo na siyo kuogopa kimvuli chake na sauti yake kwa yale aliyokuwa akiyakemea. Ni lazima viongozi wetu wawajali ,kuwapigania ,kuwatetea na kuwasemea watanzania wanyonge wasio na Sauti.ni lazima kila mmoja ajiulize ataifanyia nini Tanzania na siyo Tanzania itamfanyia nini yeye binafsi.

Ni lazima kila kiongozi ajuwe cheo ni dhamana.na kwamba mali ,pesa na vyeo vyote ni vya kupita tu. Ni lazima viongozi wetu wajuwe ni bora jina zuri kuliko mali na utajiri wote wa Dunia.na kwamba kitakachokumbukwa kutoka kwao na kukufanya uendelee kuishi hapa Duniani hata kama umetangulia mbele za haki ni matendo yako mema kwa watu,utu wako,kugusa kwako maisha ya watu,kutenda kwako haki kwa watu wote pamoja na mengine mengi kama haya.ukitenda mabaya ukiwa madarakani basi tambua yakuwa utakufa siku hiyo hiyo utakayotoka madarakani hata kama utakuwa bado upo hai maana watu watakusahau kabisa katika mawazo na akili zao kama umewahi kuwa kiongozi wao, kwa kuwa hukugusa maisha yao kwa namna yoyote ile ukiwa kiongozi.
 
Ni nini faida ya hiyo sanamu Kwa watanzania kiuchumi?

Hiyo sanamu ni Tsh ngapi?

Gharama za kwenda na kurudi msafara mzima ni Tsh ngapi?

Huyu mama anajua tuko gizani hakuna umeme?

Sijawahi kuona bibi mtembezi kama huyu
Uwe na heshima kwa Mheshimiwa Rais wetu unapomzungumzia. Rais wa nchi siyo sawa na Rais wa bao au kikundi cha bendi.
 
Huyu apewe tu Wizara ya mambo ya nje....; sisemi kwamba hii asingekwenda bali huenda kule Norway na USA alikokaa wiki na zaidi angeweza kuwakilishwa.... (ifike wakati achague sio kila sehemu lazima afike)
 
Kwa elimu ipi?
Politics za Dunia ya sasa huitaji Elimu ya Darasani ni talalila nyingi na peoples skills... Tena ukipeleka elimu zako kwenye politics utakuwa frustrated.... (Hii Tasnia ishakuwa ya Kisanii na Ulafi)
 
Heshima kubwa kwa muasisi wa Taifa letu Hayati JK Nyerere.

Kiongozi wetu Rais wetu hana budi kuipokea/kushiriki katika tukio hilo muhimu kwa Muasisi wa Taifa letu.
Heko kwa Rais wetu kwa kushiriki.
Hakika katika awamu hii ya 6 Taifa letu lipo active.
Mama yupo kazini.
 
Huyu apewe tu Wizara ya mambo ya nje....; sisemi kwamba hii asingekwenda bali huenda kule Norway na USA alikokaa wiki na zaidi angeweza kuwakilishwa.... (ifike wakati achague sio kila sehemu lazima afike)
Ziara za Mheshimiwa Rais nje ya nchi zimekuwa na faida kubwa sana kwa Taifa letu,kwa kuwa zimeleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kibiashara .ndio maana ndani ya muda mfupi tumeona ongezeko kubwa la watalii kufika million 1.8 kwa mwaka. Tumeona wawekezaji na uwekezaji ukiongezeka hapa nchi hali iliyopelekea hata mapato yetu kwa mwezi kuongezeka sana.
 
Ziara za Mheshimiwa Rais nje ya nchi zimekuwa na faida kubwa sana kwa Taifa letu,kwa kuwa zimeleta fursa mbalimbali za kiuchumi na kibiashara .ndio maana ndani ya muda mfupi tumeona ongezeko kubwa la watalii kufika million 1.8 kwa mwaka. Tumeona wawekezaji na uwekezaji ukiongezeka hapa nchi hali iliyopelekea hata mapato yetu kwa mwezi kuongezeka sana.
Sera ni kitu muhimu sana...; Tulivyopata uhuru tulikuwa na Sera za Self Reliance (kujitegemea) unajua hakuna kitu cha muhimu sana kama mentality - sasa wewe kama mentality yako ni kuzunguka huku na huku ili watu waje wafanye na kukufanyia badala ya wewe kwenda kufanya huko ni kama kuwa na ulemavu...

Unaongelea Utalii kuongezeka sasa kama umeongezeka na mapato kuongezeka hizo dollar kupungua kunatokea wapi ? Ni nini faida kwa mwananchi kwa vitu hivyo kuongezeka wakati yeye hana faida ? Si bora azunguke ndani na kuhakikisha huyu mwananchi hata anapata umeme wa uhakika ili juice anazotengeneza sisichache kwa kukosa umeme ? Hizo gharama za safari zisizoisha nina uhakika ni pengi zinaweza kutumika...
 
Back
Top Bottom