Rais Samia ashiriki Misa Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Oktoba 14, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki Misa Maalum ya Kumuombea Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere leo tarehe 14 Oktoba, 2023 Babati, Mkoani Manyara.


View: https://www.youtube.com/live/KmuRAUC9pSQ?si=GqCzOhpasVu7Yf4w

HOMILIA YA ANTHONY LAGWEN, ASKOFU JIMBO KATOLIKI MBULU

Hayati Baba wa Taifa alivipiga vita vizuri hadi mwendo alipoumaliza, vita vizuri dhidi ya ujinga, maradhi, umasikinj, rushwa na ufisadi. Alikuwa kiongozi mpatanishi ndani na nje ya mipaka yetu.
Alikuwa kiongozi mzalendo kwelikweli. Tulipata bahati ya kuongozwa na mtu aliyemcha mwenyezi Mungu. Alikuwa kiongozi mwenye upendo na mwema.

Bado ni hazina kwa wanasiasa na wananchi. Alipenda kumsikiliza mwenyezi Mungu hivyo alijariwa hekima na busara. Aling’aa, alijaliwa maono ambayo sisi tunachukulia kama utabiri.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha yake, kwa kuonesha mengi ya kufaa tena yenye mkono wa mwenyezi Mungu.

Ili tumuenzi vizuri inafaa tutambue kuwa amani, umoja na mshikamano ni msingi wa maendeleo ya kweli. Tutambue kwamba tuna jukumu la kulinda amani, tuna wajibu wa kuleta maisha ya fadhira na dhamiri njema, tukwepe kupuuza au kushabikia uovu au jambo lolote tunaloona ni aibu kwa mtu au fedheha kwa taifa letu, mambo kama ushoga, usagaji na biashara ya binadamu yanapaswa kupigwa vita.

DKT. PHILIP MPANGO, MAKAMU WA RAIS
Baba wa Taifa aliamini katika Usawa. Aliwaona binadamu wote kuwa ni ndugu zake. Kwahiyo nasi tuna wajibu wa kuyaishi haya…

Alichukia sana rushwa. Hakuvumilia vitendo vyovyote vyenye harufu ya rushwa wala ufisadi. Kwahiyo ni wajibu wetu Watanzania kuyaishi haya.

Alithanmini sana dhamana aliyopewa. Hakutumia cheo chake kwa faida yake. Makongoro yupo hapa. Hata kale kanyumba kazuri kaliyopo Butiama alikuja kujengewa na Serikali. Sasa viongozi tujitafakari. Wale wanaojilimbikizia mali kwa kutumia vibaya nafasi zao, siy njia njema ya kumuenzi Baba wa Taifa letu.

Alitumia elimu yake na vipaji alivyopewa kwa faida ya wote. Kupiga vita umasikini, wote tunafahamu. Nikweli alikuwa ni mwalimu; alikuwa ni mwalimu Hodari wa kufundisha.

Alikuwa mkweli. Hakutaka fitina Mwalimu. Kwahiyo nasi tujitahidi sana kukwepa kuwa wafitini.

Alikuwa ni mnyenyekevu. Hakusita kujisahihisha pale ambapo alidhihirika kabisa na yeye akatambua amekosea. Na sisi, viongizi kwa wananchi, pale ambapo tunakosea tukiri kabisa tumekosea na tujisahihishe.

Mzee mmoja aliyefanya kazi karibu na Baba wa Taifa, wiki hii ameandika aliunde wilaya mpya ya Serengeti na tukio lile likafanyika Bunda, lakini makao makuu akayatangaza yaende ----, watu wakaondoka hata kwenye mkutano. Lakini Mwalimu alijisahihisha akaunda wilaya mpya, akapeleka makao makuu ya wilaya pale Bunda. Kwahiyo na sisis tukikosea tusisite kujisahihisha.

Alikuwa muadilifu sana. Hakupenda kutumia mali ya umma kujinufaisha. Alikuwa mlinzi wa rasilimali za umma. Alijenga na kuimarisha maadili kwenye jamii yet una wala hakusita kukemea matendo mabaya ambayo yalichochea mmomonyoko wa maadili.

Alikuwa ni mwanamazingira hodari sana. Wale ambao wamepita Butiama, alikuwa fundi wa kulinda ule msitu wake pale. Baba wa Taifa alikuwa mkulima Hodari. Alipenda sana kazi ya kulima yeye mwenyewe. Maana yake ni kwamba nasi Watanzania tumuenzi kwa kuendelea kuchapa kazi, tena kwa bidi kabisa kuboresha Maisha yetu na kuinua vipato vyetu na kipato cha taifa letu.

KWA NIABA YA RAIS SAMIA
Na kwa sababu ya muda kama ilivyoelezwa, napenda, kwa niaba ya Mh. Rais, ambaye amenipa heshima ya kusimama mbele yake na mbele ya umma huu wa Watanzania wanaofuatilia shughuli hii, kumuwakilisha kusema salamu fupi.

Mhashamu Baba Askofu ninakushukuru sana, sana kwa ibada hii nzuri na mahubiri yako mazuri. Na kwa wananchi na waumini wote mlioko hapa, ahsanteni sana kwa kujumuika nasi katika ibada hii nzuri kumuobea kiongozi wet una tutumie nafasi hii pia kuendelea kuwaombea viongozi wa taifa hili, na hasa kiongozi wetu mkuu ambaye ameungana nasi katika ibada hii.

- Msichoke kuendelea kuliombea taifa letu
Mhashamu Baba Askofu, kwa jukwaa hili pia naomba msichoke kuendelea kuliombea taifa letu amani na utulivu. Hili ni jambo kubwa sana, na umeeleza vizuri, “bila amani na utulivu hakuna amani katika taifa lolote”. Na mnaona yanayoendelea huko kwingine. Kwahiyo tuendelee kumsihi Mungu taifa letu kweli liendelee kukaa kwa amani na mtumishi wake Mwl. JK Nyerere aendelee kuliombea taifa letu amani huko alipo.

- Ahadi ya Tsh. Milioni 100 kwa Kanisa Katoliki
Mheshimiwa Rais amenituma mambo mawili. Mhashamu Baba Askofu, kwa ajili ya lile zoezi la kutabaruku kanisa mwakani, Mh. Rais kwa ukarimu wake kwa raia wake na kwa kanisa Katoliki, ameniagiza nitangaze kwamba ataleta shilingi milioni 100. Kama hiyo haitoshi, Mh. Rais amekuja na zawadi na ataikabidhi baadaye kidogo baada ya ibada hii. Sasa hiyo naomba nisiiseme, itatolewa kwa wahusika mara moja.

Na kwa jambo hilo kubwa na mimi naomba nimuige bosi wangu, lakini mimi sitafika huko. Naomba nimuige kidogo nimuunge mkono…

(Ghafla Rais anasimama akiwa miongoni mwa waumini. Anasema jambo ambalo Dkt. Mpango anashindwa kulisikia vizuri akiwa kwenye madhabahu. Sekunde kadhaa baadaye anakuwa ameupata ujumbe wa Rais, kisha anaendelea kuzungumza)

Bosi wangu ananipenda eeh? Kumbe katika ile 100, nusu ananitolea mimi msaidizi wake. Tumsifu Yesu Kristo!...
 
Happy Nyerere Day!
October 14, 2023
1697217842669.jpg
 
Back
Top Bottom