Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
Unapokuja mkutano Mkuu wa CCM siku chache zijazo bila ya shaka kati ya mambo ambayo CCM inaweza kufanya ni kuangalia kama Katibu Mkuu wao Lt Mstf Yusuph Makamba amewafaa sana au la. Je utendaji wake ukilinganisha ule wa waliomtangulia kina Kawawa, Kolimba, Mangula n.k umeifaa CCM hasa katika mazingira ya kisiasa ya wakati huu? Je, ataendelea kuwafaa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa 2010? Je unaridhishwa na jinsi ambavyo ameiongoza CCM katika kujibu hoja na tuhuma mbalimbali ndani ya CCM na ndani ya serikali ya chama chake?
Inawezekana kuwa mzee Makamba kazi hii ya Ukatibu Mkuu imeanza kuwa ngumu na anashindwa kutafutia majibu ya kuelewa hasa kutokana na kauli zake ambazo huko nyuma zimewahi kutishia mufaka wao na CUF na hasa kauli za kutoyapa uzito unaostahili maswala ya kitaifa na hoja zinazohusu Taifa?
Je, wakati umefika CCM ijitafutie KM mpya ili iandane na wakati na kujiandaa kujibu mapigo. Je, Mangula arudishwe? Itakuwaje kama Mwanri atapandishwa cheo na kuwa Katibu Mkuu? Mnaonaje kama Kinana akarudishwa na kupewa Ukatibu Mkuu?
aende asiende, na kwanini?