Hatimaye Jerry Muro ashinda kesi yake

Hatimaye Jerry Muro ashinda kesi yake

Aliyekuwa Mtangazaji wa TBC1, Jerry Muro na wenzake 2, wameachiwa huru leo na hakimu Frank Mosha wa mahakama ya kisutu baada ya kuwaona hawana hatia na makosa waliyoshitakiwa nayo. Jerry na wenzake walikuwa wakikabiliwa na mashitaka matatu ya Kula njama ya kutenda kosa, kuomba rushwa na kujifanya maafisa wa Takukuru, madai ambayo yametupiliwa mbali kwa kukosa ushahidi.
 
hongera Muro. unaonesha kuwa ulikuwa kweli unafanya kazi yako kiusahihi
 
hatimaye Mwandish wa habari Jeri Muro ameachiwa huru.mwandishi huyo aliyekuwa anafanya kazi TBC alikuwa anakabiliwa na kesi ya kudai rushwa...
pole sana jerry tht is bongo polce for you
 
Dah! Pole sana Jerry..Karibu tena uraiani. Lakini naamini utakuwa umeshapata fundisho. Siyo kila mtu ni wa kuchezea ndani ya TZ hii
Acha urongo..kwani alikosa mudhamini??
 
unamaanisha nn mkuu au ndo masa.. at work?

Kwani hujui kuwa Jerry Muro alikuwa anawafanyia kazi CIA? Hukumbuki kipindi cha ziara ya Bush alivyokuwa busy kuzunguka na camera nchi nzima? Wakulu walipoanza kuona mambo yanageuka wakamzushia zengwe ili wampunguze kasi.
 
hana tena mvuto..baada ya kufukuzwa TBC alijiunga na Tumaini university..kuna mwalimu alimfukuza kama paka! Kila mtu tumaini alikuwa anamuona kichefuchefu.
Juzi juz hapa nimekutana naye maeneo ya Calabash na GX 100 yake, maskini kachooka. Nikamblock kwanza! Nilikuwa nasubiri alianzishe bahati nzur akawa mpoleee

hovyooooo........huna lolote wewe hapo ulipo...naona ulitamani sana afungwe ..hiloooooo..
 
Sheria za nchi zinasema ukishashtakiwa mahakamani hutakiwi kuajiriwa tena na kampuni yoyote ile. Huyu Jerry Murro imekula kwake moja kwa moja.

Mwita stop lying Great Thinkers! iF One Door is Closed Anorther one is open!
 
hovyooooo........huna lolote wewe hapo ulipo...naona ulitamani sana afungwe ..hiloooooo..
Acha mipasho sasa. Mimi siyo hakimu. Best judgement has been reached. Tumuache naye sasa awe huru. Mimi nimempa onyo tu! Aangalie pa kugusa, siyo kila mahali panafaa kugusa. Wanaoona wananyamaza siyo wajinga.
 
Mwita stop lying Great Thinkers! iF One Door is Closed Anorther one is open!

Mkuu haina haja ya kubishana na Mwita
Naona anafurahisha tuu hapa na kuweka post ambazo hana uhakika nazo
 
Thr is another THREAD regarding this TOPIC, Look For It
 
Rejao bado hujakua kweli,
siku yakikukuta ya jeri muro wewe tuseme unayosema utajisikiaje,
geuza shilingi.
 
Mwita stop lying Great Thinkers! iF One Door is Closed Anorther one is open!

Labda uitaje hiyo sheria. Maana haki ya Kikatiba ya mtu kupata ujira wa haki itakuwa imevunjwa. Kwani kushtakiwa ndio kunaondoa haki ya mtu kufanya kazi halali? Tuambie ni sheria ipi inasema hivyo isije kuwa ni yale yale ya JK kudai kuwa "anafuata Katiba" bila kusema ni kifungu gani cha Katiba anachokifuata kwenye mchakato wa Katiba mpya. (From MwanaKijiji ) na mimi pia nomba kujua hii sheria ni ya wapi!
 
hana tena mvuto..baada ya kufukuzwa TBC alijiunga na Tumaini university..kuna mwalimu alimfukuza kama paka! Kila mtu tumaini alikuwa anamuona kichefuchefu.
Juzi juz hapa nimekutana naye maeneo ya Calabash na GX 100 yake, maskini kachooka. Nikamblock kwanza! Nilikuwa nasubiri alianzishe bahati nzur akawa mpoleee

Aibu imekupata...lol wivu kama .......imekula kwako
 
Rejao bado hujakua kweli,
siku yakikukuta ya jeri muro wewe tuseme unayosema utajisikiaje,
geuza shilingi.
Hujanielewa mamndenyi. Mimi huwa najitahidi kuwa makini sana. Siyo kila mahali napagusa. Nikiona maji marefu na siyawezi napotelea mbali. Ndio maana mimi nimempa ushauri kuwa na yeye asiwe anagusa pasipogusika!
 
Back
Top Bottom