Hatimaye EU wakubali kutoa Sh. 860 billioni za maendeleo

Mimi nawashuru sana wafadhiri make unaona vitu vidogo tu ambavyo serikali ingefanyia kazi (ubadhirifu ktk serikali namashirika ya uma) wanapata kigugumizi bado wafadhiri wanapata mwoyo wa kusaidia tu jiweke saaafi kwanza ndio muombe misaada. Inamaana serikali inafiki wafadhiri ni vipofu au hawaoni mtazamo wa watanzania walio wengi? Jisafisheni, jiwekeni katika kuondokana na viulizo vingi mtapata misaada. halafu mimi nashindwa kuelewa kodi lukuki bado misaada? Serikali inabidi ipate somo kutoka kenya kupunguza utegemezi katika bajeti zetu.
 
Kalamu,
1. Elimu 2. Elimu 3. Elimu
Naafikiana nawe kiasi fulani tu!
Mimi ningesema Elimu na infrustructure. Utajengaje shule wakati huna barabari kupishia building materieals? Hivyo Vyuo/shule zitajengwaje bila miundo mbinu?
Or kalamu do you mean Elimu na Associated Infustructure to support Development in Elimu?
 
Kalamu,
1. Elimu 2. Elimu 3. Elimu
Naafikiana nawe kiasi fulani tu!
Mimi ningesema Elimu na infrustructure. Utajengaje shule wakati huna barabari kupishia building materieals? Hivyo Vyuo/shule zitajengwaje bila miundo mbinu?
Or kalamu do you mean Elimu na Associated Infustructure to support Development in Elimu?

Ninamaana, misaada inayotolewa na wafadhiri - priority ni Elimu.
Miundombinu ni mhimu, fanya juu chini kuishughulikia hata kwa pato la ndani na harambee ya wananchi. Barabara za tope nyingi vijijini kote zimechimbwa na nguvu za wananchi. Endelea kuziimarisha kadri ya mafanikio ya "Elimu" yatakavyoendelea kuimarika.
 
lakini jua kwamba viongozi wetu ni ving'ang'anizi kweli, kama kuna siku nilisoma gazeti eti kiongozi fulani "huyu anatajwa kila leo" ni EL alikuwa akiwaelekeza watu wenye fani yao jinsi ya kufanya kazi, na wao wakaamua kufanya walivyoelezwa na bosi wao mwishowe wakavurunda.
viongozi wetu lazima wabadirike ili kupata maendeleo.
 
Kalamu,
Shukran kwa kunipa swali hili gumu ambalo nina hakika kabisa kuwa ndio linajibu hoja nzima ya swala hili ktk mitazamo tofauti. Na kusema kweli mimi ninakuwa na mtazamo tofauti.
Kwanza, nitalitaza gonjwa letu kwa diagnostic medical sonography (utrasound) kisha baada ya hapo nitatumia msaada huo kwa dharura ya KUPONYA kwanza gonjwa lenyewe kisha ndipo nitajenga mikakati ya kinga kuhakikisha Ugonjwa huo hausambai na rahisi kuponyeka na hata kuwa historia ktk jamii yetu.
kwa hiyo ikiwa Umaskini wetu ni Epidemic nadhani my first priority would be - Kutafuta virus vya huo Umaskini badala ya kutegemea sana waganga toka nje. Wagonjwa wa Umaskini ni sisi na wao huko nje wana magonjwa yao ambayo kila kukicha wao pia hutafuta dawa za dharura kulingana na magonjwa yao. Kama alivyoelezea ndugu yetu hapo nyuma kuhusu nchi za magharibi, Asia na kadhalika.
Umaskini wetu ni sawa kabisa na ugonjwa wa TB ambao umewapa mshtuko mkubwa sana Marekani hivi majuzi. Wakakusanyika madaktari wengi sana wenye kila ujuzi wa magonjwa na kusema kwa pamoja kuwa TB alopata raia wao mmoja ilikuwa TB ambayo haina dawa!...mshtuko mkubwa kwao lakini sio kwa Mbongo!
Kuna daktari mmoja Mbongo mwenzetu ambaye anaishi hapa alinambia kuwa hawa jamaa kweli hawafahamu TB zaidi ya elimu ya kitabuni. Nikamuuliza kwa nini?..
Akasema:- ' hawa jamaa kweli wanayo elimu kubwa ya Udaktari wa magonjwa kunizidi lakini nina mashaka kama wamewahi ku-expertize ktk gonjwa hili yaani TB!...haiwezi hata kidogo TB kuponyeka kwa siku 10 tu ama kuona dalili ya kuponya baada ya siku 10, sasa wanataka kumkata huyu jamaa mapafu yake bure maskini wa watu.'
Kwa hiyo nikamuuuliza kama diagnosis waliyoitoa sii ya kweli!... akasema ni ya kweli lakini wanachokosea ni kutegemea muda wa tiba kuwa chini na pengine dawa wanayotumia sii nzuri... wee subiri utasikia baada ya mwezi kuwa huyo jamaa hali yake inaendelea vizuri!.... na kweli jamaa sasa hivi hali yake shwariii!
Sasa nirudi ktk mada yetu, mimi naamini kabisa kuwa tunaanza kujengewa imani ya kwamba Umaskini is an Incurable Epidemic, na ndio maana focus ya dharura inaondoka na epidemic hii kuwa ni part of our life - being Africans. Hii ni imani inayoendelea kujengwa na wafadhili wetu ambao hofu yao kubwa sio maisha yetu ila maradhi haya kusambaa na hata kufika kwao kwa njia za wahamiaji. Biashara na meningeyo mengi tu yanaweza kuwa sababu kubwa ya sisi kupewa darasa la Umaskini kama ni Ugonjwa wa kudumu ktk nchi za sub-sahara kwa hiyo malengo ni ya muda mrefu na sio dharura!

Kwa hiyo, umeuliza ni vitu gani nitatanguliza mbele kama vipaumbele vya fedha za misaada!
Nadhani kwanza ni kuhakikisha kuwa asilimia 80 ya wananchi wetu ambao ni wakulima wadogo wadogo wanaojenga hesabu kubwa ya UMASKINI wanapata nafasi kubwa ktk Ulimwengu wa Utandawazi. Tatizo ambalo nimeliona Bongo ni kwamba leo hii hesabu hiyo imekwisha ondoka. Wakulima wamebaki wachache sana, kila mtu ni mjasiriamali wa Ulanguzi, kuagiza mali za nje na wizi mdogo mdogo wa kiujanja. Hesabu kubwa ya wananchi vijijini wamesha uza mashamba yao kwa ujenzi wa majumba ya fahari. Tunaanza kupoteza mashamba madogo madogo na raia wengi kujikita ktk biashara zinazohusu mali toka nje. Tumeshindwa kufidia kilimo kwa ajira za huduma (services) kwa sababu elimu na exposure sio mpango wa short term wala dharura.
Kumbuka tu kwamba tumetoka ktk Ujamaa na kuingia dunia hii mpya ya Utandawazi na soko huria bila kujiandaa vya kutosha na pia tukiwa bado wagonjwa yaani - Maskini. Tulikosa kutazama virus vya ugonjwa huu mwilini mwetu tukafikiria kwamba tukibadilisha mazingira yetu labda matatizo yetu yataweza ondoka kwa msimu wa nyakati.

Tulipokea misaada wakati wa Ujamaa na leo bado tunapokea misaada kwa sababu hiyo hiyo... gonjwa ndio kwanza lazidi kusambaa kwa sababu virusi bado vipo!
Kwa hiyo mimi kitu kitakacho tangulia yote haya ni kuwawezesha aslimia 80 ya wananchi wetu ambao ni Maskini.
Hi ndio dose ya haraka na dharura kwa wananchi!.... Ujenzi wa miundombinu utakuwa umelenga wizara zinazohusiana zaidi na Kilimo chetu ikiwa ni pamoja na Ukulima, Uvuvi na Ufugaji ili kuwawezesha hawa asilimia 80. Na kikubwa zaidi ni ile itikadi ya kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi wao.
Ni aibu kubwa sana unapotembelea supermarket zetu na maduka yote ya retail yamejaa mali za nje! vitu ambavyo vinaweza kabisa zalishwa humu nchini na pia kusafirishwa nje ktk standard ya hali ya juu kabisa...Hizi zote ni ajira tunazipoteza bure bila kuboresha maisha ya walalahoi wengi.
ELIMU ni ktk long term plan, mimi siwezi kuiweka elimu kama ni dharura kwani hata tukikumbwa na Kipindupindu, kitu cha kwanza ni kuhakikisha unazo dawa za kuwatibu wagonjwa!...elimu inafuata ama kuambatana na tiba. Elimu itatangulia kila siku ya maisha yetu hata kama kun dharura ama hakuna! Na elimu ndio kinga pekeee yenye umuhimu zaidi ktk madhara yote.
Tanzania tumisha kumbwa na hili gonjwa la Umaskini na yaonyesha wazi linahitaji dawa, tatizo kubwa linalotupata ni kwamba elimu inatumika wakati sisi ni ni wagonjwa!..huwezi kumwambia mgonjwa wa HIV atumie condom kila anapojisikia na ukasahau kumpa dawa za kinga...kibaya zaidi ni kwamba hata tunapopewa hizo sindano, kutokana na matatizo yetu mengi sisi tunazitumia ktk kujidunga na unga wa kilevi - cocaine! hizo biashara za mali toka nje ati ujasiriamali!
Waleta unga akina nani?... viongozi wetu sasa nambie hapo elimu kweli itafanya kazi kwa zungu la unga! pamoja na kwamba siamini kabisa kuwa Umaskini wetu ni sawa na HIV. Ni maradhi ya kujitakia sio kabisa incurable epidemic!
Umaskini wetu unaponyeka na tunaweza kabisa kuufuta ktk muda wa miaka michache ikiwa kuna mipango kamambe. Na yote haya yanatrokana na kuwa viongozi wetu badala ya kununua dawa wanachukua fedha hizo na kuziweka ktk uboreshaji wa madangulo la Umalaya (uwekeshaji bomu). Wanazidi kuagiza madawa feki na ujenzi wa vituo vya afya visivyokuwa na dawa wala mipango kamambe ya kuponya gonjwa hili la Umaskini.

Hayo ndio mawazo yangu! tofauti kati ya dharura na maisha ya kila siku!
 
Ninamaana, misaada inayotolewa na wafadhiri - priority ni Elimu.
Miundombinu ni mhimu, fanya juu chini kuishughulikia hata kwa pato la ndani na harambee ya wananchi. Barabara za tope nyingi vijijini kote zimechimbwa na nguvu za wananchi. Endelea kuziimarisha kadri ya mafanikio ya "Elimu" yatakavyoendelea kuimarika.

Kalamu,
Pesa za kodi ndo zitumike katika elimu au misaada? Kama wewe ni baba wa familia ni vyema kweli Wafadhili wakusomeshee watoto wako na wewe utumie mapatao ya ndani katka barabara? Mimi I would prioritise kusomesha kwa mapato ya ndani- na kama ukipatikana msaada ujenge barabara!
 
Kalamu,
Pesa za kodi ndo zitumike katika elimu au misaada? Kama wewe ni baba wa familia ni vyema kweli Wafadhili wakusomeshee watoto wako na wewe utumie mapatao ya ndani katka barabara? Mimi I would prioritise kusomesha kwa mapato ya ndani- na kama ukipatikana msaada ujenge barabara!

Mzalendohalisi, ni sawa mawazo yako. Kama hela ya ndani ipo kutosheleza malengo yaliyowekwa kwa kila mwaka kufikia maendeleo ya elimu kilichokadiriwa kufikiwa. Kama pato la ndani halitoshelezi kufikia hayo malengo ya mwaka nitasitisha miradi ya barabara kwa muda. Hakuna ubaya wowote kwa kutumia pesa ya misaada kwa kuendeleza elimu; ni kiasi cha kupanga tu na kukubaliana na wafadhiri. Usisahau, wengi wa wasomi wetu hapa Tz wamesoma kwa misaada hiyo hiyo. Ninathubutu hata kusema kuwa asilimia zaidi ya tisini za Ph.D. hapa zimepatikana kwa pesa ya misaada.
Mikakati yote inayofanyika sasa hivi kufufua elimu, Primary hadi sekondari unazozisikia kila leo, angalia kama si mikopo au misaada; pamoja na madeni tuliyosamehewa! Sasa mimi nasema, hayo madeni tuliyolimbikiza miaka yote hiyo ambayo sasa yanasamehewa, sehemu kubwa ya madeni hayo tungekuwa tumeyaelekeza kwenye elimu, hali yetu wakati huu ingekuwa nafuu zaidi kuliko tuliyonayo sasa hivi!

Naomba uelewe kuwa sipingi 'Infrastructure' kuwa mhimu sana katika jitihada za kuleta maendeleo. Lakini kwa maoni yangu ni kwamba msisitizo maalum kwa kipindi cha miaka kadha ningekielekeza kwenye elimu kwanza.
 
Mkandara, nimefurahishwa na 'analogy' yako kama ulivyoitumia katika mchango wako #45 hapo juu. Kwa bahati nzuri nimeweza ku-relate vizuri na mfano wako huo kwa ufahamu nilionao katika mabo hayo.
Kwa ufupi tu huo ugonjwa wa TB na yule mgonjwa uliyemzungumzia - sio masihala hata kidogo; hawa jamaa hapa na CDC (Center for Disease Control) yao wako mbali sana. Nadhani huyo rafiki yako daktari hakutaka kukufunulia zaidi. Kuna 'Superbugs' wasiosikia dawa yoyote ile. Huyo mgonjwa waliyetaka kumwondoa sehemu ya pafu kwa dhana ya kuwaondoa hao wadudu nadhani ilikuwa ni haraka ya kihelehele, ipo kila mahali, na hasa hapa ambapo pana ushindani kati ya wataalam mbalimbali kuonyesha umahiri wa fani zao. Mfano mzuri ni katika ugonjwa wa saratani ya titi (breast cancer), ambapo miaka michache tu iliyopita kila mama aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo, tiba ya mwanzo ilikuwa ni kisu (surgery). Mambo yamebadilika sana sasa hivi, na sio kwa sababu ya kupatikana dawa za uhakika zaidi kutibu ugonjwa huo, bali pamekuwepo na uelewa zaidi katika fani mbalimbali za matibabu za ugonjwa huo.

Ugonjwa wasioujua kabisa hapa ni malaria. Bahati yako ulipokwenda na kurudi hukupatikana na janga hilo. Mimi liliwahi kunipata. Ilikuwa ni pata shika kweli.

Haya, mjadala wetu mhimu wa ugonjwa wa maendeleo.
mimi ningeufananisha umaskini na ugonjwa sugu (chronic disease). Hauhitaji "emergence treatment" na hauui kwa masaa au siku. Kuendeleza kilimo (kwa kuwawezesha wananchi) ni dawa; lakini sio dawa ya dharura ili kuokoa maisha. Hii ni dawa ambayo mgonjwa ataambiwa aendelee kutumia kwa vipimo mahususi kwa kipindi maalum, au hata katika sehemu nzima ya maisha yake, kama ilivyo na matibabu ya HIV.

Ili kupunguza idadi ya watu wanaokabiliwa na ugonjwa huu, kazi mhimu ni kuzuia, au kuendelea kupunguza kwa kasi usiwapate vizazi vipya. Dawa ya uhakika ni elimu. Piga picha katika darasa lako pale Kibara madukani. Mliofanikiwa kusogea mbele zaidi, na wale ambao kwa bahati mbaya hawakuweza kusogea. Kuna rafiki zako wengi tu ambao kama wangewezeshwa kusogea miaka minne tu mbele maisha yao wakati huu yangekuwa ahueni kidogo na yalivyo sasa. Na hii ingekuwa ni katika kizazi kimoja tu baada ya kupatikana uhuru. hata kilimo chao kingekuwa ni tofauti kabisa na hiki ulichokuta wakishughulika nacho wakati huu. Ninaichukulia elimu kuwa dawa ya kutibu 'acute disease' (ugonjwa unaoshambulia haraka).
Wakati mwingine huwa ninajiuliza jinsi CCM ilivyofanikiwa kujipenyeza kila sehemu ya nchi yetu. Pangekuwepo na mafanikio ya aina hiyo katika elimu tungekuwa tumepiga hatua moja au mbili mbele. Ofisi za CCM si ni ktk kila shina au sio?

Pengine mifano ya nchi zilizofanikiwa, na ambazo zimekwama katika mambo haya inaweza kuwa ya manufaa: Hivi tunaweza kusema kuwa Cuba ni mfano wa kuigwa katika mambo ya elimu na maendeleo yao? Haiti je? Viinchi kama Latvia, Ireland, Korea ya Kusini, na sasa hata Vietnam - wanatuzidi nini - Elimu. Sehemu kubwa ya raia zao wamefikia a 'critical mass' ya kwawezesha kuendelea hata bila ya kuwa na utajiri asili.

Napenda nieleweke vizuri. Sisemi kamwe kwamba wakati elimu inapewa status ya u-emergency,; haina maana kwamba shughuli nyingine zinaachwa kabisa.

Elimu bado ni chaguo langu mhimu (emergency) katika mikakati ya kuiendeleza Tanzania ktk muda wa kipindi kifupi na cha kati. Weka miaka ukitaka, 10 - 20 max.
 
Mzalendohalisi, ni sawa mawazo yako. Kama hela ya ndani ipo kutosheleza malengo yaliyowekwa kwa kila mwaka kufikia maendeleo ya elimu kilichokadiriwa kufikiwa. Kama pato la ndani halitoshelezi kufikia hayo malengo ya mwaka nitasitisha miradi ya barabara kwa muda. Hakuna ubaya wowote kwa kutumia pesa ya misaada kwa kuendeleza elimu; ni kiasi cha kupanga tu na kukubaliana na wafadhiri. Usisahau, wengi wa wasomi wetu hapa Tz wamesoma kwa misaada hiyo hiyo. Ninathubutu hata kusema kuwa asilimia zaidi ya tisini za Ph.D. hapa zimepatikana kwa pesa ya misaada. Mikakati yote inayofanyika sasa hivi kufufua elimu, Primary hadi sekondari unazozisikia kila leo, angalia kama si mikopo au misaada; pamoja na madeni tuliyosamehewa! Sasa mimi nasema, hayo madeni tuliyolimbikiza miaka yote hiyo ambayo sasa yanasamehewa, sehemu kubwa ya madeni hayo tungekuwa tumeyaelekeza kwenye elimu, hali yetu wakati huu ingekuwa nafuu zaidi kuliko tuliyonayo sasa hivi!

Naomba uelewe kuwa sipingi 'Infrastructure' kuwa mhimu sana katika jitihada za kuleta maendeleo. Lakini kwa maoni yangu ni kwamba msisitizo maalum kwa kipindi cha miaka kadha ningekielekeza kwenye elimu kwanza.

Una ushahidi wowote wa takwimu kuhusu hilo dai lako? Au unajisemea tu...
 
Kalamu,
Your arguments are very interesting! When you talk of 'critical mass' products in education- which type of education? All levels?
I agree with you- it is now the quality of human resources that count in the development of a country- and not only land, water and mineral resources! When you talk of 'critical mass' do you mean in both quality and quantity? Is it feasible to achieve both at the same time? -will this not lead us to "UALIMU PASIPO ELIMU"?
What we see presently in development of education sector in Tz is construction of many schools without teachers focusing on quantities. What is the point of departure- quality on quantity? Remember if you have limited resources you can not get both!
I would suggest starting with quantitative change (this is what is happening in Tz) then qualitative change! Schools need to be there first then pupils then teachers! The issue of quality you may improve as we go alone- but you can not improve from no where!
Kalamu- one danger I see of having a ‘critical mass’ in education without work to do is frustration leading to brain drain- where most educated citizens leave the country for greener pastures such as Philippines, Ghana or Nigeria- nothing bad with this but it would be nice if the 'critical mass' could be retained to develop Tanzania.
One key challenge is how to retain high quality human resources!
 
Kalamu,
Sawa kabisa naweza kubali hilo chronic disease lakini haina maana kwamba hauwezi kutibika!. Tanzania hatujawahi tumia dawa wala kufuata nyakati za kunywa dawa hizi. Sasa emergence ama sio nitali zungumza mbele!

Nadhani hapa swala kubwa ni hiyo mikopo tunayopewa!...Sote hapa tunapenda sana kutopokea misaada hii ya masharti magumu na zipo nchi ambazo hazipokei kabisa misaada hii pamoja na kwamba wao pia magonjwa yapo kila siku. Budi tuzielewe kwanza tofauti hizi.
Umaskini wetu ndio sababu hasa ilotufanya tujiingize ktk madeni haya mabaya ambao yana sheria toka Upande mmoja tu. Na hawa jamaa IMF wangetuona wajinga sana kama tungekuwa ktk unafuu wa hali tukaendelea kuomba misaada hii.
Hii ndio tofauti kubwa ya fedha hizi na ndio maana hata ukisoma mikakati ya hawa jamaa inatokana na utafiti unaohusiana zaidi na Umaskini wetu. Ukiangalia nchi zote ulizozitaja hapo juu kama Cuba, hatuwezi kuwaweka ktk hesabu ya mfano bora kwa sababu wao pia wamo ktk denial ya maradhi haya kwa sababu wanaamini madawa ya Amerika yana sumu fulani itakayo waua wao taratibu... hivyop basi gonjwa wanalo na wanaendeleza imani yao.

Tanzania tulikuwa maskini kabla ya Uhuru wetu na Mwalimu alipoingia yeye pia alijenga imani ya kuamini miti shamba ya Kichina (Ujamaa). Ni uganga unaokubalika sana kinadharia kwani madawa karibu yote hutokana na miti shamba lakini mzee wangu madawa haya bila vipimo (ELIMU) ilikuwa shida sana kisha kama unavyojua huwezi kumlazimisha mgonjwa kunywa dawa. Atazifutika zote chini ya mto na kunywa maji matupu na ndivyo tulivyomfanya Nyerere ktk Ujamaa miaka ya 80.
Kalamu, watu wanasema mengi sana kuhusu Nyerere na kuanguka kwake lakini sikufichi kabisa kwani wakati huo nilikuwa nachemsha kishenzi mijini. nadiriki kusema kwamba wananchi tunachukua hesabu kubwa ya kutofanikiwa kwake mbali na siasa mbaya ya Ujamaa ktk biashara.
Pamoja na upungufu wa vitu vyote, watanzania walikuwa wakificha mali zetu na kwenda ziuza nchi za jirani ambako walikuwa na njaa kuliko sisi. Sukari, Sigara, Matairi ya General tire, vyakula na kadhalika vilikuwa ndio biashara kubwa ktk ziwa Nyanza na Tanganyika. Sii Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Msumbji watu walikuwa wakipishana na mali zetu kuingia huko tukiletewa sisi Mitumba, sabuni, Colgate na kadhalika (baada ya kupigwa marufuku). Ebu angalia, pima trade hiyo kisha nambie mwenyewe!
Kwa hiyo wenzetu waliokuwa na shida ya vitu muhimu sana ktk maisha waliweza kulipa mara tano ya bei ya Tanzania ambayo serikali iliweka kiwango. Kama watumwa vile jamaa waliweza kutununua kwa shanga!
Kuna watu wengi sana ktk Ukanda wa maziwa walianza kupata utajiri wao wakati ule na hata baadhio ya viongozi wa mashirika ya Umma walipata utajiri wao wakati huo wa shida...
Kwa hiyo kama nilivyosema Tanzania hatujawahi tumia dawa kama inavyotakiwa na hata ile dawa ndogo ya kinyeji ya mwalimu tuliiona chungu.

Sasa wapi napo kosana kimawazo na wewe ktk maelezo yako, ni pale unaposema haihitaji emergence treatment!.. hapa kidogo umeniacha nje kwa sababu kama hatuhitaji dawa haraka hivyo then umerudi pale pale kuwa hatuhitaji misaada hii ya IMF!..
Natofautiana na wewe na kusema Umaskini ni emergence na ndipo napokubali hii mikopo kwa malengo ya tiba ya huu ugonjwa ambao ni chronic. Ugonjwa ambao tayari umetu tufanya kuwa vilema wa kujikokota na magongo.
Hata kama sii ugonjwa wa kutuua kesho, mzee wangu hatuwezi fanya kazi tukiwa vilema na magongo yetu mikononi!..kwa hiyo mbali na Umaskini tunashindwa hata kujikongoja na hata hiyo ELIMU haiwezi kusaidia kitu ikiwa wale wanaotakiwa kuwa ktk uzalishaji ni vilema...Ebu fikiria mshikaji mtu anaenda kazini hali mshahara wake wa mwezi kesha umaliza tahrehe 10 ya mwezi!.. huyu mtu ana watoto sijui wanne wote wanahitaji Chakula, elimu, Afya yao bado hujaizungumzia. Huu ndio Ulemavu naouzungumzia mimi ktk gonjwa hili la Umaskini.
Now, baada ya kuwa tuna madini yote hayo, gas ndipo kidogo hali ya mgonjwa unaanza kuwa na nafuu kwa sababu tunaziuza hizi kwa kupata madaktari toka nje!.. hawa madaktari hawajawahi kupitia Ugonjwa huu - wanausikia tu. Kweli wamesoma sana kama wale waganga wataalam wa US waliokuwa wakizungumzia kuhusu TB. Tatizo ni kwamba wanajua tu elimu ya kitabuni lakini hawajawahi kuumwa wala kuponya mtu! Hata ktk ubishi wa hapo nyuma unaweza kunipa hesabu ya wagonjwa wa TB USA kwa mwaka?.. ni madaktari wangapi wamesha tibu! ukisha pata hesabu nambie unaweza kuta ni asilimia 1 ya madaktari wote wa US wamewahi kutibu mgonjwa wa TB.
Sisi ndio wagonjwa na tunao madakatari pia ambao wamesoma shule kama zao na kizuri zaidi hawa wa kwetu sio tu wame specialize ktk gonjwa hili la Umaskini bali wamewahi kuumwa gonjwa hili la Umaskini. Hata dakrtari wa mifupa ama magonjwa ya wanyama anaujua ugonjwa huu TB kama vile tunavyoujua Umaskini!
(Trust me, mimi namuamini sana huyu daktari wetu wa kibongo alonambia kwamba TB haiwezi kupona kwa siku 10 hata kama iwe ni US au mwezini!.. na wala dalili za kupona haziwezi kutokea ktk muda mfupi kama huo walioutaka hawa jamaa.
Sasa basi tofauti na TB hawa jamaa wanao wagonjwa wa Umaskini pia, lakini tazama basi wao wanaovyoukabili.. wanawapa ZAKA!.. food stamps! kisha ni asilimia chini ya 10 ya population yao.
Leo hii wamekuja na mikakati yao ya KUPUNGUZA UMASKINI ambayo ni dose ndogo kama wanayo itoa kwao hali tanzania ni zaidi ya asilimia 60 kama sio 80 ni maskini. Hawa hawa madaktari wetu hunishangaza wanaposema Tanzania tumepiga hatua kubwa sana kimaendeleo kisha tena hawa hawa watasema pato la mtu kwa siku ni chini ya Dollar moja!.....come on guys, average ya pato la Mtanzania kuwa sTsh 1000 unasema tumepiga hatua hali huwezi kununua hata kilo la mboga!

Mshikaji bado nadhani Umaskini ni dharura! unahitaji sana emergence teatment na ndio maana tunachukua mikopo laa sivyo basi hatuna haja kabisa ya hiyo mikopo ikiwa Umaskini wetu utawekwa ktk long term plan!..
Umaskini ni kama magonjwa mengine hatuwezi kuumaliza kabisa, watakuwepo wagonjwa lakini sio kwa asilimia tuliyokuwa nayo!...pia kumbuka hao wasomi ni binadamu wanao ogopa maradhi haya yanayo ambukiza, watafanya kazi vipi ikiwa hakuna sheria, utaratibu na nyenzo za kufanyia kazi.
Mfano mzuri na wazi kabisa kwetu ni hao viongozi wetu walioshika madaraka wametuweka ktk caranteen! yaani wananchi wote sisi wagonjwa, wao wanacheza golf viwanjani na misuti mikubwa. Kweli ni ujinga kujichanganya na wagonjwa wanaoambukiza!...haya ndio mawazo ya wengi wetu.
Watanzani wote ni wakulima kwa asili na ndio zawadi kubwa ya kipaji Mungu alichotupa... tukitumie!
 
Wafadhili wataka ufafanuzi wa tuhuma za ufisadi
* EU yataka serikali ijibu tuhuma za rushwa

* Yasema isipojibu watu wataamini kuwa kweli

* Pia walipa kodi wao wataka kujua fedha zao zinatumikaje

* Ujerumani nayo yataka ufafanuzi


Waandishi Wetu
Mwananchi

SAKATA la tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali na wafanyabiasha nchini linaendelea kutimua vumbi baada ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) kutaka serikali itoe ufafanuzi wa kina ili kurejesha imani kwa wafadhili na wananchi.

Katika mahojiano Maalum na Mwananchi, Mkuu wa Mabalozi wa EU walioko nchini, Maddens Peter, alisema hadi sasa tuhuma za rushwa dhidi ya baadhi ya viongozi hazijakanushwa na akaonya kama serikali itaendelea kukaa kimya basi huenda watu na nchi wafadhili wakadhani kuwa tuhuma hizo ni za kweli.

"Tuhuma zinaonekana bado hazijakanushwa. Serikali inatakiwa kueleza vema kazi, sera na hata mafananikio yake. Mawasiliano ni jambo muhimu sana kwa nchi wafadhili, hivyo ndivyo demokrasia na utawala bora inavyotaka," alisema.

Peter alisema ni kazi ya serikali kutoa ufafanuzi wa tuhuma hizo ili nchi wafadhili ziweze kuwaeleza wananchi wao.

"Nchi wafadhili wanatakiwa kuwaelezea walipakodi wao jinsi fedha zao zinavyotumika katika nchi hii hivyo tunatakiwa kuwa na ripoti sahihi na ya uhakika ili tuendeleze ushirikiano tuliokubaliana," alisema.

Kuhusiana na ukaguzi unaoendelea Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Peter alisema nchi wafadhili wana wawakilishi nchini Tanzania wangependa kuona uchunguzi wa kina unafanyika na wakaguzi walioteuliwa.

"Serikali iliwaahidi walipakodi kwamba uchunguzi makini utafanyika na sisi tunasema, si kuwa na ripoti ya ukaguzi tu, lakini pia kuona utekelezaji wa mapendekezo ambayo yatatolewa," alisema.

Kampuni ya Ernest and Young ambayo imepewa kazi hiyo, ilianza kufanya ukaguzi wa mahesabu BoT Septemba 10, mwaka huu na inatarajia kumaliza kazi hiyo baada ya siku 60.

Wakati huo huo; Balozi Msaidizi wa Ujerumani nchini Tanzania, Ingo Herbert, aliishauri serikali ya Tanzania kujibu shutuma zote za rushwa zinazotolewa dhidi ya baadhi ya viongozi wake kwa sababu nchi wafadhili zinafuatilia kwa karibu malumbano yanayoendelea na kwamba zingependa kufahamu ukweli.

�Tuhuma zinazotolewa kuhusu ufisadi ni nzito, nasi tungependa serikali ikatoa tamko lake mapema iwezekanavyo kuhusu tuhuma zilizotolewa na vyama vya upinzani dhidi ya baadhi ya viongozi,� alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar es Salaam jana, Herbert alisema ni vizuri serikali ikazingatia misingi ya utawala bora ambayo dhana yake ni uwazi, ukweli na uwajibikaji.

Alisema Ujerumani ni mshiriki mkubwa wa maendeleo ya Tanzania, kwani katika miongo minne iliyopita imetumia kiasi cha Euro bilioni 1.8 kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo hivyo hata walipa kodi wa Ujerumani nao wangependa kufahamu kuwa kodi zao zinatumiwa vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.

Herbert alikuwa akieleza kuhusu wiki ya Ujerumani iliyoanza jana, ambayo lengo lake ni kuwatambulisha Watanzania kuwa Ujerumani ni miongozi mwa washirika wakubwa wa maendeleo nchini, hivyo Ubalozi wa nchi hiyo umeandaa maonyesho ya shughuli zake inazofanya Tanzania chini ya taasisi zake za maendeleo ambazo ni Partner for the Future Worldwide (Gtz), Hanns Seidel Foundation (Hsf), Konrad Adenauer-Stiftung (Kas), Friedrich Ebert Stiftung (Fes), Deutsche Welle na Germany Capacity Building International (Inwent).

Alisema serikali ya Ujerumani imeshiriki katika sekta tatu muhimu za maendeleo nchini Tanzania ambazo ni huduma za afya, miradi ya maji safi na salama na uimarishaji wa serikali za mitaa.

Alisema miradi yote hiyo inaendeshwa chini ya mpango wa mashirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania ambao lengo lake ni kutekeleza sera ya maendeleo ya Ujerumani ambayo ni kusaidia kunyanyua kiwango cha maisha cha watu wa nchi zinazoendelea.

Herbert alisema katika makubaliano ya ushirikiano baina ya Ujerumani na Tanzania, kipaumbele zaidi kimewekwa katika mpango wa serikali ya Tanzania wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini (Mkukuta), ili

kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia ambapo nchi hiyo inaisaidia katika nyanja tatu ambazo ni kukuza uchumi na kupunguza umasikini wa kipato, kuboresha kiwango cha maisha ya watu na huduma za jamii na kukuza utawala bora na uwajibikaji.

Kuhusu suala la utawala bora na uwajibikaji, Herbert alisema wanafuatilia kwa karibu siasa za Tanzania na Ujerumani imeguswa na malumbano yanayoendelea ambayo yanawahusisha viongozi wa serikali na tuhuma za rushwa.

Huyu ni balozi wa tatu wa nchi wahisani wa Tanzania kutoa maoni yake kuhusu tuhuma za rushwa na ufisadi zilizotolewa na Dk Wilbroad Slaa dhidi ya viongozi mbalimbali zinazohusisha ufujaji na upotevu wa rasilimali za umma.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Balozi wa Uholanzi Karel van Kesteren, alielezea kukerwa kwake na tuhuma hizo dhidi ya viongozi waandamizi wa serikali na kutaka serikali itoe tamko lake haraka iwezekanavyo.
 
Date::7/19/2008
Waziri wa Fedha atoka mikono mitupu kwa wafadhili
*Waendelea kuzuia fedha zao za bajeti 2008/09
*Wanataka kibano kwa mafisadi wa EPA, BoT

Na Boniface Meena
Mwananchi

NCHI 14 wahisani zinazochangia bajeti ya serikali, jana zilishindwa kueleza ni lini zitaanza kutoa fedha walizoahidi kwenye bajeti ya mwaka 2008/09 kwa kile walichosema wanasubiri hatua kuchukuliwa dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi.

Jana wafadhili hao walikutana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, jijini Dar es Salaam katika moja ya mikutano yao na serikali kujadili maendeleo yatakayowawezesha kuamua kutoa fedha, lakini hawakutamka ni lini hasa watatoa fedha ambazo zimeahidiwa kwenye bajeti ya mwaka huu.

Taarifa ya maandishi kwa gazeti hili kutoka kwa Mwenyekiti wa kundi la wafadhili hao 14 ambaye pia ni Balozi wa Denmark nchini, Bjarne H. Sorensen, ilisema: "nathibitisha kwamba kundi la nchi wafadhili lilifanya mkutano na Mheshimiwa Mkulo, Waziri wa Fedha na Uchumi.

"Mkutano huo ni sehemu ya mikutano ya kawaida na mijadala ya tunayofanya na Mheshimiwa Waziri, ambako hujadili na kuangalia maendeleo muhimu yatakakayotupa fursa ya kuamua ni lini tutaanza kutoa fedha kwa bajeti ya 2008/09."

Kutokana na kauli ya wahisani hao, inaonekana bado wanaendelea kuiminya serikali hadi itakapochukua hatua zilizopendekezwa dhidi ya watuhumiwa wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA); ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Msimamo huu unakwenda sambamba na kauli waliyotoa wakati wakiridhia kusaidia katika bajeti ya mwaka huu, wakisema:

"Kabla ya kutoa fedha kusaidia bajeti tunatazamia kupokea taarifa zaidi za utekelezaji wa namna serikali inavyopambana na tuhuma za rushwa, kuboresha utawala, na utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) yaliyohusu ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2005/06."

Waziri Mkulo jana aliulizwa juu ya mkutano wake na wafadhili na maamuzi waliofikia, alisema kuwa mambo waliyokubaliana ni mazuri na yanakwenda vizuri.

Mambo yamekwenda vizuri lakini ni vizuri ukawasiliana na Balozi wa Denmark kwani ndiye atakayetoa msimamo wa tuliyokubaliana ili kuondoa kwamba waziri kasema hivi balozi kasema vile, alisema Mkulo.

Wafadhili hao wameahidi kuchangia asilimia 34 kwenye bajeti ya mwaka huu ya Sh 7.2 trilioni, hali ambayo inaiweka serikali kwenye wakati mgumu kama hazitatolewa kwa wakati kwani ndizo zinategemea kuendesha miradi ya maendeleo.

Mara ya mwisho wafadhili kuibana serikali katika bajeti yake ni wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi, waliokataa kufadhili Tanzania kutokana na serikali kushindwa kukusanya kodi kiasi cha Sh bilioni 70 wakati huo.

Makusanyo ya kodi serikalini wakati huo, yaani 1995, ilikuwa ni Sh 28 bilioni kwa mwezi. Kiasi kikubwa cha kodi ambazo hazikukusanywa ilikuwa ni misamaha ya ovyo ya kodi pamoja na wafanyabiashara wakubwa kukwepa kodi. Hali hiyo ilidhibitiwa baada ya Rais Benjamin Mkapa kuingia madarakani.
 
Hawa ni lazima wawe wagumu kutoa kuna aricle ya zamani katika gazeti la The Copenhagen Post.

African officials embezzling aid

24.04.2008

Following revelations of foreign aid going astray in Tanzania, Danish development aid will be scrutinised to avoid inconsistencies

Millions of kroner in foreign aid end up in the wrong pockets in the African nation of Tanzania, reports public broadcaster DR.

According to Arthur Andreasen, a Danish accountant who has worked in Tanzania for 20 years, up to half of the aid does not reach those who need it.

Andreasen recently investigated Norwegian aid to the nation on behalf of the Norwegian government. His report, which caused a stir in Norway, showed that between a third and half of the aid disappeared before it reached its intended recipients.

Danish aid to Tanzania - over 500 million kroner annually -makes Denmark the seventh largest donor to the country.

However, as was the case with Norwegian aid, up to half of the money has wound up in the pockets of corrupt officials and politicians, said Andreasen.

He said one way of embezzling the money was to allocate it for non-existent projects and people. Another method was to write fictitious or excessively high bills and receipts.

His findings caused Erik Solheim, the Norwegian development minister, to withdraw 250 million kroner in support from a nature regeneration project recently.

At the same time, the Norwegian government decided to strengthen monitoring of development aid, but Andreasen said that it was not enough for only one country to react.

'If all governments follow suit, it would have an effect. However, if only one country does it, the recipient country might not react,’ he said, urging the Danish government to heighten its controls on foreign aid.

Ulla Tørnæs, the development minister, told DR that she would address the matter with her Norwegian colleague.

Denmark has been giving aid to Tanzania since the early ‘60s and finances projects dealing with gender equality, human rights, democratisation and corruption
 
Safi sana, lakini it is too little too late! Wafadhili wangeanza kibano cha misaada na kuiendeleza miaka yote, tungekuwa mbali sana! but they were throwing good money after bad na waliendelea kuiweka CCM madarakani kwa kuwapa misaada na kuufanya uchumi uonekane kama unafanya kazi kumbe it has been propped up! Finally things are starting to move in the right direction. Hiyo 34% ya budget ikisimamishwa utashangaa kuona malengo ya 50% ya matumizi ya bajeti yatashindwa kufikiwa, maana tayari hiyo % ni changa la macho! We are SOOOO dependent on donors that we are screwed!
Lakini hiyo 2010 mbona mbali????!!
 
Heshima mbele.... Kuna ndugu aliwahi kusema, "Ni bora kupata kibano kwa kipindi kifupi ili upate starehe/raha ya muda mrefu au kwa vizazi vijavyo".

Swali ni, Je tupo tayari kupokea kibano kwa ajili ya mabadiliko???
 
Heshima mbele.... Kuna ndugu aliwahi kusema, "Ni bora kupata kibano kwa kipindi kifupi ili upate starehe/raha ya muda mrefu au kwa vizazi vijavyo".

Swali ni, Je tupo tayari kupokea kibano kwa ajili ya mabadiliko???

Mimi binafsi naona kama kibano kimeshaanza, na nimekulia enzi za Nyerere wakati sabuni ya Foma ilikuwa kama almasi pamoja na colgate! So no problem, bring it on! Lakini naomba baada ya dhiki kweli tupate faraja. Je Morani, wewe uko tayari kwa ajili ya kibano hiki?
 
Back
Top Bottom