Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 217
- 860
Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa nchi 10 zenye madeni makubwa katika Bara la Afrika ikishika nafasi ya nane kwa kuwa na deni kubwa la nje, huku nchi ya Misri ikiongoza kwa kuwa na deni la zaidi ya dola bilioni 7.2 (Sh 18.76 trilioni).
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC imezitaja nchi nyingine kuwa pamoja na Côte d'Ivoire inayoshika nafasi ya pili kwa zaidi ya dola bilioni 3.6 (Sh9.40 trilioni), ya tatu ni Kenya ikiwa na deni la zaidi ya dola bilioni 2.87 (Sh7.48 trillion), Ghana ikiwa na deni la zaidi ya dola bilioni 2.72 (S 7.09 (trilioni) na Angola yenye dei la zaidi ya dola bilioni 2.43 (Sh6.33 trilioni).
Nyingine ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa na deni la zaidi ya dola bilioni 2.19 (Sh5.71 trilioni), Ethiopia yenye deni la zaidi ya dola bilioni 1.76 (Sh4.58 trilioni) na Tanzania yenye deni la dola bilioni 1.33 (Sh3.46 trilioni) ikifuatiwa na Zambia yenye zaidi ya dola bilioni 1.27 (Sh3.31 trilioni) na Cameroon ikishika nafasi ya 10 kwa deni la dola bilioni 1.15 (Tsh3 trilioni).