Hatimaye EU wakubali kutoa Sh. 860 billioni za maendeleo

Wakuu niwekeni sawa. Hapo mwanzoni wafadhili walikuwa na uwezo wa kufadhili miradi moja kwa moja mfano JICA walikuwa na uwezo wa kufadhili kilimo au barabara fulani. Sasa hiviserikali imekataa na badala yake pesa zote za wafadhili lazima zipite hazina na dheni serikali iamie namna ta kutumia (wanaita Ownership) je huu mpango nyie mnauona je? kuchanganya ahadi tuu za wafadhili na kodi za wananchi na kuzipangia hizo ahadi budget? Kenya nawapa Tano wamesema hawawezi kuweka ahadi za wafadhili kwenye mpango wa matumizi bila kupokea pesa.
 
Misaada/Mikopo kama hiyo nayo ina kasoro zake. Kwa mfano tutapewa mkopo/msaada wa $100 million ambao una masharti kwamba wataalam wa kusimamia mkopo/msaada huo watoke huko uliko toka mkopo/msaada na wanalipwa mishahara mikubwa kutoka katika mkopo/msaada huo huo na pia una masharti kwamba vifaa vya shughuli itakayofanyika lazima vikanunuliwe katika nchi hiyo hiyo pamoja na kwamba vinaweza kuwa ni ghali mno ukilinganisha na bei katika nchi nyingine. Matokeo yake 70 - 80% ya mkopo/msaada wa $100 milioni inarudi katika nchi mtoaji na kwa mantiki hiyo basi msaada/mkopo halisi ulikuwa ni $20 million tu! Kama ni mkopo tumeachiwa zigo la mkopo na riba kubwa tu.

Wakati mwingine hii mikopo/misaada pia inatumika kucreate kazi kwa wananchi wa nchi mtoaji na ndiyo maana hao MATX wengi huwa hawataki kurudi kwao wanapomaliza mikataba yao na wengine hutoa mchozi ili kubaki bongo au hutafuta jinsi labda kuoa ama kuolewa waendelee kuula. Maana mishahara wanayolipwa kupitia mikopo/misaada hiyi ni minono hata kwao hawapati pesa nzuri kiasi hicho.
 
Kada. Misaada ambayo serikali wanasema inaitwa (ODA) Hii inaiclude loans and grants. Nchi yeyote duniani inakopa hata US wanakopa na wanadaiwa. Tatizo ni vipi hizo pesa zinatumiaka?
Mfano Japan baada ya vita II ya dunia ilipata misaada na ndio ikaweza kutake off hii ni kwamba misaada ilitumika vizuri. Kama unakumbuka kitu kinaitwa Marshal plan hii ilikuwa ni misaada ya kujenga uchumi na zilitumika vizuri. South Korea, Malaysia, Thailand (Tiger countries(miracle economies)) na China wote walikuwa aid recipient countries lakini sasa wamegraduate from Aid recipient to aid provider hwa walipata misaada ambayo waliitumia vizuri kwa infrustructures, human capital na busness invironment kuiwezesha secta binafsi. Mfano kwa sasa hivi tanzania na Vetnam ni pilot study ya General budget support programme lakini angalia nature ya misaada na matumizi ya ke kwa Vetinam na Tanzania ni tofaut kabisa. Vetnam ni kuimarisha infrustructucture both human and physical lakini sisi ni good governance, corruption etc. Tofauti hapa nini? Ni kuwa ya Vertnam imelenga Economic growth and attraction of FDI by good investment environment na hivi karibuni tuu nakuambia nao watagraduate. So misaada sio mibaya ila misaada itumike vizuri kama njia ya kutupeleka kwenye self dependancy.Wakuu niwekeni sawa. Hapo mwanzoni wafadhili walikuwa na uwezo wa kufadhili miradi moja kwa moja mfano JICA walikuwa na uwezo wa kufadhili kilimo au barabara fulani. Sasa hiviserikali imekataa na badala yake pesa zote za wafadhili lazima zipite hazina na dheni serikali iamie namna ta kutumia (wanaita Ownership) je huu mpango nyie mnauona je? kuchanganya ahadi tuu za wafadhili na kodi za wananchi na kuzipangia hizo ahadi budget? Kenya nawapa Tano wamesema hawawezi kuweka ahadi za wafadhili kwenye mpango wa matumizi bila kupokea pesa.
 
Misaada/Mikopo kama hiyo nayo ina kasoro zake. Kwa mfano tutapewa mkopo/msaada wa $100 million ambao una masharti kwamba wataalam wa kusimamia mkopo/msaada huo watoke huko uliko toka mkopo/msaada na wanalipwa mishahara mikubwa kutoka katika mkopo/msaada huo huo na pia una masharti kwamba vifaa vya shughuli itakayofanyika lazima vikanunuliwe katika nchi hiyo hiyo pamoja na kwamba vinaweza kuwa ni ghali mno ukilinganisha na bei katika nchi nyingine. Matokeo yake 70 - 80% ya mkopo/msaada wa $100 milioni inarudi katika nchi mtoaji na kwa mantiki hiyo basi msaada/mkopo halisi ulikuwa ni $20 million tu! Kama ni mkopo tumeachiwa zigo la mkopo na riba kubwa tu.

Wakati mwingine hii mikopo/misaada pia inatumika kucreate kazi kwa wananchi wa nchi mtoaji na ndiyo maana hao MATX wengi huwa hawataki kurudi kwao wanapomaliza mikataba yao na wengine hutoa mchozi ili kubaki bongo au hutafuta jinsi labda kuoa ama kuolewa waendelee kuula. Maana mishahara wanayolipwa kupitia mikopo/misaada hiyi ni minono hata kwao hawapati pesa nzuri kiasi hicho.


Mkuu nakubaliana na wewe kabisa na hili ni tatizo maana hata hao ma TX wenyewe ni vilaza tuu hawana kitu sasa ukichangia na watu wakiona Mzungu wanadhani ni mtaalam, Ubovu pia upo kwa wataalamu wetu wanaoishauri serikali (Technocrats) na viongozi wetu pia. Wao wanafikiria kuwa ni msaada lakini ukweli ni kwamba si msaada na LDC ni wateje wa hayo mashirika ya kimataifa na hizo nchi tajiri. Kama hatukopi na hatuhitaji misaada then World bank haina kazi. Hizi nchi tajiri nazo hii mikopo sio misaada bali ni biashara kwao. wanapata riba na wanapunguza tatizo la ajira nchini kwao pia. So hapa palitakiwa pawe na mutual benefit lakini viongozi na wataalamu wetu ni vichwa maji.
 
Mtoto wa Mkulima,
Iwe itakavyo kuwa hii mikopo tunaihitaji kwa sababu tuna matatizo!
Na ndio maana hapo juu umekuwa na mitazamo miwili tofauti ktk mipango ya kuthibiti hizi fedha kati yetu na Kenya.
Kisha ebu tazama kitu kingine ni kwamba imekuwaje nchi ambazo zinasonga mbele ni zile zisizo jifunga kitanzi na mikopo hii (Tied Aid Credits)! kisha tutazame tena ni wakati gani nchi zote duniani zimekuwa zikitegemea fedha hizi?....
Naomba somo kidogo unaposema US nao huchukua mikopo hii ya ODA, na wakati upi samahani lakini!

Kwa nini nchi zetu hasa kusini mwa sahara tumekuwa ndio maisha yetu!... ikiwa mpango huu ni transfer of resources then why hawa jamaa wanaenda wekesha China, India na nchi za Asia za mbali ambazo kwanza hawana mikataba kama hii ya UDA na kisha hawa matajiri wenyewe hupewa masharti na kuweka sahihi mikataba ya kubadilishana biashara!
Mtoto wa Mkulima, tuwe macho kidogo ktk swala hili tulitazame kwa maslahi yetu zaidi ya kukubali kuwa watumwa wa kufikiri. Ni lazima tukubali kwamba hata wewe hapo binafsi huwezi ku transfer resources zako kwenda Africa kwa jamaa ama ndugu yako ambaye ni mlalahoi kabisa!.. haaminiki mlevi na mpenda anasa. Utamtumia fedha za kumsaidia leo na kesho huku matusi kibao yakiandamana na fedha hizo, Hivi ndivyo tunavyoonekana ktk nchi za magharibi na ndio maana hutafuta waaminifu nje ya ringo letu na wakafanya biashara nao. Sisi kwetu wanatengeneza njia za kuweza kuchota na ndio maana wana masharti yao kwetu na hakuna masharti yetu kwao!

Sikubaliani kabisa na hii dhana kwamba misaada yao ati ni trasfer of resources kutoka nchi tajiri wakati ukweli unaonyesha kuwa ni transfer of resources kutoka Africa kwenda kwao na kurudi tena kwetu kama finished product.
hata wakati wa mkoloni, mkoloni alitujengea reli, mabarabara, bandari hata viwanja vya ndege kwa sababu hivi ni muhimu sana ktk ukusanyaji wa hizi resources zetu. Wakati ule tuliyaita haya kuwa ni maendeleo na nchi kama Kenya tuliona kama ni London ya Africa!
Na kizuri cha wakati ule dunia ilikuwa ktk mafungu mafungu kiasi kwamba Muingereza hakuwa na ujanja nje ya Kenya!.. Tanganyika tulikuwa chini ya Mjarumani, Zanzibarmwarabu na msumbiji alikuwepo Mreno. Kwa hiyo ktk kila nchi ktk coast zetu hawa jamaa waligawana nchi sio kwa malengo ya kuziendeleza hizi nchi bali kuzitawala na kuchuma.
Leo hii hakuna tena utawala na namna hiyo na milango iii wazi kwa yeyote yule maadam bibie mzuri Africa kesha ridhika na mfuko wa hawa mabwana. Vita ya leo kiuchumi ni kubwa mara mbili ya ile tuliyokumbana nayo wakati wa mkooloni.
Sasa mimi nasema kama kweli tumeamua kuwa malaya basi tujaribu kuwa wale malaya wa high class!..sio machangu doa ambao hata nyumba ya kulala ni taabu!.. tuwe na jicho la ujuzi wa kumtazama bwana mwenye nacho na sio kukubali kuliwa kwa mkopo ati maadam bwana huyu kapanda dau kubwa!..mali tunayo sisi pamoja na kwamba sisi pia ni wahitaji!...
Utanisamehe unajua tena nikisha fika ktk janvi hilo hushindwa kujizuia!.... hata hivyo naomba kuwakilisha.

Kama vile unavyompa fedha ombaomba ukimsisitiza akanunue chakula asiende kutafuta chupa ya gongo ndio hali wanayo tuchukulia hawa jamaa!. Hilo mwanzo pili hawa jamaa wanaweza kuwa wanatusaidia kwa moyo mmoja wakitegemea kesho tunaweza kuwa na nafasi nzuri za kufanya nao biashara lakini sisi macho yetu ni kuendelea kukaa pale na mabakuli yetu kusubiri mwisho wa sala ya Ijumaa!

Hii haitusaidii kitu kama kweli tunafahamu kwamba sisi sio vilema ila ulemavu wetu sio wa viungo bali unyonge wa kutofikiri.
 
Naomba somo kidogo unaposema US nao huchukua mikopo hii ya ODA, na wakati upi samahani lakini!
Mkuu Mkandara narush kidogo nikirudi nitakujibu yote uliyouliza. Kwa hili la US sikusema kuwa wanakopa ODA. ODA hii ni official assiatance Aid. Na hii mikopo ni kwa nchi masikini na wenyewe wanaiita concessional loans but in reality they are not ni kama tool box ya kufix Developing economies. US wana credit reting nzuri na huwa wanakopa kwa kuishu dhamana za serikali kama Bonds na Bills kwa nchi nyingine na Japan is the major creditor kwa US. Na nakuambia US is the Dobtor number one in the world tembelea website ya IFS kwa zaidi.

Mimi tatizo langu sio mikopo na misaada Mkuu Mkandara. Kukopa sio kitu kibaya. Kupokea misaada sio kitu kibaya. Mimi tatizo langu ni kuwa tutakuwa tegemezi hadi lini? je misaada na mikopo hiyo inawafaidisha wana nchi ambao wanailipa na vizazi vyao vitakavyolipa? Je ni akina nani wanafaidika na hiyo nisaada (inawafikia walengwa)? na je masharit ya hii mikopo na misaada ni kwa masilahi ya taifa au kwa wageni? Ofcourse inatakiwa iwe kwa pande zote mbili maana hakua free lunch hakuna mtu anaweza kukupa pesa ya bure! sasa viongozi na wataalamu wetu ndio walaumiwe. Mimi najua kamati ya taifa ya misaada na mikopo hata Attorney General ni mwanachama wa kudumu (soma government loans, grants and guarantee Act 2003 kweny www.mof.go.tz) Hawa ni wataalamu wetu wa sheria na ndio wanaishauri serikali. Kwenye kamati kama hii kuna wachumi pia kama Dr. Bukuku nk. Hawa wanauwezo wa kuishauri serikali na uongozi na wataalamu ndio walaumie. Mimi binafsi mikopo naisupport kama itatumika kwa kazi zinazoweza kulipa hii mikopo direct or indirect.I will come back later.
 
Mkandala nakupa 5,
Wakati wa Marshall plan -strategically WB na IMF viluindwa kutoa mikopo- ambayo by 1960s (10-15 years) tayari matokeo yalishaonekana!
Sasa sisi ni miaka 40 au 50 misaada na mikopo lukuki- mbona hali inazidi kuwa ngumu?
Hili pakacha linavuja- huwezi kuwa na budget support na ufadhili (42%) this year wakati Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema over a trilion Shs (20% of total budget) zimepotea au zimetumika vibaya!
Hizi pesa vinaliwa tena kiulaini.
Je kuna haja gani ya hii mikopo/misaada?
Mimi siamini ktk hand outs!
Kama tunakopa pesa zijenge barabara na kweli barabara safi tuzione- au Hospitali.
Kama hizi pesa zinapotea HII MIKOPO na MISAADA KWA SASA KWANZA ISITISHWE ILI KIELEWEKE!
Umeeenda Mbezi Beach, Mikocheni, Kimara Mbezi N.k ukaona haya mahekalu ya kifahari yanayoporomoshwa na wafanyakazi wa serikali? Duu- ni balaa!!!!
Yet inabidi sisi au watoto wetu waje kulipa haya madeni.
Mimi ndo natofautiana na hii Dhana ya UMATONYA!
 
Guys, take5, all of ya!! Your comments above are truly educational. Thanx!

SteveD.
 
Mtoto wa Mkulima,
Sasa mkuu nimekuelewa vizuri maanake nilifikiria unataka kuifananisha mikopo yetu ya Aid na Grant na mikopo ya hizo Nchi za magharibi. Wao ni biashara kati ya nchi na nchi jambo ambalo linakubalika na ndio hasa maana ya Utandawazi na Soko huria.
Kwa mfano Marekani leo hii wana deni kubwa kwa China linalosababishwa na Wal-Mart ambao wanadhaminiwa na benki zao kununua mali toka China. Hakuna mtu wala nchi inayo fanya biashara kama hizi kwa cash money ni Africa tu ambako bado kabisa tupo nyuma na kibaya zaidi ni kwamba tumefikia mahala pa kutofikiria kufanya biashara ila kuagiza mali, elimu na ajira. SIku zote tutakuwa omba omba hii misaada ya zaka - Official Development Assistance (ODA).
Pamoja na kumchukia kwangu Mh. Mkapa huyu jamaa alikuwa bingwa sana inapofikia kuzungumzia msimamo wa nchi zetu maskini ktk mataifa makubwa. Hotuba zake zilikuwa bomba kishenzi na mara nyingi aliwafunga magoli nchi hizi - Tatizo lake kubwa was to Practice what he preached!.... watu hawa wapo hata ktk misikiti na makanisa yetu.

Siku tutakayo weza fikia kuweka mikataba na hawa jamaa kiasi kwamba maslahi ya taifa letu yako mbele ya kupewa misaada nadhani ndio wakati pekee ambao tunaweza kusema sasa tuna mwanzo mpya!... lakini kama tutaendelea kujikongoja na magongo yetu IMF hali hatuna kilema chochote sidhani kama tutaweza kwenda hata hatua moja mbele.

Tukumbuke tu kwamba misaada ipo kwa dharura na itumike kwa dharura na sio kutegemea misaada hii kuwa ndio solution ya matatizo yetu kimaendeleo. Hii ni ndoto ya maskini ambaye kila siku hushinda msikitini akiomba kuwa ONE DAY YES! Mungu atamsikia kilio chake na kumwangushia bonge la ushindi - Lottery
 
Mkandala nakupa 5,
Wakati wa Marshall plan -strategically WB na IMF viluindwa kutoa mikopo- ambayo by 1960s (10-15 years) tayari matokeo yalishaonekana!
Sasa sisi ni miaka 40 au 50 misaada na mikopo lukuki- mbona hali inazidi kuwa ngumu?
Hili pakacha linavuja- huwezi kuwa na budget support na ufadhili (42%) this year wakati Mkaguzi Mkuu wa Serikali anasema over a trilion Shs (20% of total budget) zimepotea au zimetumika vibaya!
Hizi pesa vinaliwa tena kiulaini.
Je kuna haja gani ya hii mikopo/misaada?
Mimi siamini ktk hand outs!
Kama tunakopa pesa zijenge barabara na kweli barabara safi tuzione- au Hospitali.
Kama hizi pesa zinapotea HII MIKOPO na MISAADA KWA SASA KWANZA ISITISHWE ILI KIELEWEKE!
Umeeenda Mbezi Beach, Mikocheni, Kimara Mbezi N.k ukaona haya mahekalu ya kifahari yanayoporomoshwa na wafanyakazi wa serikali? Duu- ni balaa!!!!
Yet inabidi sisi au watoto wetu waje kulipa haya madeni.
Mimi ndo natofautiana na hii Dhana ya UMATONYA!

Hayo maneno yako kama vile umeyatoa kinywani mwangu. Mimi kila siku huwa nabishana na watu kwenye jambo hili. I am a very practical oriented guy who is more concerned with reality and action rather than ideas and theories. Kama ulivyosema hapo juu ndugu yangu wewe, misaada na mikopo kila siku lakini rumba bado au linazidi kuwa kali. Kwa mtu practical kama mimi nitauliza kwa nini. Ni wazi kuna kitu sio sawa na ninaafikiana na wewe kuwa hii misaada na mikopo isitishwe hadi kieleweke. Lakini nikisemaga hivyo huwa sisikilizwi na watu wanasema eti upeo wangu wa kuchambua mambo ni mdogo. Yeah right....
 
Nyani Ngabu,
Waache waseme wanavyofikiria wao lakini reality on the ground ndio jawabu!. Kuna wakati hekima kama hizi zinahitajika zaidi ya maandishi na maneno matupu. Mapendekezo kama haya watakuona mchawi tu hata ufanye nini pamoja na kwamba wanajua unachozungumza ndio Ukweli.
Zamani mchawi alikuwa ni mtu mwenye roho mbaya, wivu na hatari kwa jamii siku hizi mchawi ni mzalendo, mwenye uchungu na nchi yake wao husema anaifanya mali ya serikali kama mali ya baba yake!
ndio Bongo yetu inabidi mengine tuyakubali kama tunavyofungiwa!
 
Jamani nataka kuuliza kitu kimoja!

Tukipiga marufuku import za mali ndogo ndogo na kuwashauri mashirika ya nje kama wanataka kuuza mali zao kwetu inabidi waje wajenge viwanda vyao ndani nchi kwetu itakuwaje?...
Naomba somo!...
 
Hongera Wafadhili, tena waendelea kutotoa hiyo mikopo/misaada mpaka titakapo set priorities zetu vizuri.
Maana tukisha pewa misaada kidogo basi mshahara wa katibu mkuu na kuendelea mbele unaongezwa, posho ya madiwani inaongezwa, posho za wa bunge zina ongezwa, mashangungu yanaongezwa, wakati tunacho hitaji ni miundo mbini kama barabara, matrekta, maghala ya kuhifadhia chakula, Mabwawa ya kuhifadhia maji, hivyo ndivyo vitu vya msingi, hiyo mishara nma mafao bora kwa viongozi yatakuja baadae , yakiwa ni matokeo ya kuwekeza kwenye vitu vya msingi.
Zaidi ya hapo misaada inau creativity kwa case ya Tanzania
 
Mkandara, Nyani Ngabu, Agust na wengine,
Yaani mmenikuna sana moyo wangu na haya mawazo- kuna siku 2 years ago niliongea haya mambo mbele za wafadhili- basi watu waliniangalia wakasema sina ubinadam- it is a cycle- hawa wafandhili wanatuma watu wao na wanakula huko huko! Kikubwa kinarudi kwao kwa njia ya consultancies, 'technical advice' n.k. Na hii ni advocacy ya elite wa magharibi.
Ndiyo maana inakuwa ngumu ati!
Tukikataa kuna wafdhili wengine watakuja kutupigia magoti basi nakuambia!
 
Jamani huko nyuma niliomba nieleweshwe kidogo kuhusu huu mpango wa Budget support nyie mnauonaje? maana nimesoma document nyingi za serikali kama Joint assistance strategy na Tanzania assistance strategy lakini bado sijapata vizuri inakuwaje kama kuna mtu anaelewa nitashukuru kwa kunipa somo. Analysis zenu zinasemaje?
 
Mtoto wa Mkulima,
1. Kwanza kuna Sector Support mfano Denmark wana Health Sector Programme Support (HSPS), or Agricultural Sector Pr. Support (ASPS) - hizi bado zinaendelea pia kwa sasa. Ila zina limitations- some are concentrated in some Regions- kwa hiyo serikali ikasema why not pull resources together in a common fund to support equally all areas? Ndo kukawa na 'Basket Fund'. Hizi pesa mf. Katika sector ya Afya hupewa Halmashauri zote kulingana na idadi ya watu kwa kila Wilaya.
2. Kuna nchi kama UK philosophy yao ya msaada wape serikali iliyochaguliwa na waninchi- ndiyo in mandate. Kwa hiyo wanatoa direct funding to the Treasurer (Budget Support)- E.g. Japan, EU, etc.
3. Joint Assistance Strategy (New Development)- Development partners coming together in a transparent way and agree priority funding areas, whether is Budgetary Support or Sector Support.
4. USA mara nyingi hapendi kushikiana na wengine- kwa hiyo yuko mwanyewe mara nyingi. May be kwa kuwa ana msuli mkubwa!

I hope others may chip in!
Ila ni maneno tu yanbaddilika kila kukicha Ufadhili ni ufadhili tu!
 
Jamani nataka kuuliza kitu kimoja!

Tukipiga marufuku import za mali ndogo ndogo na kuwashauri mashirika ya nje kama wanataka kuuza mali zao kwetu inabidi waje wajenge viwanda vyao ndani nchi kwetu itakuwaje?...
Naomba somo!...

Ndugu yangu Makandara. Nani atakuja kuwekeza hapa mkuu wakati umeme hamna, bara bara mbovu, bandarini mzigo unachukua mwezi kuclear, kusajili kampuni hadi utoe kitu kidogo, siasa zinzingilia shughuli za kiuchumi. nk. hawajamaa ni enterprenures hawawezi kuja kuwekeza kwetu maana gharama za uzalishaji ni kubwa. Pili jamaa wanafanya dumping kwenye nchi zetu pia lakini tu be honest bado investment environment bado kabisa. Ni carrote to attract investors to come and invest there.
 
Duh!
Sasa ikiwa ndio hivyo, dawa ya umaskini huu ni upi? maanake kama tunavyoona maswala yote ulotaja hapo juu yanajengwa kwa malengo ya muda mfupi. Hasa hizo startegies ukizitazama ni za muda mfupi na zimekuwa zikibadilishwa kila mwaka kabla ya lengo la kwanza halijafikiwa. .
Na huu mpango wa kupitisha misaada yetu benki kuu sijui kama nimekuelewa vizuri lakini nadhani hii kamba tulisukiwa kabla wafadhili hawaja shtukia sol la benki kuu na Mafia!.
halafu kuna wale Independent Monitoring Group walokuwa wakiongozwa na Prof. Wangwe sijui nao wanatumia zaidi elimu yakitabu bila kutoa report kamili ya hali halisi ama nao wamo ktk freezer!.
Tukitaka mikopo ya hizi aids na grant ife nadhani hawa jamaa ndio wa kuwatafuta! kwa sababu sioni kabisa kitu ambacho tunaweza kuweka mezani hawa matajiri wakaweza kutusikiliza sisi kama business partner!
Inabidi kwanza tupigwe na njaa labda ndio tutaweka akili.
 
"Tukumbuke tu kwamba misaada ipo kwa dharura na itumike kwa dharura na sio kutegemea misaada hii kuwa ndio solution ya matatizo yetu kimaendeleo." #29 Mkandara.

Ungeulizwa utaje dharura tatu ambazo zingehitaji kupewa hicho kipaumbele cha misaada ungeiorodhesha miradi ipi? Orodha yangu ni:
1. Elimu
2. Elimu
3. Elimu

Mathalani, miaka 40 hii baada ya uhuru wetu, na baada ya misaada yoote tuliyokwishaipata, hata ile ya kujenga barabara ambazo leo hii tena tunaitafutia misaada ya kuikarabati barabara hizo hizo; kama tungewekeza katika elimu (nikiwa na maana bila ya ubadhirifu tunaoufahamu), si kidogo tungekuwa na wasomi angalao wasiotumia barabara nzuri? Sasa jiulize wangefanya nini!
Mengine yoote yangefuatia baada ya hapo.
 
Mtoto wa Mkulima,
1. Kwanza kuna Sector Support mfano Denmark wana Health Sector Programme Support (HSPS), or Agricultural Sector Pr. Support (ASPS) - hizi bado zinaendelea pia kwa sasa. Ila zina limitations- some are concentrated in some Regions- kwa hiyo serikali ikasema why not pull resources together in a common fund to support equally all areas? Ndo kukawa na 'Basket Fund'. Hizi pesa mf. Katika sector ya Afya hupewa Halmashauri zote kulingana na idadi ya watu kwa kila Wilaya.
2. Kuna nchi kama UK philosophy yao ya msaada wape serikali iliyochaguliwa na waninchi- ndiyo in mandate. Kwa hiyo wanatoa direct funding to the Treasurer (Budget Support)- E.g. Japan, EU, etc.
3. Joint Assistance Strategy (New Development)- Development partners coming together in a transparent way and agree priority funding areas, whether is Budgetary Support or Sector Support.
4. USA mara nyingi hapendi kushikiana na wengine- kwa hiyo yuko mwanyewe mara nyingi. May be kwa kuwa ana msuli mkubwa!

I hope others may chip in!
Ila ni maneno tu yanbaddilika kila kukicha Ufadhili ni ufadhili tu!

Mkuu nashukuru sana kwa hii elimu uliyonipatia. Thanks.
 
Back
Top Bottom