Ruto: “Nimekopa Kidogo”; Treasury: Deni Limeongezeka Sh4.25 Trilioni

Ruto: “Nimekopa Kidogo”; Treasury: Deni Limeongezeka Sh4.25 Trilioni

Omu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
414
Reaction score
86
Rais William Ruto anasema serikali yake imekopa kidogo kuliko tawala zilizomtangulia.

Lakini rekodi rasmi za serikali zinaibua swali: Ikiwa tumekopa kidogo, kwa nini deni la Kenya limefika zaidi ya Sh13 trilioni?

Ruto aliingia madarakani Septemba 2022 wakati public debt ikiwa karibu Sh8.76 trilioni. Kufikia Juni 2026, data ya Treasury na CBK inaonyesha deni la umma lilikuwa takribani Sh13.01 trilioni - ongezeko la karibu Sh4.25 trilioni katika kipindi cha miaka minne.

Hata hivyo, hilo halimaanishi kwamba Sh4.25 trilioni zote ni mikopo mipya. Thamani ya deni hubadilishwa pia na exchange rates, repayments, disbursements na valuation adjustments.

Lakini tukifuata actual borrowing, Treasury bado inaonyesha kiasi kikubwa.

Serikali ilipata takribani Sh759.7 bilioni net financing mwaka wa fedha 2022/23, Sh818.3 bilioni mwaka 2023/24, zaidi ya Sh1.03 trilioni mwaka 2024/25 na karibu Sh983.7 bilioni mwaka 2025/26.

Wakati huo huo, Controller of Budget Margaret Nyakang’o ameonya kuwa deni limefikia 68.5% ya GDP, juu ya benchmark ya kisheria ya 55%, huku takribani 71% ya mapato ya serikali yakielekezwa kulipia deni.

Hapo ndipo hoja ya Rais inahitaji context.

Kusema deni limeongezeka kwa asilimia ndogo kuliko wakati wa Kibaki au Uhuru kunaweza kuwa sahihi chini ya metric fulani, lakini percentages zinaathiriwa sana na starting point. Serikali inayorithi deni kubwa inaweza kuongeza matrilioni na bado ikaonyesha percentage growth ndogo kuliko serikali iliyoanzia kwenye deni dogo.

Kwa hivyo swali halipaswi kuwa tu:
“Ruto amekopa zaidi au kidogo kuliko Uhuru?”

Swali muhimu zaidi kwa mwananchi ni:
Kenya imekopa kiasi gani, pesa hizo zimeenda wapi, na kwa nini KSh7 kati ya kila KSh10 za mapato sasa zinaelekea kwenye deni?

Na ikiwa deni limefika Sh13 trilioni huku serikali ikipanga kuendelea kukopa kufadhili deficits, ni lini hasa Kenya inaanza kutoka kwenye mzunguko wa kukopa ili kulipa yaliyokopwa?
 

Attachments

  • HSKDGxrXYAIlcxJ.jpg
    HSKDGxrXYAIlcxJ.jpg
    105.6 KB · Views: 3
Back
Top Bottom