Hatimaye EU wakubali kutoa Sh. 860 billioni za maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye EU wakubali kutoa Sh. 860 billioni za maendeleo

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by KadaMpinzani, Jul 6, 2007.

 1. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Wafadhili wagoma kuipa serikali mabilioni
  Na Hassan Mghenyi

  BAADHI ya wafadhili walioahidi kutunisha bajeti ya serikali mwaka uliopita, wameshindwa kutimiza ahadi zao na hivyo kukwamisha miradi mingi ya maendeleo.


  Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliyotolewa Juni mwaka huu, inaonyesha kuwa misaada ya wahisani na mikopo nafuu ambayo haijalipwa katika kipindi cha bajeti ya 2006/07 inafikia asilimia 35.


  Katika kipindi hicho, bajeti hiyo ya serkali ilitegemea wafadhili kwa asilimia 39. Jumla ya fedha kutoka nje iliyolipwa ni Sh939.7 bilioni kati ya Sh1.439 trilioni zilizoahidiwa.


  Katika kipindi hicho, kiasi cha mikopo yenye thamani ya Sh673.8 bilioni kiliidhishwa na wafadhili, na sehemu ya fedha hizo zilitumika kupunguza pengo la bajeti na sehemu iliyobakia ilitumika kulipa deni la ndani.


  Wakati hali ikiwa hivyo, serikali katika mwaka huu wa fedha imeongeza utegemezi wa fedha za wafadhili katika bajeti yake kutoka asilimia 39 hadi asilimia 42.


  Vile vile serikali imeongeza utegemezi wa fedha za nje katika miradi ya maendeleo kutoka Sh1.092 trilioni mwaka jana hadi Sh1.462 trilioni mwaka 2007/08, sawa na ongezeko la asilimia 33.9.


  Kwa mujibu wa ripoti hiyo, deni la taifa limeongezeka hadi dola za Marekani 6,112.4 milioni kufika Mei mwaka huu kutoka dola 6,041.6 milioni Aprili mwaka huu na sababu zinazoelezwa ni kutokana na shughuli za serikali na kupungua kwa thamani ya shilingi.


  Kati ya deni hilo, asilimia 75.9 ni la nje na silimia 24.1 ni deni la ndani. Hadi kufika Mei mwaka huu deni la nje liliongezeka hadi kufikia dola za Marekani 4,636.3 milioni kutoka dola 4,597.2 milioni mwezi uliotangulia, ambalo ni ongezeko la asilimia 39.1.


  Ripoti hiyo inaeleza kuwa watumiaji wakubwa wa fedha kutoka nje ni serikali kuu ambayo imetumia dola za Marekani 2,684.3 milioni sawa na asilimia 78.1, sekta binafsi dola 583.2 milioini (asilimia17) na mashirika ya umma dola 167.6 milioni (asilimia 4.9)


  Mchanganuo wa ripoti hiyo unaonyesha kuwa deni la ndani nalo limeongezeka hadi kufikia Sh1.857 trilioni mwishoni mwa Mei mwaka huu kutoka Sh1.846 trilioni Aprili 2007 na sababu inayoelelzwa hapo ni amana za serikali ambazo ni asilimia 99.1.


  Wadai wakubwa wa deni la ndani ni benki za biashara asilimia 43.2, mifuko ya pensheni asilimia 28 na Benki Kuu asilimia 19.2.


  Kuhusu matumizi ya serikali ambayo yamekuwa yakiisumbua serikali kwa muda mrefu, yalifikia Sh3.796 trilioni kwa mwaka wa fedha 2006/07, wakati makusanyo ya kodi za ndani na fedha kutoka nje zilifikia Sh3.377 trilioni hadi Mei 2007, na kusababisha upungufu wa Sh419.7 bilioni.


  Katika bajeti yake ya 2006/07, serikali ilikuwa imepanga kutumia jumla ya Sh4.85 trilioni ambapo makusanyo ya kodi za ndani yakiwa Sh2.46 trilioni na fedha kutoka nje Sh2.226 trilioni.


  Serikali katika mwaka wake wa fedha mpya (2007/08) inategemea kutumia jumla ya Sh6.067 trilioni, kati yake makusanyo ya kodi za ndani ni Sh3.502 trilioni na fedha za nje ni Sh2.549 trilioni.


  Serikali imetenga kutumia Sh3.866 trilioni kwa matumizi ya kawaida na matumizi ya miradi ya maendeleo ni Sh2.201 ambapo kati ya hizo fedha ya nje ni Sh1.462 trilioni.

  source: http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=361

  maoni yangu binafsi ni kwamba mie naona afadhali sana tena sana kabisa serikali yetu kunyimwa pesa kama mambo yenyewe yataendelea kuwa hivi, wee fikiria mtu kila mwaka anafikiria kukarabati ofisi yake, nyumba yake na mapati kila leo, mambo haya wapi na wapi jamani ? sasa kilichobaki nadhani ni serikali kuanza kupata hasira na inachotakiwa kufanya ni kuisafisha serikali nzima ikiwa pamoja na viongozi wake.
   
 2. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 0
  Juzi naona WB wametoa $ 60 Million kwa ajili ya sekta ya Afya...
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  Jul 6, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  KadaMpinzani,
  Mimi siamini kwenye AID or HAND OUTS ili kutatua matatizo tuliyo nayo- labla on purely humanitarian reasons- ukame, mafuriko n.k. Ndo maana hatuendelei!
  Pia hata hizo $ Mil. 60 Icadon ktk Afya- sii zinaiishia kujenga majumba ya kifahari ya wakubwa? Mwananchi wa kawaida haambulii kitu!
  Kuna ufafiti ulionyesha kuwa about 50% ya budget huishia hapa katkati- serikli kuu hadi Halimashauri- siyo chini zaidi- haiwafikii walengwa. Hebu angalia Mapungufu ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali yaani bilions of Shs zimepotea au kutumika vibaya- yet hakuna aliyechukuliwa hatua!
  Sii heri tu msaada usije ili kweli ya ulaji ieleweke?
  Yafaa nini kuendelea kuweka katika pakacha linaloendelea kuvuja?
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Mzalendohalisi, ndio maana nikasema nasapoti kabisa serikali kunyimwa pesa. yaani inasikitisha sana kuona wapi hizo pesa zinapoishia.
   
 5. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #5
  Jul 6, 2007
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Je inawezekana kuwa na citizen campaign against foreign donations, loans and handouts? Vitu hivi ndivyo vimelemaza kabisa nchi yetu, na nashangaa kabisa kuwa viongozi wetu wanavionea ufahari. Inabidi watanzania tuamke tivipige vita. Misaada yote isiwe inapitia serikalini, badala yake iende kwa wananchi moja kwa moja kama nguvu ya ziada baada ya serikali kuwa imetimiza wajibu wake kwa raia.


  Hebu fikiria wewe kama baba wa familia yako, tuseme una wake wawili na watoto kumi wanoakutegemea lakini eti huwezi kuwahudumia. Sasa kwa vile huna uwezo unaenda kuomba msaada kutoka kwa mtu mwenye uwezo, naye anakuambia kuwa atatoa msaada kwa kuwanunulia watoto wako na wake zako nguo pamoja na mahitaji yao mengine kama matibabu; wewe uwe unanunua chakula tu pamoja na mavazi yako mwenyewe. Je kweli utaona ufahari wowote katika familia yako? Je jamaa huyo akiwanunulia wake zako nguo za ndani zinazowasha mwili wewe utasema nini?

  Ni kama mfano huo wa familia, ndiyo maana inabidi serikali yetu pia ione aibu hiyo kwa kuondoa kabisa component ya bajeti inayotegemea misaada na mikopo. Kama msaada utakuja basi tutaupokea na kuongezea juu ya uwezo wetu lakini tusiishi kwa kutegemea misaada na mikopo kabisa. Zamani hizo Azimio la Arusha lilitufundisha hivi: "Kujitawala ni kujitegemea. Kujitawala kwa kweli hakuwezekani ikiwa taifa moja linategema misaada na mikopo ya taifa jingine kwa maendeleo yake."
   
 6. t

  tz_devil JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2007
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 272
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ninadhani strategic sanctions inaweza ikafanya kazi na wananchi tunaweza kufanya kampeni ya sanctions na ikafaanikiwa. Africa ya Kusini kwa mfano, walifanya wakati wa ubaguzi wa rangi (apartheid) na walifaanikiwa. Misaada inatolewa in the name of mwananchi wa kawaida, lakini haimfikii mlengwa (mwananchi). Kunafaida gani ya msaada ambao haumfikii mlengwa? Let us sanction these people.
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2007
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kuna taarifa moja hivi niliisikia kutoka bbc, itabidi niitafute niipate,kwani ilielezea vizuri kweli kuhusu mambo ya kutegemea misaada na madhara yake. mambo ya misaada kusema ukweli yanatia aibu na kama Kichuguu unavyo eleza, misaada wakati unauwezo kweli ni aibu za nguoni. kila kitu tanzani kipo, kinacho hitajika ni ununuzi tu wa haki miliki za kutengenezea mitambo, hati miliki za michoro ya mabara bara, majengo, madaraja n.k., na pia kinacho hitajika ni hela za kununulia vifaa vya kisasa ambazo zinaweza kutokana na kualika wawekezaji au katika makusanyo ya kodi. maisha yetu yanaweza yakaonekana duni kwa miaka mitano hivi tu, lakini baada ya kujiondoa kwenye utegemezi huu wa misaada, maisha yetu yatakuwa bora maradufu hapo punde tu. Tukumbuke nchi nyingi za mashariki ya mbali zimejikomboa zenyewe baada ya kuepuka misaada mingi na masharti yake na sasa ni vivutio vikubwa vya kitalii na maendeleo katika jamii.

  SteveD.
   
 8. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  SteveD, Kichuguu na Tz Devil pokeeni 4,
  Mnajua Bajeti ya Jirani zetu Kenya 100% ni self financed? Wakati ulo wa Moi in 1990s wafadhili waligoma kumpata tafu Moi- akawaambia waishie! Kwa hiyo mwanzoni ilikuwa shida ila sasa wamesimama! Budget 100% ni kodi yao- ukuja msaada Inshalah- usipokuja- ok.
  Yet sisi tumeongeza utegemezi to 39% to 42% mwaka huu.
  Je huko ndo kusonga mbele? Na zaidi kuna pesa za Millenium Challenge toka US ambazo zinasubiriwa sana kwa ham- na karibu kila jibu Bungeni in this budget serikali injibu tusubiri pesa hii!
  Huku ndo kusonga mbele?
   
 9. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2007
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,718
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  Madhara makubwa ya misaada/ufadhili ni kukosa uhuru wa kujiamulia mambo.

  Ukiona serikali inajisifia kwa kufanikiwa kupata misaada mingi, ujue kuna tatizo la msingi katika fikra za watawala.

  Misaada hutumika tu as a bridge kujijengea uwezo wa kujitegemea huko mbele ya safari.

  Angalia Tanzania: Mwaka huu utegemezi kwa wafadhili ndio kwanza umeongezeka.

  Serikali makini inatakiwa kuwa na mkakati. Kwa mfano: Mwaka 2006/07, utegemezi katika budget ni asilimia 39. Mwaka ujao, mkakati wetu ni kupunguza utegemezi kwa asilimia labda 2, na kufikia 37%. Wakati huo huo kubuni vyanzo mbali mbali vya mapato vya ndani.

  Kupunguza utegemezi kutoka nje ndio kuongeza uhuru na usalama wa nchi. Kwa sasa hivi nchi yetu sio huru wala salama kwa asilimia kubwa.


  Do we have strategic thinkers in the JK government?
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Jul 7, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Lakini jamani ebu nambieni kitu kimoja!
  Inakuwaje wasomi wengi humu wanaweza kuliona hili lakini sio viongozi wetu?... Je hii inatokana na maelezo ya Invincible hapo juu kuwa ni Tatizo la msingi katika fikra za watawala!.

  Kusema kweli nashindwa kabisa kuelewa jinsi tunavyofikiria ama wanavyo fikiria viongozi wetu wanapofikia swala hili tena huona siafa kubwa kulitangaza bungeni pale tunaposamehewa!.
  Je, kuna uwezekano kweli viongozi wetu wanafikiria kwamba Tanzania inaweza kuwa nchi ya kwanza duniani kuweza kuendelea mbele kutokana na mikakati ya ukombozi ya IMF na mfuko wa mtu mwingine?

  kama alivyosema Kichuguu, hii familia yetu ina wazazi vichaa kabisa hasa pale wanapozidisha hesabu ya wake (mikataba feki) kila wanapopewa msaada. Hivi kweli ni akili hiyo wakati watoto wako wanashinda njaa, mwanamme mwingine anasimama kulea famila yako kisha wewe kwa upuuzi wako unaongeza wake zaidi!.

  Sintawalaumu WB hata kidogo ikiwa sisi wenyewe hatujafikia kutambua kuwa umaskini ni kilema badala yake tunatumia kilema hiki kama ndio kitega uchumi cha kusimama msikitini kila Ijumaa!...tukilalamika kuwa ni kazi ya Mungu - Aliyewapa wao ndiye katunyima sisi!
   
 11. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #11
  Jul 7, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  kitu kimoja, watu wengi wanadhani kwamba misaada inatusaidia ( raia ) kumbe hapana, nadhani kwa njia moja ama nyingine ndio kwanza inwalemaza viongozi wetu mpaka wanaanza kuwasahau wananchi wake. serikali isipewe misaada kwa miaka 30 au 40 ijayo ( unless there is a need to ) lakini kama hamna isipewe halafu tuone kama hawatoamka !
   
 12. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2007
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,867
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mkandala,
  Ni matatizo ya fikra ya watawala wetu wa sasa! Lakini pia upeo (vision) ni mfupi. Ni ile ya kufikiria tu 5 years CCM ifanyeje kupata kura/kula!
  Kubwa zaidi dhana ya UMATONYA kuwa- sisi ni maskini- na hatuwezi kwenda mbele bila msaada!
  Kuna mtu mwenye uzoefu wa mikakati ya namna ya kubadili fikra? Nyerere alisema "Heri umaskini wa raslimali/vitu kuliko umaskini wa mawazo".
  Miaka 40 uhuru imepita- yet as a country tunajipiga kifua eti ufadhili (HAND OUTS) umeongezeka!
  May be hawa watawala wa sasa wanahitaji miwani maalum zaidi kuona kuwa kamwe hatutosonga mbele kutokana na ongezeko la misaada! Macho waliyokuwa nayo sasa inawafanya hawaoni au wanajifanya hawataki kuona!
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Jul 7, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  eeeeh bwana wee bonge la point.... Mawili, Wataamka wapende wasipende ama ndio wakati uleee wa kufunga mikanda miaka 17 unaweza rudi!
   
 14. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Hizi pesa za misaada ndio zinatafunwa na wenye meno makali. Angalia BOT scandal ni ya pesa za kutoka nje. Huko ndio kumejaa wizi wa hali ya juu lakini cha kusikitisha ukisha ukwaa umungu mtu masikio unaweka pamba halafu walalahoi wanaolipa kodi wanakiona cha mtema kuni.

  Soma hapa
   
 15. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  yap ! lakini BOT nao wamebanwa wajieleze pesa zimeenda wapi, hapo ndipo kunyoosheana vidole kutaanza. patamu hapo !
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Jul 7, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mimi naomba wafunge kabisaaaa hiyo misaada yaani wafukuzwe kama machinga ambao kwa unafuu mkubwa walijitajihidi kutafuta riziki zao!
  Tukisha fungiwa labda tutakuja tia akili na nina hakika wote wataukimbia Uongozi.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,457
  Likes Received: 81,708
  Trophy Points: 280
  Hata mimi naliunga mkono hili la kufanya kampeni ili Tanzania isipate misaada au mikopo toka mashirika ya kimataifa au nchi za magharibi, Asia na mashariki ya mbali. Sababu yangu kubwa ni kwamba tunapata mikopo na misaada kila kukicha na sasa huu ni mwaka zaidi ya wa saba tangu tuanze kuambiwa uchumi wa Tanzania unaongezeka kati ya asilimia tano hadi saba kwa mwaka, lakini mishahara imedumaa pale pale na ajira haziongezeki.

  Nchi nyingine uchumi ukikua kiasi hicho kunakuwa na neema ya hali ya juu na wananchi wengi wa nchi hizo wanaiona neema hiyo, lakini siyo nchi yetu.

  Sasa hivi tunaambiwa TRA inakusanya bilioni 250 kwa mwezi hii ni sawa na trilioni 3 kwa mwaka au sawa na $3,000,000,000 hii ni pesa nyingi sana, lakini matunda yake bado hatuyaoni! Wananchi walio wengi bado wana dhiki kubwa kimaisha lakini kundi la wajanja wachache wanakuwa mamilionea na mabilionea kila kukicha.

  Serikali yetu bado inaishi kama serikali ya kitajiri kutaka kununua magari ya kifahari ambayo ni bei mbaya na gharama za kuyaendesha ni kubwa mno.

  Kwa hiyo kampeni kama hii ina umuhimu mkubwa kuifanya na watakaoumia zaidi ni wajanja wachache wanaonemeeka na misaada na mikopo hiyo.
   
 18. Mtoto wa Mkulima

  Mtoto wa Mkulima JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2007
  Joined: Apr 12, 2007
  Messages: 687
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mimi kidogo nina mawazo tofauti. Misaada ni muhimu sana katika maendeleo. Miaasa au wanavyoiita ODA is like transfer of resources from rich countries to poor countriies. Tatizo kubwa hii misaada inatumika je? Tunahitaji misaada ya aina gani? Na tunahitaji misaada hadi lini? Tanzania tumekuwa tukipata mizaada tangu tulipo pata uhuru takriban miaka 46 iliyopita. Hapo ndio umatonya wetu ulipoanzia maana tulianza kulia kuwa sisi ni taifa changa tunahitaji kusaidiwa na kuhakikisha tunapata misaada kila kona tukawa na sera ya kutokufungamana na upande wowote. Kipindi hiki tulipata misaada mingi sana kama matrecta pesa za kuanzisha viwanga nk. Mwalimu alikuwa na nia nzuri ya kujitegemea baadae. Lakini hadi leo hatujaweza kujitegemea na hii tabia ya omba omba imekuwa kama gonjwa sugu.


  Tulikuja kuelemewa na madeni yanayotokana na mikopo ambayo faida yake haionekani. Tukalia tukafutiwa madeni na kila siku serikali inajisifika kupata msamaha (Shem on them). Kutokana na hili tulipoteza uhuru wetu wa ndani na Mabwana zetu (WB na IMF) ndio wakatugaragaza watakavyo na vile mkapa alivyokuwa inlove na globalization matatizo tunayaona. Tumegenisisha uchumi wetu, tumegawa rasilimali zetu na tumeuza uhuru wetu. Sasa mabwana zetu tunaowaita development partners kila siku tunazidi kuongeza utegemezi kwao na kujisifia kuwa wafadhili wamekubali kugharamia Budget yetu hii ni aibu sana. Niambie sasa hivi wakisema tumejiondoa na huu utegemezi wa 42% itakuwa je?

  Je hizi pesa zinatumiakaje? Account ya madeni na misaada ya nje BOT ndio account ya kusomeshea watoto wa wakubwa, ndio account ya kuhamisha pesa kwenda Uswiss.

  Kinachotakiwa ni kuwa misaada itumike inavyokusudiwa kwa lengo moja tuu la kuondokana na utegemezi. Tupate misaada ya kutengeneza Miundo mbinu, investment environment na human capital (transfer of Knowledge) sasa hivi ukiangalia kama Good governance na coruption inapata misaada mingi kuliko Elimu na afya. Je kuondoa ruswa tunahitaji misaada ya wafadhili? je uongozi bora unahitaji wafadhili? Naomba niishie hapa maana ninaona nazidi kupata hasira hasa kila nikisoma gazeti naona picha ya Mgonjwa akisaini mikataba ya mabilion mbele ya bendera ya Taifa na wananchi hawafaidiki.
   
 19. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  mimi sishangai kwa nini you are for misaada, simply because " wewe ni mtoto wa mkulima" you need that to survice huku ukilemaza viongozi wetu.
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  lakini hata hivyo mtoto wa mkulima umetoa points nzuri mzee, ebu kua 10 !
   
Loading...