Hata kama hujazoea hiki kitu katika mahusiano, chukua hatua bado mapema sana

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
486
606
Kwa mara ya kwanza unapoingia kwenye mahusiano na mtu, unakuwa hujisikii huru sana kuwa naye, lakini baada ya muda una mzoea mtu huyo na kuanza kuona kila kitu kipo sawa kwako.

Kwa mara ya kwanza unapoingia kwenye biashara, unakuwa pia hauko huru sana na biashara hiyo, lakini inafika muda unaizoea biashara hiyo na kuona kila kitu ni cha kawaida.

Pia kwa mara ya kwanza unapotaka kuanzisha au kuchukua hatua katika jambo lolote, unakuwa haupo huru, lakini ukishaanza tu, unazoea na unaona kawaida kwako.

Hivi ndivyo huwa ilivyo, kwa mara ya kwanza karibu kila mtu huwa hayuko huru kwenye jambo analolianza. Inakuwa hivyo kwa sababu ya hali ya mazoea aliyokuwa ameizoea.

Kutokuwa huru huko kunatakiwa kusikuzuie kitu chochote. Kama ni hatua unatakiwa kuchukua, huko kutokuwa huru kutokana na kitu kipya utakuzoea na kupiga hatua mbele za kimafanikio.

Kuna watu kutokana na kutokujisikia huru sana, wao huwa wanaamua kabisa, kuacha hicho wanachotakiwa kukifanya. Kuamua kutokufanya kisa huna mazoea, ni kosa kubwa sana.

Ni hatari sana kuacha hicho unachotakiwa kukifanya kwa sababu ya kukosa uhuru kidogo, huo uhuru kidogo usikunyime kitu hata mara moja, utazoea na utafanya makubwa ya kutisha.

KITU CHA KUZINGATIA NA KUELEWA, wewe chukua hatua, bila kujali kitu hicho umekizoea au hujakizoea. Kwa kadri unavyochukua hatua, utajikuta unazoea mbele ya safari.
 
Back
Top Bottom