Hasunga: Ushirika unalazimisha wasio wanachama kuuza mazao yao kupitia Vyama. Serikali ina mpango gani kuruhusu Wafanyabiashara kununua kwa wakulima?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga amesema kwa mujibu wa Sheria, Ushirika ni kwa Wanaushirika wenyewe lakini hali ilivyo sasa, Ushirika umekuwa ukiwalazisha watu wasio Wanachama kuuza mazao yao kupitia kwenye Vyama vya Ushirika.

Akiwa Bungeni Dodoma, Hasunga ambaye amewahi kuwa Waziri wa Kilimo amehoji Serikali ina mpango gani kuruhusu Kampuni binafsi na Wafanyabiashara kununua moja kwa moja kwa Wakulima bila kupitia Ushirika.

Akimjibu, Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, "Tunaamini mfumo wa Ushirika ndio njia sahihi ambayo itamsaidia Mkulima mdogo kuwa na 'Collective Bargaining Power' ambayo itamsaidia kupata Haki yake".
 
Kimantik iliekwa kumsaidia mkulima lakin watendaji wamebadili mwelekeo na kufanya ndivo sivyo

Sasa ushirika umekua ni hasara kwa wakulima
 
Kununua moja kwa moja ni kumuumiza mkulima na kumbufaisha mfabyabiashara.

Imagine mnunuzi kangomba ananunua moja kwa moja kutoka kwa mkulima ufuta kwa shilingi 800 - 1,000 halafu anaupeleka kwenye ushirika na kuuza kwa shilingi 2000-2200 kwa kilo!!!

Au anauuza kwa makampuni makubwa kwa bei hiyo!!!!!

Kumsaidia mkulima ingefanyika kama ethiopia. Serikali ianzishe commodity exchange, mazao ya wakulima yauzwe kupitia exchange wakulima wauze moja kwa moja kupitia vyama vyao kwa mfumo wa stakabadhi.

Wakati huo huo wathibiti ujanja ujanja uliyojaa kwenye vyama vya msingi...

Hapo sie wakulima hali itakuwa saaaaaaaafi!!!!!! Tutauza ufuta na dengu zetu kwa bei inayoeleweka

Kazi iendelee!!!!!!
 
Ni simple sana, mkulima mwenye pesa/uwezo hawezi uza kangomba, atapeleka ghalani..

Wanaouza kangomba ni wakulima wenye shida, hawa wasaidiwe kwa mikopo kidogo kidogo ya kujikimu na kuendesha shughuli zao za kilimo na maisha. Hawatoweza kukubali kuuza kangomba.

Tatu, malipo yafanywe kwa wakati, haiwezekani niuze mazao yangu leo then pesa nilipwe baada ya mwezi mmoja. Hii ndio inakatisha wakulima moyo wanaona bora wauze kangomba apate cash..
 
Mfumo wa ghalani ni mzuri sana.

Ila ili kupata bei nzuri lazima mfumo wa maboksi vyama viachane navyo.. teknolojia imekua kufanyike maboresho.

Wanunuzi washindanishwe kwa uwazi.

Hapo ndipo swala la exchange linapokuja .

Na ikiwezekana kuwe na mfumo wa kumlipa mkulima moja kwa moja baada ya makato
 
Mwaka uliopita kwenye Korosho mnada wa box ulikuwa na bei kubwa kuliko wa TMX.. Sijui unafahamu hili??

Swala la malipo ni utashi/uaminifu na usharp wa viongozi wa AMCOS na Maafisa Ushirika.
 
Back
Top Bottom