Wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya soya, Ufuta na Mbaazi watinga Mahakama Kuu Kanda ya Songea kumshitaki Mkuu wa Mkoa

Maguguma

Member
Mar 13, 2023
13
6
Mei 22, 2023, Wakulima na wafanyabiashara wa mazao ya soya, Ufuta na Mbaazi walitinga katika mahakama kuu Kanda ya Songea kufungua shitaka la kupinga waraka uliotolewa na mkuu wa mkoa wa Ruvuma unaowazuia wakulima na wafanyabiashara kuuza Wala kununua mazao hayo kinyume na stakabadhi gharani.

Wakulima na wafanyabiashara zaidi ya 198 walifurika mahakamani kuwasilisha shitaka la kupinga mwongozo huo uliotolewa na Mkuu wa Mkoa ambao unakandamiza Uhuru wa mkulima kutumia mazao yake atakavyo ambapo mwongozo unawataka mazao hayo yauzwe kwa mfumo wa Stakabadhi gharani kupitia vyama vya Ushirika.

Kiukweli mfumo wa Stakabadhi Gharini ni mfumo Kandamizi kwa kuwa wakulima wanakosa uhuru wa kuuza mazao yao kwa bei wanayoitaka wenyewe.

Mfumo huo wa Stakabadhi Gharani umezua migogoro kwa wakulima wa kahawa wa Wilaya ya Mbinga ambapo hadi sasa wengine bado hawajalipwa pesa za msimu uliopita.

hali ilivyo hivi sasa Songea wakulima wakisafirisha soya, ufuta au mbaazi wanawindwa na kukamatwa kama vibaka wakati wanalima wenyewe bila msaada wa serikali.

Serikali kama inawapenda wakulima wa nchi hii iondoe mfumo wa Stakabadhi Gharani kupitia vyama vya ushirika kwani mfumo huo ni mfumo wa kibabaishaji unaowanufaisha watu wa chache na Mabenki pekee!

Wakulima wanatangatanga sana hawana msaada, habari nyingi kwenye vyombo vya habari zinaandikwa za kusifia zaidi kinyume na uhalisia ulivyo kwa hivi sasa.

Aidha kesi ipo Mahakamani huku wakulima "wanyonge" wakisubiri kupata majibu ya haki toka kwa hakimu ambaye yupo chini ya mkuu wa mkoa ambaye ndiye aliyeshitakiwa kwenye kesi hiyo.
 
Mfumo wa stakabadhi ghalani umepitwa na wakati. Hii ni dunia ya free market, soko huria. CCM inataka kuwarudisha wakulima zama za giza za ujinga, zama za giza za ujamaa
 
Watanzania wenzangu, bila kuungana wote na tukakiwasha nchi nzima hakuna mabadiliko. Kila mtu anateseka kwa wakati wake na na sababu yake. Kuna wanaonyang'anywa ardhi, kuna wanaonyang'anywa haki zao, yaani watawala wamejisahau kweli kweli.
 
Hatari nawatakia heri kwenye hilo na nawasifu Mungu awasaidie
 
Kulima ulime mwenyewe, sijui wadudu na dawa juu yako, mvua jua juu yakko alaf ukivuna kuna msengemsenge na kitambi chake amekaa huko anakupangia bei?
Huu ndo ujinga nlikataa nkaacha kabisa kulima mazao yanayotolewa macho na serikali kama pamba, ufuta mbaazi korosho n.k
 
Back
Top Bottom