Hassan Mwakinyo ndio bora wa wakati wote hapa Tanzania. Wabongo wanataka kumshusha

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,525
7,377
20231010_215336.jpg


Wote tunajua kwenye mchezo wa boxing hajawai kutokea bondia mwenye uwezo wa kupigana ngumi hapa bongo kama Mwakinyo.

Dunia nzima inajua Hassan ndio alama ya boxing hapa Tanzania. Ndio biashara kubwa ya ngumi East Africa ukitaka kufanya biashara ya ngumi na upate hela isiyo na longolongo basi mtumie Mwakinyo.

Mwakinyo kaitoa boxing kwenye fight za kwenye bar za Keko na Manzese mpaka ngumi zinapigwa Masaki.
Huwezi mpandisha Hassan ulingoni eti apiganie gari anaijua thamani yake.

Na tatizo ndio linaanzia hapo watu wanashindwa kumtumia kwa urahisi hivyo wanapigana vita ya kumpoteza.

Mnataka mpoteza Mwakinyo ili mbaki na nani?

Anachopitia Mwakinyo alishawai kukipitia Diamond.

Kuna wakati Diamond alipigwa vita na kila mtu kama sio mashabiki wake kusimama nae leo hii tungekuwa tunaongea mengine na sababu walizotoa ni hizi hizi.

Anaringa sana, anajiona mkubwa, anavimba, muda wake umeisha ila aliwaprove wrong na wengine kwa sasa wapo kwenye team yake wanajifanya wanampenda kuliko ndugu zake amebaki kuwachora na kuwagawia riziki.

Mwakinyo awe makini sana na acheze game yake very smart, yupo kwenye nchi iliyojaa watu wenye chuki na roho mbaya zisizo na sababu.

Waswahili ni watu wa kuyakadilia mafanikio, kuna mstari wa mafanikio ukiuvuka hata wale waliokupeñda wanageuka kukupiga vita upotee. Huo ndio uhalisia. Na sasa Mwakinyo ana mtihani wa kupambana na ili kundi ambalo limekuwa kubwa likifanya jitihada apotee kabisa.

Tanzania ni nchi iliyojaa watu wajinga, ujinga ukaleta ugonjwa wa roho mbaya na husda na ikifika wakati wa kumuadabisha mtu mwenye mafanikio uwa wanaungana wanakuwa wamoja.

Kwa sasa asipokuwepo Mwakinyo hakuna mwingine wa kukaribia brand yake ila wenye chuki wanaona bora tubaki na kina Kaoneka. So sad ila ndio taifa letu lilivyo.

Naamini ili suala la Mwakinyo litaisha ila inabidi awe makini sana, na fight yake atayopambana hana option nyingine zaidi ya kushinda. Bila hivyo itakuwa ni sherehe kubwa kwa wenye chuki na roho mbaya.
 
Huyo mnaemsifia anakosa proffesionalism. Huwezi acha pambano kwa sababu ya ugomvi wa kindugu halafu pia ishu kama ile ilibidi imalizwe na management/Team manager.

Sasa yeye kutuma tu mavoice note anatoa lawama kwa promota hataki kampuni fulani kama mdhamini. What a Nonsense
 
Umenena kweli
Wabongo wanamhukumu kijana eti anaringa kwani kuringa kosa kama anaringa na kipaji ni chake kuna shida gani?

Wanamtafutia sababu wamshushe waharibu kipaji cha kijana

Mwakinyo ni brand ameajiri watu

Ana connection za kimataifa

Anaweza kuwasaidia vijana wengine

Wanaleta ubabaishaji kijana ana exposure na international flights anakataa huo uhuni wanasema eti anaringa

Sio vizuri Mwakinyo muacheni kijana apigania ugali wake hicho chama kiwepo kusaidia vipaji na sio kukomoa na kuharibu Tallent za boxers


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo mnaemsifia anakosa proffesionalism. Huwezi acha pambano kwa sababu ya ugomvi wa kindugu halafu pia ishu kama ile ilibidi imalizwe na
Waliokosa professionalism ni waliolazimisha afanye biashara na watu asio na maelewano nae.

Huwezi mlazimisha Kiba au Harmonize afanye biashara na Wasafi kwa kigezo chako unachotaka bila maelewano.

Ndio maana Simba walikataa kuvaa nembo ya GSM japo mikataba ilishasainiwa ila lazima kuwe na maelewano.

Lakini hizi ni sababu zimetafutwa na zitaendelea kutafutwa ili kumshusha mshikaji uzuri wabongo tunajuana vizuri sana.
 
Umenena kweli
Wabongo wanamhukumu kijana eti anaringa kwani kuringa kosa kama anaringa na kipaji ni chake kuna shida gani?
Mwakinyo ni brand kubwa huwezi muokota kama mabondia wengine kina Kiduku.

Pia anapigania Azam afanye investment kama kwenye soka aondoe wababaishaji wa katikati vita yake hiwezi kuwa nyepesi
 
Naamini ili suala la Mwakinyo litaisha ila inabidi awe makini sana, na fight yake atayopambana hana option nyingine zaidi ya kushinda. Bila hivyo itakuwa ni sherehe kubwa kwa wenye chuki na roho mbaya.
Hapo Baba aingie chimbo apige tizi Mwaka mzima mwakani atafute pambano amtie mtu kibano cha kufa ngamia alafu hao PAF Promotion na wengine watamuelewa maana ni njama ya muda mrefu kuhakikisha anapotea akiwaambia wafanye hivi wao wanapita hivi nilimsikiliza jamaa wa PAF nikaona sasa huyu jamaa anafanya Jambo na mtu alafu anafanya kwa kumtegea ili baadae ampeleke Mahakamani sio fair kabisa
 
Nadhani hilo shirikisho la ngumi za kulipwa lijitafakari limefanya maamuzi ya kipumbavu

Serikali hasa waziri wa michezo aingilie kati kijana apambane atafute ridhiki....
Lakini ngumi zinasheria na kanuni zake na ili ukubalike na jamii husika lazima uzifuate, pia nidhamu na upendo ndiyo msingi wa kuijenga jamii husika
 
Waliokosa professionalism ni waliolazimisha afanye biashara na watu asio na maelewano nae.
Huwezi mlazimisha Kiba au Harmonize afanye biashara na Wasafi kwa kigezo chako unachotaka bila maelewano...
Mwakinyo hana management? Kama hana basi sio proffesional kama ulivyo muainisha hapo, kama ana mgt walikua wapi kusawazisha haya yasifike huku?

Kwa nini Mwakinyo anajieleza sana kwenye media? Poster moja yenye mfumo wa barua wawe(Mwakinyo mgt) wamemaliza mchezo.
 
Back
Top Bottom