Ndugu walivyochangia matatizo ya Pogba na Mwakinyo

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,098
12,472
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kazi iendelee.

Damu nzito kuliko maji ndio msemo maarufu unaolezea uzito na ukaribu wa ndugu wa damu lakini msemo huo ni tofauti na dunia ya sasa.

Wakati kule ulaya Paul Pogba akitofautiana na ndugu zake na huku Tanzania Hassan Mwakinyo mashabiki na ndugu zake wakiwa mstari wa mbele kuhakikisha anarudi tena kazi yake ya kunyaa pale kasera jijini tanga. Kwa ambao sio wenyeji wa tanga kunyaa ni kitendo cha kwenda kudowea samaki wa wavuvi baada ya wao kurudi baharini na kuwauza kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya kuwa professional boxer.

Paul pogba alipotofautiana na ndugu zake kwa tabia yao ya kuomba omba hela kila wakati na Pogba kuichoka hali hiyo walianza kumzushia skendo nyingi ikiwemo kaka yake wa damu kudai kwamba Paul Pogba anaroga sana ili afanikiwe kwenye soka na hata kwenye France national team alikuwa akiwaroga wenzake akiwemo Kylian Mbape.

Hawakuishia hapo hapo bado waliendelea kumwandama huku mama yao mzazi akiwa upande wa watoto wake wengine licha ya Paul Pogba kumsaidia kila anapohitaji msaada na kuwa nae bega kwa bega katika kila hatua.

Kwa hali ilivyo inaonekana wameshafanikiwa kummaliza Paul kwasababu mpaka sasa anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kusisimua misuli ambayo adhabu yake inaweza kuwa kifungo cha miaka minne kujihusisha na masuala ya mpira.

Paul Pogba alinukuliwa karibuni kwenye moja ya interview kwamba anatamani angekuwa mtu wa kawaida maana hana furaha na hafurahii kuwa star kwa sasa baada ya kutofautiana na familia yake kwasababu ya pesa.

Hassan Mwakinyo international boxer aliyeipeleka tasnia ya ngumi katika hadhi ya juu na kuwafanya mashabiki kurudisha morali ya kukesha mpaka usiku kusubiria ngumi vita aliyopigwa ni kubwa sana baada ya kuwa juu kwenye masumbwi wakiwemo watu wa karibu na mashabiki ambao walitaka ili athibitishe ukubwa wake lazima apigane na Twaha Kiduku na wengi kudai anamuogopa maana hamuwezi Twaha.

Lakini licha ya Mwakinyo kukataa bado waliendeleza shauku yao ya kuwaona wawili hao wanapanda ulingoni pamoja. Mashabiki ni kawaida kuwasema mastaa wao wanavyotaka lakini inapotokea kwa familia inashangaza sana.

Ni juzi tu hapa shirikisho la ngumi limetoa tamko la kufungiwa kwa Mwakinyo kwenye tasnia ya masumbwi kwa mwaka mmoja baada ya kugoma kupanda ulingoni lakini nilishangaa kuona kaka yake wa damu kumsema na kumkana mdogo wake badala ya kumtetea baadae ikajulikana kwamba wawili hao wana ugomvi wa muda mrefu mpaka kufikia hatua ya wawili hao kila mmoja kutamka asihudhurie kwenye msiba wa mwenzake inasikitisha sana.

kumbuka kaka yake mwakinyo ndio alikuwa kocha wake na manager wake wakati Mwakinyo anaanza safari ya masumbwi ila walikuja kutofautiana kwasababu ya maslahi na ugomvi visasi na chuki vilianzia hapo mpaka juzi hatima yake ilipotimia walimtafuta muda mrefu sana.

Hii ndio Africa ukifanikiwa unachukiwa na ndugu na watu wa karibu kama ilivyotokea kwa Samata kipindi fulani, ndugu bwana hasa wa Africa tuna shida sana.

Mungu awasimamie Paul Pogba na Hassan Mwakinyo maana ndio pekee aliyebaki wa kuwaokoa kwa mnayopitia, maana mashabiki wana furahia, ndugu zenu wanafanya party na kusherehekea lakini Mungu aliyemsaidia Yusuph baada ya ndugu zake kutaka kumteketeza atawasimamia na nyinyi Dunia imegeuka upande wenu, umaarufu wenu umekuwa shubiri badala ya asali.

Alamsik.
 
Kwenye issue ya Hassan kila upande una makosa baina yake na promota! Hiyo ya kunyaa ni Hamis ndio zilikua mishe zake na sio Hassan, na pia suala la kupishana kiswahili Hassan yeye ndio anatia ugumu sana suluhu ipite ila kaka yake (Hamis) yupo fresh tu!
 
Yule kaka mtu kiazi huwezi ukamzungumzia vile mdogo wako badala ya kumtetea tena mbele ya vyombo vya habari.
 
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kazi iendelee.

Damu nzito kuliko maji ndio msemo maarufu unaolezea uzito na ukaribu wa ndugu wa damu lakini msemo huo ni tofauti na dunia ya sasa.

Wakati kule ulaya Paul Pogba akitofautiana na ndugu zake na huku Tanzania Hassan Mwakinyo mashabiki na ndugu zake wakiwa mstari wa mbele kuhakikisha anarudi tena kazi yake ya kunyaa pale kasera jijini tanga. Kwa ambao sio wenyeji wa tanga kunyaa ni kitendo cha kwenda kudowea samaki wa wavuvi baada ya wao kurudi baharini na kuwauza kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya kuwa professional boxer.

Paul pogba alipotofautiana na ndugu zake kwa tabia yao ya kuomba omba hela kila wakati na Pogba kuichoka hali hiyo walianza kumzushia skendo nyingi ikiwemo kaka yake wa damu kudai kwamba Paul Pogba anaroga sana ili afanikiwe kwenye soka na hata kwenye France national team alikuwa akiwaroga wenzake akiwemo Kylian Mbape.

Hawakuishia hapo hapo bado waliendelea kumwandama huku mama yao mzazi akiwa upande wa watoto wake wengine licha ya Paul Pogba kumsaidia kila anapohitaji msaada na kuwa nae bega kwa bega katika kila hatua.

Kwa hali ilivyo inaonekana wameshafanikiwa kummaliza Paul kwasababu mpaka sasa anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kusisimua misuli ambayo adhabu yake inaweza kuwa kifungo cha miaka minne kujihusisha na masuala ya mpira.

Paul Pogba alinukuliwa karibuni kwenye moja ya interview kwamba anatamani angekuwa mtu wa kawaida maana hana furaha na hafurahii kuwa star kwa sasa baada ya kutofautiana na familia yake kwasababu ya pesa.

Hassan Mwakinyo international boxer aliyeipeleka tasnia ya ngumi katika hadhi ya juu na kuwafanya mashabiki kurudisha morali ya kukesha mpaka usiku kusubiria ngumi vita aliyopigwa ni kubwa sana baada ya kuwa juu kwenye masumbwi wakiwemo watu wa karibu na mashabiki ambao walitaka ili athibitishe ukubwa wake lazima apigane na Twaha Kiduku na wengi kudai anamuogopa maana hamuwezi Twaha.

Lakini licha ya Mwakinyo kukataa bado waliendeleza shauku yao ya kuwaona wawili hao wanapanda ulingoni pamoja. Mashabiki ni kawaida kuwasema mastaa wao wanavyotaka lakini inapotokea kwa familia inashangaza sana.

Ni juzi tu hapa shirikisho la ngumi limetoa tamko la kufungiwa kwa Mwakinyo kwenye tasnia ya masumbwi kwa mwaka mmoja baada ya kugoma kupanda ulingoni lakini nilishangaa kuona kaka yake wa damu kumsema na kumkana mdogo wake badala ya kumtetea baadae ikajulikana kwamba wawili hao wana ugomvi wa muda mrefu mpaka kufikia hatua ya wawili hao kila mmoja kutamka asihudhurie kwenye msiba wa mwenzake inasikitisha sana.

kumbuka kaka yake mwakinyo ndio alikuwa kocha wake na manager wake wakati Mwakinyo anaanza safari ya masumbwi ila walikuja kutofautiana kwasababu ya maslahi na ugomvi visasi na chuki vilianzia hapo mpaka juzi hatima yake ilipotimia walimtafuta muda mrefu sana.

Hii ndio Africa ukifanikiwa unachukiwa na ndugu na watu wa karibu kama ilivyotokea kwa Samata kipindi fulani, ndugu bwana hasa wa Africa tuna shida sana.

Mungu awasimamie Paul Pogba na Hassan Mwakinyo maana ndio pekee aliyebaki wa kuwaokoa kwa mnayopitia, maana mashabiki wana furahia, ndugu zenu wanafanya party na kusherehekea lakini Mungu aliyemsaidia Yusuph baada ya ndugu zake kutaka kumteketeza atawasimamia na nyinyi Dunia imegeuka upande wenu, umaarufu wenu umekuwa shubiri badala ya asali.

Alamsik.
Ninakuelewa sana hapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom