Bondia Fadhili Majiha avunja rekodi ya Mwakinyo kwa kufikisha nyota 4.5

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Bingwa wa ndondi Mkanda wa WBC Afrika, Fadhili Majiha na bondia namba moja Tanzania 'Kiepe Nyani' ameweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza kupata hadhi ya nyota nne na nusu tangu nchi ipate uhuru huku akivunja rekodi ya Hassan Mwanyiko na Tony Rashid katika mtandao wa Boxrec.
7250fea5-33e6-46e6-b6a8-73e22c6ac3a9.jpeg
Majiha ameweka rekodi hiyo ikiwa zimetimia siku saba tangu ashinde mkanda wa ubingwa wa Afrika kwa kumchapa kwa pointi Bongani Mahlangu wa Afrika Kusini katika pambano la raundi 10 ambalo lilipigwa kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam.

Majiha au Kiepe Nyani ambaye asili yake ni Mkoa wa Lindi katika Wilaya ya Ruangwa mbali ya kufikisha nyota hizo nne na nusu lakini ameingia katika orodha ya mabondia 10 Bora Duniani akiwa kwenye nafasi ya saba katika mabondia 1,056 wa uzani wa Bantam.

Ikumbwe kuwa Bondia Hassan Mwakinyo ndiyo bondia wa kwanza nchini kufikia hadhi ya nyota nne pamoja na kuingia kwenye kumi bora ya Dunia uzani wa Super Walter kwa kukaa katika nafasi ya tisa kabla ya Tony Rashid kufuatia kwa kufikisha nyota tatu na nusu na kuingia kwenye 20 Bora ya Dunia uzani wa Super Bantam yenye mabondia 1,248.
Fadhili.JPG

Mwakinyo rate.JPG

Tony.JPG
Mafanikio ya Majiha yamekuja baada ya kuchukuliwa na Kampuni ya HB Sadc Boxing Promotion ambayo ndiyo waliohusika kumuandalia pambano lake la kuwania Mkanda wa Ubingwa wa WBC Afrika dhidi ya Bongani Mahlangu licha ya Mtandao wa Boxrec kuonekana kwa majina ya Mghana, Azumah Coffie ambaye jina lilikuwepo baada ya Majiha kumtwanga Harvey Horn wa Uingereza, Novemba 25, 2022.

Chanzo: Boxinghubtz
 
Niliona pambano la huyu jamaa, simply the best, sio kubebwa bebwa kama yule jamaa yenu morogoro.
 
Si ndio kama hii, lakini pia Media nyingi za Bongo hazifuatilii rekodi kama hizi, ni mpaka itokee mtu anayefuatilia awape tip kama hii.
Unaongopa mchana kweupe wewe. Nimejaribu ku-search kwenye vyama vyote vikubwa vya ndondi duniani: IBF, WBA, WBC na WBO kwenye ranking ya bantam, top 10 kwa dunia nimetoka hola kila mahali.
 
Kwa kukurahisishia tu.

Ingia boxrec m search Fadhili Majiha huko utapata kila utakalolihitaji.
 
Alishawahi kushinda pambano huko nje?
mwaka Jana alishinda Uingereza dhidi ya bondia Harvey horn ambaye alikua hajapoteza pambano, na mpaka sasa kapoteza pambano moja alilopigwa na Majiha, na pambano hilo lilikua ndio pambano kubwa kwa siku hiyo
 
Bondia mchovu huyo. Mimi natumia zile sites zinazojulikana na kuaminika. Kujua ku-search na kujua uta-search wapi na nini ni vitu viwili tofauti.
Punguza ujuaji, huwezi kufatilia mchezo kwa kutumia sites, ungekua unaupenda mchezo wa ngumi, unaujua na kuufatilia usingehangaika hata kumtafuta majiha kwenye sites maana uwezo wako uko bayana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom