Kati ya Ibrahim Class (King Class Mawe) na Hassan Mwakinyo Champez (Colorado King/Tornado) nani anafaa kuwa Pound for Pound namba 1 hapa nchini?

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,442
21,137
Ibrahim Class anacheza uzito wa super feather wakati Hassan Mwakinyo anacheza uzito wa light middle weight.

Je kama wangekuwa kwenye uzito sawa unahisi nani angeshinda pambano?


Kwa upande wangu mimi binafsi naona Ibrahim angeshinda pambano ,na kwangu ndio Pound for Pound namba 1 hapa bongo na ndiye Face of boxing kwa hapa bongo na sio Mwakinyo.

Ibra mara nyingi huwa anapigana kwa kutokea nje (outside boxer) na anajua sana kutembea na jab.

Kitendo cha yeye kupigana kwa kutokea nje kinamfanya kuona mashambulizi kutoka kwa mpinzani wake kwa urahisi hivyo ni rahisi kukwepa.

Pia Ibra ana speed sana kuliko Mwakinyo ,hivyo ni rahisi kuingia kwa mpinzani kwa haraka sana kushambulia na kutoka.

Pia Ibra ana shabaha sana na ni mzuri kwenye kupiga combinations za uhakika.

Kitu ambacho Ibra hana ni powerfull punches .


Kwa upande wa Mwakinyo yeye mara nyingi anacheza kwa kuingia ndani (inside boxer) ila huwa anabadilika kama atakutana na pressure fighter hapo atabadilisha mfumo na kucheza kama outside boxer ila huwa sio mzuri na hajui kutembea na jab.

Mwakinyo anapendelea zaidi body punches hivyo kama atakutana na outside boxers kama Ibra ni ngumu hizo body punches kufika .


Njia pekee ya Mwakinyo kumpiga Ibra ni kwa kupitia Knockout ila kupitia points Mwakinyo hatoboi, Ibra ana ngumi za mahesabu sana ndio maana akapewa jina "Class".


Haya ni machache tu kwa haraka haraka .

-1408174071.jpg
-1466662513.jpg
 
Mwakinyo japo sikubaliani na shombo zake ila ni bondia mkali huyo ibrahim class hamfikii hata kwa punje

Tena nlitaka liandaliwe pambano la Class na Mwakinyo
 
Back
Top Bottom