Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

duuuu hapo huna mke kuna point moja ilikuwa inazungumziwa heri kuwa na beki tatu akakutia moyo japo hana hela unaweza kumungulia hata biashara ukatoka lkn hawa wenzetu ni shiiiiiidah hapo huja muoa ila ukimuoa mambo mengi yataend kombo nafuu umefunguliwa njia oa second wife
 
Asee nadhani kuna vitu vingine vibaya aliwahi kukufanyia sema ulikuwa huelewi kwa sababu ya mapenzi...na mama yako kuugua mpaka kuletwa hapa mjini nadhani ni mpango wa mungu kukuonyesha zaidi ubaya wa huyo mchumba wako...mpige chini ahirisha harusi mpaka mwakani then tafuta dem mwingine taratibu...huyo aliyekusaidia nae endelea kumsoma naona anafaa ila hakikisha unampenda na anakuvutia kimapenzi..
 
haaa kwanza asante kwa kunijuza ulinunua plot ya ten million turud kwenye mada wanasema vitu vidogo vina maana kubwa sana katika mapenzi ni ngumu kukushaur uachane nae au uendelee nae kwa kua mwisho wa siku wewe ndo mwenyw maaumzi ndo unajua ni vipi moyo wako umemuelemea huyo dada ila kibinaadam amekosea sana gari na uhai asee mh hajui kama bila huyo mama asingekuona wewe ??

Huyo si mke wa kutoa kaka tusizunguke sanaa,utashangaa mengi Baada ya ndoa endapo utajaribu kumuoa.Endapo itatokea ukakosa kazi hatakusaidia hata ni mbinafsi na anapenda vitu hana utu.Hii hatabadilika amini
Usiamini.
 
wakati mwingine Mungu huwa anakuonyesha dalili zake mapema kuwa kama huyo ni wa kufa na kuzikana, hakika huyo hafai hata kidogo achana nae kabisa ipo siku atakuacha humo ndani peke yako, ki ukweli nakushauri uachane nae sogeza mbele mambo mengine yaendelee,
 
Pole sana ndugu,jipe muda tena kabla ya kufanya maamuzi ya kuoa,huyo mchumba wako wa kwanza hakufai kwakweli hapo amekupa picha ni jinsi gani alivyo rohoni,ni bora kusamehe kosa la kucheat lkn sio kuwa na mtu ambaye anaroho ngumu namna hiyo ni sawa sawa na muuaji tu.
 
Kosea Kujenga Nyumba, Utabomoa, Kosea Kununua Gari Utauza, Lakini Usije Ukakosea Kuoa Utajuta Maisha Yako Yote, Huyo Sio Mke Wa Kuishi Nae, Huyo Ni Wa Kuluka Nae Tu Bass.
 
Akaolewe na gari..oa mke anayependa kutembela wagonjwa na kuwaogesha wagonjwa hata kama sio ndugu zako..awe anajitolea jmosi anaenda Amana anawaogesha wagonjwa na kuwapamujinwa ulezi kwa moyo wake wote
 
Inawezekana ulitumia nafasi yako ya Kum- train huyo dada kumlazimisha akupende. Poleeeeee. Hapo hakuna wa kuoa..jipe muda utafakari.
 
Muache huyo duh hata kujigonga hakujigonga....lazima anachepuka pia.

Wanawake wa tabia hiyo na dharau hata mkiwa wachumba ni hatari...

Asubirie kuolewa na gari....ameuzi bora angebana pesa ila hata hospitali hakwenda tangu mwanzoni...mmmh

Wahi wahi
 
Wakuu narudia tena kuwashukuru kwa Upendo wenu
Kiukweli napitia kipindi kigumu sana
Maana kuna vikao vinaendelea usiku na mchana kutatua tatizo hili
Nilikuja kuomba ushauri hapa wakati vikao vinaendelea ili kupata nguvu zaidi hivyo nawashukuru wote

Pia kazini kuna mgogoro umejitokeza juu ya jambo hili
Lakini unaendelea kutatuliwa kiutu uzima na uongozi

Tukifika mwisho Wa hii tufani nitawapa mrejesho
Kila nikipitia hizi comments zote nakua kama napona rohoni
Nawashukuru sana


we kuwa na msimamo wako bhana, usibadilishe uamuzi...acha wafanye vikao vyao wewe msimamo pale pale..mwisho wa siku ni maisha yako..huyo mwanamke lazima atakuwa mwanga tu si bure..HAFAI hata kusalimiwa huyo..piga chini
 
Piga chini oa mwanamke atakayekuwa msaada kwako mwache na maisha yake anunue gari lake na mshauri awe analipenda gari lake kama unavyompenda mama yako!
 
Katika maisha yule anayekujari katika shida ndio rafiki wa kweli.
Akili kichwan mwako kumuoa mwanamke alieona bora gari kuliko uhai wa mama yako au kumuoa aliyesaidia kuokoa Uhai wa mama ako...
 
haina haja ya kuwa na mshenzi km huyo,huyo lengo lake ni ndoa tu hana mapenzi ya kwel kwako..mshikilie huyo mwenye kukujali ww na mzazi wako.
 
Unasema upo njia panda? Mbona hili suala lipo wazi sana! Huyo mbinafsi hana sifa ya kuwa mke, ni malaya tu wa kugonga basi. Ila huyo aliyekupa msaada wakati unauhitaji bila shaka ndio mke bora, yani hili hata tahira wa pale Milembe anaweza kabisa kuliona, sembuse wewe mleta mada?

Kwa kuongezea tu, kuhusu hilo la kubadilisha bibi harusi nalo sio jambo geni. Maana kaka yangu mkubwa alikuwa katika mkasa kama huu lakini tatizo halikuwa pesa, alikuwa na ishu tofauti kidogo, lakini alibadili bibi harusi na ndoa ilifungwa kama ilivyopangwa! Sasa yupo na mkewe takribani miaka 3 na wanafuraha sana.
 
Wakuu nawashukuru wote kwa mawazo yenu mazuri
Ingawa nipo chini ya shinikizo kutoka kwake na ndugu zake kuwa wameshafika mbali kwenye maandalizi ya send off na kwamba wanadai tuzungumze tuyamalize ila kwa kweli moyo wangu umegoma kabisa
Nawashukuru sana

Pole mkuu...story yako imenigusa sana.Ila huu ni wakati wa kumuomba sana Mungu akusaidie ufanye maamuzi sahihi.Pia jipime moyoni mwako mwenyewe kwanza "JE" bi harusi wa pili na wa kwanza ukiweka mbali matatizo yaliyotokea ni yupi moyoni mwako unamkubali zaidi.....(anavigezo ambavyo ungetamani mke wako wa maisha awe navyo)mimi naona hilo ni jambo la msingi sana na lenyewe kulipa nafasi.Pia msamaha kwa sisi WAKRISTO ni jambo la msingi......kama mtu atajutia makosa yake na kuomba msamaha.
 
NINI UNAJISHAURI KAKA WAKATI JIBU UNALO;HATUOI MTI TUNAOA MKE NA KIPIMO CHA MKE NI UTU.PIGA CHINI HUYO NA GARI LAKE FUATA ANAEMJALI MAMA NA BAADAE ATAWAJALI NDUGU ZAKO.Gud njozi
 
Back
Top Bottom