Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Harusi ipo palepale ila nabadilisha bibi harusi

Wakuu habari za mida,

Mimi ni mfanyakazi wa benki moja ya kigeni sitaji jina, nipo hapa kwa muda mrefu sasa. Nimekuwa na uhusiano na msichana hapa kazini ambae wakati amejiariwa nilikabidhiwa kazi ya kum-train hadi ajue.

In the process of training heri tukajikuta tumekuwa wapenzi, hatimaye wachumba na baadae mipango ya ndoa ikaanza total time ya mapenzi ni miaka miwili.

Juzi kati nilipokea simu kutoka kijijini kuwa mama mgonjwa sana figo inamsumbua akapelekwa hospitali ya mkoa wakampa rufaa aje Muhimbili haraka, nami nilikuwa na laki tatu tu kwenye akaunti yangu maana nilitoka kununua plot milioni
10 siku chache nyuma hivyo nikawa sina kitu kabisa.

Nikatuma hiyo laki tatu aje kwa ndege mengine nitajua akifika. Pale Muhimbili ilitakiwa ifanyike dialysis na then operation kama sikosei, kutokana na uchelewaji wa huduma na mambo kutoeleweka huku mama akiwa na hali mbaya, hivyo tukashauriana tumhamishie Aga Khan.

Tulipofika Aga Khan tuliambiwa gharama nzima ni 1.5 milion na ni lazima utangulize million moja ndio anakuwa admited wakati huo mama alipumzishwa casualty wakisubiri malipo, nikaondoka nikarudi ofisini ili nika raise hiyo pesa nilitake risk hiyo kwa kuwa nilijua pale kazini piga ua siwezi kosa hiyo hela hata kwa kukopa.

Kazini nikaamua nianze na mchumba wangu badala ya kuhangaika na watu wengine kwanza nikachungulia akaunti yake maana nina access hiyo, nikakuta ana 4.2 million na bahati nzuri anaijua ishu yenyewe nikamueleza direct suala pesa, ahadi yangu ni kuzirudisha ndani ya wiki mshahara ukitoka.

Sikuamini masikio yangu aliponijibu kuwa hana hata senti kwenye akaunti kwamba hata nikitaka tuangalie wote nikasema poa nikamuona dada mmoja ambae tupo karibu na ni friends siku nyingi akanipa million mbili.

Mama akatibiwa after two weeks akatoka, mchumba akawa busy na kazi hakufika hospitali isipokua siku mama anaruhusiwa haya yote yanaendelea tukiwa kwenye vikao vya harusi yangu na huyo mchumba.

Harusi ni mwezi Juni tarehe sitataja, wakuu kuna mke hapo? Baada ya mwezi mama akawa vizuri anaendelea na kliniki tu hela ya watu nilirudisha siku nyingi.

Nimekaa nimetafakari sana kuhusu mchumba wangu na nataka ku reverse uamuzi wa kumuoa kwa kuwa ni selfish alikuwa tayari kuona mzazi wangu anakufa na pesa anazo na amekiri kuwa hakuwa na sababu yoyote zaidi ya kusave ili anunue Gari.

Nikiri tu kwamba nilipoenda kumshukuru dada alienikopesha pesa niliguswa sana na utu na upendo alionionesha na tuliongea mengi na nilimuuliza kama inawezekana nikasogeza tarehe ya harusi mbele tuseme July au August then nimuoe yeye maana naijua tabia yake nzuri kwa miaka sasa.

Nipo kwenye crisis: Mchumba analia anaomba msamaha nisibadilishe mawazo mshenga amenipa go ahead mama sijamwambia haya yote, mahari sina shida nayo naweza waachia.

Mimi nimekatishwa tamaa sana na hii tabia kwa kuwa nimemsaidia mambo mengi sana yahusüyo pesa na familia yake kwa ujumla ndio maana hata mshahara wake unakua hauna kazi, bibi harusi mpya alikuwa akija Hospitali na nyumbani kumuona mgonjwa daily wakati yule mwingine hadi nimpigie simu. Nipo njia panda
.

Wakuu ushauri

achana nae huyo asiyemjali mama yako...hana upendo wa dhati na wewe.oa huyo aliyekufariji wakati wa shida...
 
ulipomuuliza huyo binti aliyekusaidia kwamba usogeze siku ili umuoe je amekujibu nini
 
me nakushauri usiharakishie mambo,katisha vikao vya harusi kwanza kwa sababu yeyote ile, kaa chini tuliza akili, fikiria mara mbili, ongea na Mungu,usikurupukie watu hata kama ni huyo mdada wa pili. huyo binti kweli kakosea kama ulishamsaidia na vikao vya harusi vilishaanza hakutakiwa kua na wasiwasi tena.so tulia, endeleza uchumba na huyo mdada wa pili then mkiendelea mpange taratibu siku ya ndoa yenu labda mwakani bt not so soon
 
Kwakweli unapoteza mda zogeza kijiti kwa huyo mwingine. Huyo mkishaishi unaweza kufa kwa maleria kwa kukosa pesa ya dawa wakati yeye ana mamilioni kaweka ndani
 
Huyo si mke wa kutoa kaka tusizunguke sanaa,utashangaa mengi Baada ya ndoa endapo utajaribu kumuoa.Endapo itatokea ukakosa kazi hatakusaidia hata ni mbinafsi na anapenda vitu hana utu.Hii hatabadilika amini
Usiamini.

mimi ni dada jamani wee
 
me nakushauri usiharakishie mambo,katisha vikao vya harusi kwanza kwa sababu yeyote ile, kaa chini tuliza akili, fikiria mara mbili, ongea na Mungu,usikurupukie watu hata kama ni huyo mdada wa pili. huyo binti kweli kakosea kama ulishamsaidia na vikao vya harusi vilishaanza hakutakiwa kua na wasiwasi tena.so tulia, endeleza uchumba na huyo mdada wa pili then mkiendelea mpange taratibu siku ya ndoa yenu labda mwakani bt not so soon
 
me nakushauri tuliza kwanza akili,usikurupuke kuoa hata kama ni huyo bi harusi wa pili,endelea nae mkiwa kwenye uchumba bt sitisha vikao vya harusi kwa sababu yeyote ile,mpange siku ya ndoa hata mwakani bt not now kwa sasa tulia kwanza,huyo bi harusi wa kwanza amekosea alikua hana hisia za huruma,ila kama ulisha msaidia naye alipaswa kukusaidia bila hata kufikiria na isitoshe vikao vya harusi vilikua vimeshaanza so hakutakiwa kua na wasiwasi
 
Daa yani hawa watu! kama mie nilimtega tu huyu wangu kuwa nina shida sn naomba msaada wako wa fedha then I wll pay back.Weeeee hayo maelezo niliyopewa ni balaa.Sijui huwa wanafikiria kwa kutumia nn hawa watu?
 
Hello wise one, there is no discussion here, hakuna jipya km mtu wako unaetaka kumuoa anakupa ishara hii, no need to think twice, hapo hujaoa mambo ni hivi next time atawafukuza wadogo zako kwakua ni mbinafsi so move on with new wife, forget her gari litamuoa na kuendelea na maisha yake, nakumbuka kuna rafiki yangu ilikua hivi hivi akajipendekeza kuweka ndani yaliomkuta mkewe alikuja mmwagia maji ya moto, akalazwa for 1 month hospital, alipotoka akamwambia mama hapa ndio mwisho wetu, ulionifanyia yanatosha, think like your ID ila ingekua mimi nisingefikiria mara 2 hapo.
 
Mshukuru mungu sana kwa maana amejibu maombi yako, ya kupata mke mwema. Endelea kumsihi mungu akudhihirishie huyo mwingine uliyempata. Kama halitatokea jambo lolote funga nae ndoa ndiye mkeo/ wa ubavu wako. uamuzi wako ni wako ni wa busara ila nenda polepole sana fanya hata mwakani kaka, maana unaweza kusababisha stroke kwa huyo mwengine , pia mazingira ya kazi kwenu wote yatakuwa magumu sana.
 
Hili suala approach yako na reaction yako ni muhimu sana.
1. Hapa suala sio kunyimwa pesa wakati ulikuwa ukizihitaji. Suala hapa ni mchumba kutokujua BASIC PRIORITIES kwenye maisha, na hili ni tatizo kubwa kwa wengi.
2. mchumba kutokufanya jitihada za makusudi kujenga familia (Wakati akiwa na uwezo wa kufanya hivyo)
3. Mchumba kuwa mwongo na mnafiki - hana HISIA MWENZA!
4. mchumba kutokuchukua nafasi yake (nafasi ya kwanza ambayo umempa
5. Mchumba kufanya uzembe ambao HANA MAELEZO YA KURIDHISHA NI KWA NINI ALIFANYA HIVYO.

Lakini kuna tatizo lingine hapa:
a) Mzee una very High Expectations kutoka kwa mchumba - wakati yeye ni business as usual (Angalia sana malezi yake na matumizi yake ya muda (labda anaangalia sana TV)
b) Unaonekana kama kuna mambo mengi ya kijinga ameyafanya na ukapuuzia - Labda wewe umekuwa na tabia ya mapuuza na umeacha kumwelekeza na kumjenga ili awe raia safi kwenye familia - My advise is that you should try to take up your role as a man and try to be a leader in your family by directing and advising. Otherwise you might end up with the same disapointing results just on different woman.
c) The issue here isnt the wedding - issue ni wewe umekuja kugundua kwamba mchumba is half cooked, and she is far from ready. Cha kufanya - weigh out- where exactly did you went wrong??????????????????
 
Wakuu nawashukuru wote kwa mawazo yenu mazuri
Ingawa nipo chini ya shinikizo kutoka kwake na ndugu zake kuwa wameshafika mbali kwenye maandalizi ya send off na kwamba wanadai tuzungumze tuyamalize ila kwa kweli moyo wangu umegoma kabisa
Nawashukuru sana

Aibu yako itakufanya udhalilike..achana nao ...hiyo ni familia yao na mtoto ni wao na pia ana mapungufu...uwasikilize kutwishwa zigo hilo...ukiendelea kuwasikiliza lazima wakushinikize katika maamuzi ambayo binti yao atanufaika....kata mawasiliano nao songa mbele....ila muamuzi ni we mwenyewe labda bado unampenda sie tumetimiza wajibu wetu...maana mapenzi yana mambo mengi wakati mwingine ufundi wa mechi nacho ni kigezo unachotakiwa kuki......:😀
 
ni kweli wanawake ni wabinafsi kwenye hela zao. wala usijefikiria kutegemea hela ya mwanamke. lakini kwa hilo lako utajua cha kufanya
 
Namuonea huruma huyu the second dada, maana adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie. Make sure she will be safe and fully protected. hiyo ni vita umeanzisha.
 
Majaribu ya kitoto na wala usimuonee huyu dada , wewe ndiyo selfish wa kutupwa, kwa nini ukachkue hela kwake wakati una kiwanja cha millions kumi? Ungeuza million nane na kumuokoa mama yako ungepata Thawabu kwa mungu na mke mwema, Leo unajinyea mwanamke hujamuoa halafu unamshikia bunduki kichwani. Pumbavu weee toka hapa
 
Achana na hypothetical thinking jaman....ukipata shida wa kwanza kumweleza ni aliye karibu yako...na ndo alichofanya bobby akiamin ombi lake limefika mahala salama...what is 1.5M..inayorudishwa ndani ya week???issue siyo pesa..issue ni muda gani pesa inakuwa na matumizi???
Mtu mbinafsi ni mbinafsi tu na kutoa haimaniishi ndo unacho zaidi...utu unahusika sana
 
Majaribu ya kitoto na wala usimuonee huyu dada , wewe ndiyo selfish wa kutupwa, kwa nini ukachkue hela kwake wakati una kiwanja cha millions kumi? Ungeuza million nane na kumuokoa mama yako ungepata Thawabu kwa mungu na mke mwema, Leo unajinyea mwanamke hujamuoa halafu unamshikia bunduki kichwani. Pumbavu weee toka hapa

Una akili za kitoto sana
Yaani mgonjwa yupo theatre tayari kwa operation inasubiriwa pesa madaktari waanze na anapumlia mipira useme unaenda kuuza kuwanja Mteja apatikane after two weeks mgonjwa anasubiri tu
Uwe unasoma mawazo ya wenzio kabla hujacoment
 
kama ulikuwa umemshirikisha Mungu kupata mke mwema hakika hilo ndo amekupa jibu huyo sio mke kabisa,mm binafsi sijamuelewa ni mchoyo kupitiliza mama yako ni mama yake je angekuwa mama yake hizo hela asingetoa?

aisee yamkini huyo aliyekusaidia ndie mtu sahihi ,sasa usichukue maamuzi haraka ww endelea kumsihi Mungu,sasa hivi tulia hicho kikao peleka mbele

kuna mke wa jamaa aligoma kutoa hela ya mdogo wake alikuwa amefukuzwa chuo. mme wake alipomwuliza, akasema anasave anunue gari lake maana mmewe alikuwa nalo. ilibidi shemeji mtu aitafte hela shemeji arudi chuo.

wanawake ni hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom