Harufu ya ubwabwa porini

Harufu ya ubwabwa porini

Habari za jumapili wana JF.
Bila kupoteza muda wadau naomba kuuliza,Je ile harufu ya wali (wali nazi) ambayo tunaisikia tukiwa porini au msituni tena sehemu ambayo haina makazi ya watu inatokana na nini?
Cc. mshana jr
Si kweli kama wanajamvi wengi walivyosema ati ni harufu ya nyoka, hasa chatu, akiwa mawindoni. Maeneo mengi, yasiyo msitu, kuna nyoka na hata chatu lakini harufu hiyo haipo.

Harufu hii na nyinginezo huwapo kwenye misitu mikubwa na maeneo yenye uoto mwingi; viumbe hai wadogo sana (micro-organisms) km minyoo ya ardhini, bakteria; madini km chuma, magnesium; unyevunyevu; maji (ya vijito au mito); uozo km wa magome ya miti na majani; na mizoga ya wanyama.

Aina ya harufu itategemea aina ya udongo, na kilichooza. Mathalani waweza kunusa harufu ya wali kutokana na udongo wenye kiasi kingi cha chuma mara baada ya mvua (hewa ya oxygen iliyomo kwenye maji kuungana na chuma - kutu).

Ikumbukwe kuwa madini (ambayo ni mhimu kwa ustawi wa mimea) hutokana na kuoza kwa vitu (matter) ambapo hubadilika kuwa madini tena.

CHUNGUZA CHAMBUA AMUA CHUKUA HATUA
 
Nimepitia page 1-5 na kura imeegemea kwenye nyoka/chatu! Wachache ni shetani na wengine miti! Anyway, binafsi sijawahi experience hiyo kitu but suala la nyoka na mashetani can't buy at all!! Yaani Chatu yule acheue domo ndo kinukie kitu cha nazi? Acheni utani nyinyi....However, I can buy hao wanaosema ni harufu ya miti!! Wazee wa zamani walikuwa ni Smart Liars... kwa hofu kwamba mngetimba kusaka kitu cha mpunga wakaona bora kuwadanganya kwamba ni joka hilo!!!
 
Nimepitia page 1-5 na kura imeegemea kwenye nyoka/chatu! Wachache ni shetani na wengine miti! Anyway, binafsi sijawahi experience hiyo kitu but suala la nyoka na mashetani can't buy at all!! Yaani Chatu yule acheue domo ndo kinukie kitu cha nazi? Acheni utani nyinyi....However, I can buy hao wanaosema ni harufu ya miti!! Wazee wa zamani walikuwa ni Smart Liers... kwa hofu kwamba mngetimba kusaka kitu cha mpunga wakaona bora kuwadanganya kwamba ni joka hilo!!!
Ukwel ni nyoka akiwa anavua gamba ndo hutoa hiyo haruf nimewah kuhakikisha baada kuckia hyo haruf kutafuta tafuta nikaona gamba la nyoka, na ni nyoka yoyote sio lazima awe mkubwa, mi niliona saiz ya nyoka mdogo wa kawaida tu wanaokaa migomban,
 
Nimepitia page 1-5 na kura imeegemea kwenye nyoka/chatu! Wachache ni shetani na wengine miti! Anyway, binafsi sijawahi experience hiyo kitu but suala la nyoka na mashetani can't buy at all!! Yaani Chatu yule acheue domo ndo kinukie kitu cha nazi? Acheni utani nyinyi....However, I can buy hao wanaosema ni harufu ya miti!! Wazee wa zamani walikuwa ni Smart Liers... kwa hofu kwamba mngetimba kusaka kitu cha mpunga wakaona bora kuwadanganya kwamba ni joka hilo!!!
Ni kweli wazee wetu walikuwa na elimu asilia ya kutunza na kulinda mazingira yasiharibiwe. Kwa mfano wa hiyo harufu ya wali ilihusushwa na uwepo wa nyoka. Maeneo ya msitu yenye harufu ni yenye rutuba kubwa.
 
6cc157879c1586073e31ba31c72c5cda.jpg

Pale ambapo tembo hakuiogopa harufu ya wali
Duh!,hii ni hatari
 
Hapana mkuu huwa unazidisha. Kuandika kwako ni too low. Jaribu basi ''kujihangaisha'' kujua maneno ya kiswahili yanaandikwaje. Na hii tabia siipendi kabisa kwani inaonyesha watu kutokuwa makini na wavivu. Imaging kuna mtu mpaka kesho anaandika jina la rais kama ''Magufuri''. Tena mtu huyo unakuta ni msomi wa chuo kikuu. Hii imekuwa ni kama utamaduni wa watanzania wote.
ni kweli mkuu inakera sana! Watu wengi hawajui wapi watumie R na wapi L,tuendelee kuwakosoa tu bila kuchoka.
 
Habari za jumapili wana JF.
Bila kupoteza muda wadau naomba kuuliza,Je ile harufu ya wali (wali nazi) ambayo tunaisikia tukiwa porini au msituni tena sehemu ambayo haina makazi ya watu inatokana na nini?
Cc. mshana jr
Mkuu
Hiyo harufu inatokana na aina ya mimea. Na harufu hiyo huwa inajiri sana nyakati za jioni.
Siyo nyoka wala majini.

Mimi niliaminishwa hivyo kiwa ni nyoka mkubwa lakini nilipochunguza nikagundua si nyoka.....
 
Ni kweli ni nyoka huwa anatoa harufu hiyo au nyingine nyekuvutia akiwa kwenye mawindo ya kutafuta chakula na hasa chatu ndio mwenye sifa hiyo kwa kuna baadhi ya wanyama hufuata hiyo harufu ndio hapo anawadaka ila hii harufu ya ndio watu tumeikariri sana pia hutoa harufu ya beberu kama kuna mbuzi akiifuata anamdaka.
Kwa hiyo ze snake ana ringtone tofauti tofauti kulingana na muhusika!
 
hata me nshawai nusa hio harufu...ila sikujuaga ka ni nyoka sijui chatu...
i guess mimea pia huchangia
 
nimekumbuka mbali kidogo..mi niliambiwa ukisikia hiyo harufu kimbia fasta kwa nguvu zote..kuna siku nilitoka shule enzi za primary nikaona bungo kwenye chaka maana nkikuwa na tabia ya kupita vichakani..nikasikia hiyo harufu alaf kama tawi likavunjwa flan hivi..sasa sijui ndio huyo nyoka au vindege..sitosau nilikimbia mpaka home ila nilivunja mkono ila nilipokuwa naanguka sikujua nimevunjika
 
Back
Top Bottom