Harufu ya ubwabwa porini

Harufu ya ubwabwa porini

BINAFSI NILIPATA KUSHUHUDIA HII HATUFU NYAKATI TOFAUTI...ASUBUH...NA MCHANA WAKATI NAENDA SHAMBA ASUBUHI AMA SIKU NYINGINE WAKATI WA KURUDI MCHANA HUKO TANGA......MAJIBU YALIKUWA MAWILI NYAKATI ZOTE KUWA NI KUNA NYOKA ANAJIKOBOA MAGAMBA NA KAULI NYINGINE NI KUWA ENEO HILO KUNA MAJINI....NIMEISHIA KUSIKIA/KUAMBIWA LAKINI SIJATHIBITISHA.
 
Mimi niliwahi kuambiwa kuwa nikihisi hiyo harufu basi nisitangaze pia nijisemehe moyoni kuwa NIMESHIBA kisha niteme mate chini na niondoke eneo hilo Haraka.
 
mara nyng masimuliz za mababu huwa niza uongo uongo napia zimekaa ktk hali ya kusadikika,eg harufu porini wanadai ni nyoka kumbe ni jamii ya miti na maua huwa hutoa hzo harafu.mfano mwngne uchawi na enyewe upo katika hali hyo hyo yakufikirika haupo ktk uhalisia.
Ni kweli simulizi za kale nyingi ni za kusadikika, lengo ni kuonya, pia watu wawe makini na jambo fulani
mfano swala la kubemenda ni uongo, pia mtoto wa kiume akiangukiwa na kitovu kwenye chululuu anakua hanithi n.k n.mengi ni uongo ila yamesaidia kutuweka kwenye mstari
 
ila hakuna msosi mzuri utakaowahi kutokea kama wali nyama arage na mchicha. Uhenda haya majoka makubwa yameamua kujichanganya kwenye hii mechanism kuwavutia vitoweo vyao,
Ulichoandika ni sahihi.
Aina nyingi za nyoka hutoa harufu hiyo kwa ajili ya mawindo.
Viumbe wengi hutafuta chakula chao kupitia harufu.
Kweli utakuta imemwagwa harufu ya kutamanisha, mithili ya wali. Hapo ni kuvutia wahanga wasogee. Badala ya kula wao kuliwa.
Nyoka wakubwa kama chatu hutumia mbinu hizo pamoja na kuchezesha rangi. Anaweza akatoa rangi ya kutamanisha ambayo mhanga hujisogeza hadi mdomoni kabisa.
 
Kuna siku nikiwa shule, sekondari ya Mzumbe. Kuna mahali panaitwa faculty na ni jirani na kimsitu situ hivi. Siku hiyo mida ya alasiri kama saa 10 hivi, tulipata hiyo harufu ya kama wali hivi. Muda si mrefu alipita mbwa akiwa anakimbia kuelekea msituni. Baadaye kidogo tulianza sikia sauti ya mnyama anayelia na ambaye yupo katika maumivu. Kwanza tulidhani ni nguruwe, maana upande wa pili wa hicho kimsitu kulikuwa na mwalimu alikuwa anawafuga. Lakini baadaye tukang'amua kuwa ni mbwa. Wanafunzi wengi tulikimbilia huko na tulichokikuta....chatu anambana mbwa, yule aliyetupita faculty. Mwishoni tulifanikiwa kumuua yule chatu na mbwa alipona....Hii ilikuwa mwaka 2003. Kwa waliopitia Mzumbe sekondari watakuwa wameisikia habari hii...
Kwa uzoefu wangu huu, siku nikiisikia hiyo harufu, natoka mbio tu...
 
Katika ulimwengu huu kuna mambo mengi mno ya ajabu, kuna kitu kinaitwa miungu, hawa miungu wamegawanyika katika sehemu nyingi, kwenye mito,milima,mapango na mabwawa. Katika hali ya kupatika kwa harufu ya wali huwa mambo mawili, kwanza ni makazi ya miungu hao pili ni makazi ya nyoka ambae kwa namna moja au nyingine nae pia ni miongoni mwa miungu. Unaweza wakati mwingine ukakuta hata vyungu vya kupikia mahala hapo
Kama nyoka ni miungu waumini wake ni nani hao wasio na akili?
 
Ni majini hayo ... Kimbia haraka ukiisikia harufu
 
Back
Top Bottom