Harufu ya ubwabwa porini

Harufu ya ubwabwa porini

Kuna dogo kasema kuwa komba akikojoa huwa kuna hio smell... Kuna kama kaukweli hapo ingawa sijui maana kuna madogo kitambo kile walikuwa wakijikojolea utawatambua tu kwa harufu kali ya beche...
 
Mmh hii wengi tumeaminishwa kuwa usikiapo harufu ya wali polini jua kuna joka lakini nani Ali prove hii
Sina uhakika lakini mimi nadhani kuna miti huwa inatoa harufu ya namna hii wakati fulani eg wakati wa kuchanua. Nasema hivi kwa sababu kuna issue kama hii hii ya harufu porini lakini tofauti ni kuwa harufu inakuwa ya maziwa ya mtindi. Baada ya uchunguzi nikagundua kuwa kuna matunda fulani wakati yachanua huwa yananukia kama maziwa ya mgando.
 
Kutoka na uzoefu wangu hasa katika ngoma ya Bugoyangi ambayo huambatana na kucheza na kwenda kuwinda nyoka (majoka) kwa ajili ya show. Nyoka anapoingia kwenye shimo,anaweza ingiza kiwiliwili chote huku kichwa akikiacha nje (mwanzoni mwa shimo). Hivyo akiamua kucheua huwa anafanya hivyo kwa muda wa dakika kadhaa na hiyo harufu ndipo husikika kulingana na uelekeo wa upepo. Mkongwe wa style hiyo ni koboko ambaye anaweza pia usiku akaanza kutoa sauti mithili ya meno yanasagana (teeth friction) na akifikia hatua hiyo hapo anaelekea kuwa kichaa na akiwa kichaa hapo haangalii cha ng'ombe,mbwa wala mtoto. Wengine hulisimika barabarani kusubiri wapita njia. Kwa mliokulia mijini si rahisi kuamini hiki ila ukitaka kufanya utafiti tembelea kijijini hasa kipindi cha kiangazi huwa wana tabia ya kutafuta maji ya kunywa na vyura ambapo vichakani huwa mawindo yanakuwa machache sababu ya miti kupukutika na hivyo kuonekana kirahisi na windo lao.
 
Mkuu ukiwa porini ukanusa harufu ya ubwabwa tena ule unanukia kama Thai Jasmine am a Basmati timua mbio hapo kuna bonge la joka. Siyo uwongo hii ni kweli ila nadhan ni kuhusu nyoka alivyoumbwa kibailojia
Duuu wali jasmine umenkumbusha mbali mwana enz za ugaibuni u nanunua jasmine rice daaaa
 
Habari za jumapili wana JF.
Bila kupoteza muda wadau naomba kuuliza,Je ile harufu ya wali (wali nazi) ambayo tunaisikia tukiwa porini au msituni tena sehemu ambayo haina makazi ya watu inatokana na nini?
Cc. mshana jr
Yote tulisikia zamani lakini hiyo huwa ni harufu ya miti
 
NI mahali wachawi wamefanyia sherehe zao.Ukiwa na uwezo wa kuona unseen utawaona live.Hakuna cha nyoka wala nini
 
Ni Kweli; ni vyema ukachukua tahadhari maana yatakuwa sio mazingira mazuri kwako.....
Wakati huo nyoka atakuwa anavua gamba la kale na kuwa na mwili mpya.....wale ambao wamekulia maeneo ya meru na haswa leguruki na kwingine mtakuwa mwalijua hili vyema...ukipita kesho yake utakuta ganda la nyoka
 
Duuu wali jasmine umenkumbusha mbali mwana enz za ugaibuni u nanunua jasmine rice daaaa
mimi ni LAZIMA nile wali 'jasmine' kila siku ikipita cku sijala nakuwa mgonjwa. Yani kitu kisafi ukikifungua tu hamna haja ya kuchambua na kuosha unakimimina tu sufurian.

Maamaee Wathai
 
mkuu mbona unanishambulia sana
Hapana mkuu huwa unazidisha. Kuandika kwako ni too low. Jaribu basi ''kujihangaisha'' kujua maneno ya kiswahili yanaandikwaje. Na hii tabia siipendi kabisa kwani inaonyesha watu kutokuwa makini na wavivu. Imaging kuna mtu mpaka kesho anaandika jina la rais kama ''Magufuri''. Tena mtu huyo unakuta ni msomi wa chuo kikuu. Hii imekuwa ni kama utamaduni wa watanzania wote.
 
Habari za jumapili wana JF.
Bila kupoteza muda wadau naomba kuuliza,Je ile harufu ya wali (wali nazi) ambayo tunaisikia tukiwa porini au msituni tena sehemu ambayo haina makazi ya watu inatokana na nini?
Cc. mshana jr
Ukiwa na njaa sana lazima utahisi unanusa harufu ya ubwabwa ( reflex )
 
Back
Top Bottom