Harufu ya ubwabwa porini

Harufu ya ubwabwa porini

Mie nakumbuka zamani nilikuwa naambiwa eneo hilo lina nyoka anayejivua gamba wakati huo!
Wewe ndio imeingia ndani vizuri! Sio kwamba kuna chatu. Bali kuna nyoka anajivua gamba au ndio tayari kamaliza kujivua muda huohuo!
 
natamani nijue huko wapi
Mzee WA Copenhagen huo si ndio mchele wako huo! Unadhani utapata WA mbeya ulaya! Anyway where in Copenhagen? Mimi nlikua hapo jirani tu ukivuka daraja unaingia Marmo then Lund ushafika pande hizo?! Nlikua natembea sana Copenhagen kwenye sehemu yetu ya bangi ile! Ila sivuti
 
Hata mimi pia nilishasikia sana hiyo harufu na niliaminishwa kuwa ni nyoka anafanya yake japo sikuwahi kuprove hata siku moja.
 
Pia kuna harufu kama ya viazi mviringo vikiwa vinachemshwa wanasema ni Nyoka pia
 
Hilo la nyoka kufungua mdomo itakuwa kamba tu maanake nimewahi kuhudhuria maonesho yanayohusu nyoka mara kadhaa hasa chatu na walikuwa wanapiga miayo lakini hiyo harufu ya beche haikuwa ikinukia.

Yawezekana ni utomvu wa miti au maua tu.
Sasa chatu wa kufugwa ana njaa ?? Inawezekana huyo wa porini kakosa msosi kwa muda ikabidi ajiongeze
 
wote nie mko wrong-hii harufu ni ya mnyama mdogo sikuumbuki vizuri ni yupi either kicheche au komba akikojoa-mkojo uwa na harufu ya wali
Aisee kama ni harufu ya kicheche basi hapa kwetu kungekua kunanukia gogo deile na tena kicheche alivyo mshenzi wa tabia pa kunyea ndio anapaacha wazi na ndio mtego wake kwa kuku
 
Hapana mkuu huwa unazidisha. Kuandika kwako ni too low. Jaribu basi ''kujihangaisha'' kujua maneno ya kiswahili yanaandikwaje. Na hii tabia siipendi kabisa kwani inaonyesha watu kutokuwa makini na wavivu. Imaging kuna mtu mpaka kesho anaandika jina la rais kama ''Magufuri''. Tena mtu huyo unakuta ni msomi wa chuo kikuu. Hii imekuwa ni kama utamaduni wa watanzania wote.
Imaging ni nini ?
 
Kutokana ngano za Wakongwe..
hiyo ni ishara ya kuwa kuna Chatu maeneo ya karibu..Na hiyo ndiyo harufu akiinusa Mbwa basi hukunja mkia na kuelekea kwa chatu yeye mwenyewe huku akijilizajiliza...

Pia ukisikia harufu ya beberu katikati ya Mbuga ukue Simba yupo karibu mno na wewe..Inabidi uchukue Tahadhari..
 
mimi ni LAZIMA nile wali 'jasmine' kila siku ikipita cku sijala nakuwa mgonjwa. Yani kitu kisafi ukikifungua tu hamna haja ya kuchambua na kuosha unakimimina tu sufurian.

Maamaee Wathai
Aisee kwa tz wap unapatkana maana toka ntoke dunia ya kwanza ni shida tuu na Michele ya Mbeya ahahaha mic u jasmine rice
 
Katika ulimwengu huu kuna mambo mengi mno ya ajabu, kuna kitu kinaitwa miungu, hawa miungu wamegawanyika katika sehemu nyingi, kwenye mito,milima,mapango na mabwawa. Katika hali ya kupatika kwa harufu ya wali huwa mambo mawili, kwanza ni makazi ya miungu hao pili ni makazi ya nyoka ambae kwa namna moja au nyingine nae pia ni miongoni mwa miungu. Unaweza wakati mwingine ukakuta hata vyungu vya kupikia mahala hapo
Kwa hiyo huyo nyoka naye anapika huo wali au?
 
Aisee kama ni harufu ya kicheche basi hapa kwetu kungekua kunanukia gogo deile na tena kicheche alivyo mshenzi wa tabia pa kunyea ndio anapaacha wazi na ndio mtego wake kwa kuku
Teh! Tumemezeshwa myth nyingi sana ... Tuliambuwa kicheche akitaka kuvutia kuku, hujificha kichwa & kiwiliwili chake kwenye majani au kichaka na kuiacha sehemu ya nyuma kwa nje. Kwa kufanya hivyo hufunua sehemu ya haja kubwa, kuiacha wazi (Sehemu hii ni nyekundu) na kutengeneza umbo kama la nyanya ili kuwavutia kuku na ndege wengine wadogo. Atakayejifanya kupeleka kichwa kudonoa, kicheche humbana kichwa mpaka afe then anamla. Sijawahi kuprove kwa macho!!!
 
Haha hivi mkuu hii ni myth au ukweli ?? Kicheche anaitwaje kwa kingereza tu mgoogle hapa tujue tabia zake
 
Back
Top Bottom