Harakati za kufikisha umri wa miaka 100

Harakati za kufikisha umri wa miaka 100

Mapenzi yangu 70yrs it's enough hapo toa ajali, kiharusi, kupoteza kumbukumbu n.k

Miaka mia siitamani kabisa kabisa,,
 
Kuishi miaka mingi ni utajiri tosha kwa mwanadamu, kuliko yule aliyekuwa na utajiri mkubwa na kabla ya kufikisha miaka 70 akakata moto.​
Kuishi miaka mingi sio utajiri. Wapo watu walioishi miaka mingi Babu/Bibi lakini mara nyingi utawasikia wanaitamani siku ile ya kuambiwa "Salio lako limeisha". Wengine wanafikia umri mkubwa na wanadiriki kukataza familia "Ole wake mtu yule..hakuna kulia siku yangu ikifika"

Wapo wanaosema, ili kufikisha miaka mingi inakulazimu kila unapopiga hatua fulani za kimaisha, jitahidi kuishi maisha ya kipato cha chini, kuanzia ulaji, mazoezi, kujichanganya na jamii n.k ili kulinda afya ya mwili wako.​

Kuliko kwenye friji kujaza nyama na vyakula vya makopo, ni bora uweke matembele, mgagani, mchicha n.k​
Kuna ukweli mkubwa katika hili wani wazee wetu enzi zao ilikuwa kusikia neno presha, kisukari, moyo umetanuka,figo zinafeli ilikuwa nadra sana. Tukumbuke wale wasemaji "Mwili wako ni kile unachokula"( your body is what you eat)
Siku hizi hata hao tuliokuwa tunadhani maisha yao ni ya kiwango cha juu nao wamegeukia kula vyakula Organic foods(vyakula vya kiasilia). Vyakula vilivyosindikwa viwandani wanajitahidi sana kuviepuka. Ni sahihi kabisa tule matembele,mgagani, mnafu, mchicha, mashonanguo, n.k.


Mwili ukishaanza kuwa mzito, mashavu kujaa, kitambi kuongezeka, miguu kujaa, makalio au mapaja kunenepa, mwanaume kuishi kama mwanamke n.k ni ishara za awali za kutokufikisha miaka 100.

Ni muhimu kubadili mwenendo wa maisha, ili kuishi miaka mingi.​
Hii ni mujarabu sana. Ni heri izingatiwe kwa mustakabali wa afya zetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom