Nakumbuka kuna speech ya Late Nyerere alisema kwamba ataishi miaka 100 na ndipo Kalapini akaandika huo mstari.
Anayepanga ni Mungu ,unaweza ukafanya kila kitu kujilinda lakini ukaondoka mapema maana imeandikwa kama Bwana hatoulinda mji wake wakeshao wanafanya kazi bure.
Haujawahi kuona au kusikia jamaa amefariki amegongwa na gari alikuwa anafanya mazoezi barabarani? Lengo lake lilikuwa anafanya mazoezi ili asipate magonjwa ambayo yanayoweza kumuondoa mapema lakini ameenda barabara kufanya mazoezi anagongwa na gari anakufa mapema.
Kuna jamaa yangu aisee anafanya kazi ngumu sana za ujenzi ,kuchimba mashimo ya choo ,kulima kwenye sites lakini nashangaa alipata kisukari na maisha yake hajui kabisa maisha ya kuweka nyama kwenye friji coz kwa kipindi kile 2011 alikuwa anaishi nyumba ya udongo na haina umeme.