Happy birthday Jakaya Mrisho Kikwete

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,613
2,000
Leo Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete anatimiza miaka 70. Mimi binafsi namkumbuka kwa mambo machache aliyoyafanya:
1. Daraja la Kigamboni
2. Daraja La Kilombero
3. Daraja la Umoja
4. Daraja la Maragarasi
5. Chuo Kikuu cha Dodoma
6. Hospitali ya Mloganzila
7. Julius Nyerere International Airport terminal III.
8. Dar es salaam Rapid Transport-DART (Mwendo kasi).
9. Sekondari za Kata nchi nzima, kila kata ina shule.
10. Mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Victoria.
11. Songwe Airport
12. Kigoma Airport
13. Tabora Airport
14. Umeme wa REA
15. Benjamin Mkapa Hospital Dodoma
16. Chuo kikuu cha Nelson Mandela Arusha.
17. Dangote Cement industry
18. Bomba la gesi Mtwara to Dar
19. Hospitali ya Moyo
20. Hakuna watu wasiojulikana.
21. Hakuna mfanyabiashara kufilisiwa.
22. MOI
23. Nchi nzima kuunganishwa kwa barabara za lami, zaidi ya km 14000 zilijengwa nchi nzima.
24. Ujenzi wa Mkondo wa taifa wa mawasiliano, leo tunajimwambafai na internet.
25.Nyongeza ya mishahara kwa watumishi kila mwezi Julai.
26. Ajira kila mwaka.
27. Annual Increment ilikuwa haki ya Mtumishi.
28. Diplomasia ya kimataifa ilikuwa juu.
29. Demokrasia iliyopevuka, na alisema kuwa, hoja za kisiasa hujibiwa kisiasa, siyo kwa kipigo cha Polisi.
30. Atleast tulikula-kula bata, yaani enzi hizo laki si pesa!!
 
Eli79

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
27,394
2,000
Hakika JK alifanya, tena mambo tangible sana. Sema nini, alitukanwa mno, tena sana. Kumbe haijalishi watu umewafanyia nini, mwisho hawaridhiki tu kama asili ya binadamu ilivyo.

Alifanya yote hayo then wafipa wa ufipani wakaishia kusema wanataka dikteta, woooooi! You got what you wanted and now, everyone is crying, wanasema "be careful what you wish for". So, ngoja tuburuzwe coz it was our wish.
 
Zabron Hamis

Verified Member
Dec 19, 2016
2,744
2,000
Masikini!! Halafu wala hata hakuwahi kuchora mishahara kwenye mabango ya kura
Hakuwahi kupiga simu ili aonekane yupo
Watu walimtukana na bado akawapa ile kahawa ya ikulu
Wanatoka nje bungeni, anawaita ikulu
Alijenga barabara, akapanda ndege (alijua maisha ya watu wa chini yanategemea sana usafiri wa ardhini kuliko ndege)
 
rommy shabby

JF-Expert Member
Jun 26, 2017
738
1,000
Tena alitukanwa mnooooo akanuka mzee wa watu mpaka akakonda watu wakasema tunataka rais asiyechekacheka, rais kauza nchi kwa wachina kwa ajili ya mwanae kukamtwa, rais nchi imemshinda dah bin Adam bwn
Hakika JK alifanya, tena mambo tangible sana. Sema nini, alitukanwa mno, tena sana. Kumbe haijalishi watu umewafanyia nini, mwisho hawaridhiki tu kama asili ya binadamu ilivyo.

Alifanya yote hayo then wafipa wa ufipani wakaishia kusema wanataka dikteta, woooooi! You got what you wanted and now, everyone is crying, wanasema "be careful what you wish for". So, ngoja tuburuzwe coz it was our wish.
 
Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
52,953
2,000
@atcl kwa kipindi Cha mwezi July mpaka September imeingiza faida ya shilingi ngapi?

Happy birthday to you Mr. President, uliruhusu ushindani wa kweli wa kibiashara, Fast Jet ilitusafirisha kwa gharama nafuu sana
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
15,059
2,000
Hakika JK alifanya, tena mambo tangible sana. Sema nini, alitukanwa mno, tena sana. Kumbe haijalishi watu umewafanyia nini, mwisho hawaridhiki tu kama asili ya binadamu ilivyo.

Alifanya yote hayo then wafipa wa ufipani wakaishia kusema wanataka dikteta, woooooi! You got what you wanted and now, everyone is crying, wanasema "be careful what you wish for". So, ngoja tuburuzwe coz it was our wish.
Kwenye hicho kipengele Cha kutukana huenda hata muweka mada alifanya hivyo pia!
We subiri hata huyu papa mobimba akiondoka utawaona wanaorodhesha mambo! Ishakuwa kawaida.
 
Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,940
2,000
Ila tuache masihara... ukisikia uwekezaji kwa wananchi ndio huo sasa!!

Juzi tu hapa Serikali ya Magu imetoa tangazo la nafasi ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada... yaani Diploma!!!

Hiyo Diploma inatolewa miaka 3, na qualification ni Form IV Leavers waliopata Div I - III

Wakipata hiyo Diploma wanaenda kufundisha PRIMARY SCHOOLS na sio sekondari!!

Awamu iliyopita ilisomesha walimu wengi sana tena kwa ngazi ya digrii na kuwaajiri kiasi kwamba ikaonekana hakuna tena sababu ya kuendelea kutoa mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya cheti wakati walimu wenye shahada wamejaa na wengine wanaenda kufundisha primary schools!!

Haidhuru Magu kagoma kuwaajiri na kutumia tatizo la ajira kwa walimu kama mtaji wa kampeni!!
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,613
2,000
Hakika JK alifanya, tena mambo tangible sana. Sema nini, alitukanwa mno, tena sana. Kumbe haijalishi watu umewafanyia nini, mwisho hawaridhiki tu kama asili ya binadamu ilivyo.

Alifanya yote hayo then wafipa wa ufipani wakaishia kusema wanataka dikteta, woooooi! You got what you wanted and now, everyone is crying, wanasema "be careful what you wish for". So, ngoja tuburuzwe coz it was our wish.
Sifa huja mwishoni sio mwanzoni
 
Rubawa

JF-Expert Member
Dec 25, 2015
1,948
2,000
Happy Birthday Jakaya Khalifan Mrisho Kikwete Waukae...
IMG-20201007-WA0014.jpg

Sent from my ANE-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom