Sakala la Joshua Molel kuuawa na HAMAS lilileta mfadhahiko na tafrani kwenye jamii.
Binafsi niliona taarifa zake kuna walakini kwani Joshua tulitangaziwa na mwenzie mmoja kua walitekwa na HAMAS mnamo tarehe 7 October ila video ya mauaji ya Molel ilikuja kuachiwa mwezi December baada ya balozi wa Palestine kuanza kuelezea baadhi ya mambo kwenye media (haswa clouds tv)
Serikali ilijitokeza na kusema familia ya Molel itasafirishwa kwenda Israel kwa ajili ya taarifa zaidi,well jambo jema familia kusafirishwa kwa ajili ya briefing ila kwa mtu anaeweza kuwaza mbali inatosha kuleta maswali kua kuna taarifa zaidi za ndani haziko wazi.
Baba mzazi wa Molel amerejea kutoka Israel na kwenye mahojiano na vyombo vya habari ameeleza bayana kua mwanae alikua amevaa bullet proof na aliuawa pamoja na askari watano wa Israel walipokuja sehemu moja. Hizo ni taarifa za mzazi ambae ametoka Israel kukutana na jeshi la Israel.
Watanzania wengi wamesahau kabisa kua bado Molel iliripotiwa alikua na Mtanzania mwenzie walipotekwa na HAMAS,mbona hadi leo hatutajiwi jina lake?!! Hali yake ikoje?!! Nae alikamatwa akiwa kavaa bullet proof ama akiwa chuoni?!!.
Tumsikilize Mzee Molel mwenyewe.
View: https://www.instagram.com/reel/C1crB_6KGs0/?igsh=MzRlODBiNWFlZA==