Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ofisi ya Kata ya Mpera yawatoza Tsh 2000 Vijana wanaotuma barua za maombi ya kazi za ukusanyaji wa Anuani za Makazi

Of course, siyo kila mtu anataka pesa.

Mimi naishi Mombasa Ukonga, ila kwa Hulu barua zote ili upitishiwe lazima utoe chochote.

Lakini Kuna siku nimewahi kupeleka barua yangu serikali za Mitaa, Kinondoni hawakudai pesa yoyote ILA tu unatakiwa uwe na barua ya Mjumbe. Sasa hiyu Mjumbe ndio alitaka 3,000.
Kumbe ni mjumbe ndo alitaka hiyo elfu tatu na sio ofisi. Amka usingizini maana wengine hatuchajishwi hata mia tunapoenda ofisi hizo.
 
Kuuza na kununua mashamba ama nyumba kuna asilimia inakatwa kwa mnunuzi na muuzaji inaenda serikalini sio mifukoni mwa VEO,WEO wala mwenyekiti wa mtaa.

Hilo nimelifanya sana kwakuwa nimeuza na kununua viwanja.
Una Akili timamu?
 
Yaani 2000 tu una lalamika , wakati waweza kukuta hiyo 2000 unatumia kufanyia Mambo ya hovyo tu,

Yaani kutoa 2000 ili ukomboe maisha yako ya dhiki unashindwa, Unataka kusema haufahamu kuwa maisha ni Vita na kupigania opportunity sindio, !? Mjomba labda nikukumbushe this is Africa Kama hautaki kutoa hiyo 2000 acha ubaki na njaa zako
Ni vita isiyohitaji rushwa maana wewe ukiwa na uwezo wa kutoa rushwa halafu mwingine akawa hana huoni unamnyima haki yake ya kikatiba?
 
Kubishana kila MBUGIRA anaweza.

Sema, akikataa UTAFANYAJE ?

Toa suluhisho
Anakataa kwa misingi ipi? Kama amekataa kwasababu sina sifa hilo ni sawa ila akikataa kwasababu sijampa elfu mbili ambayo ni kinyume na ethics zake basi ntaenda ngazi inayofuata kutoa malalamiko yangu ikibidi hata TAKUKURU maana ndo kazi yao ku deal na rushwa ndogo na kubwa.
 
Halmashauri ipi?
Kwamba hujui wenyeviti wote wa mitaa na vijiji kama wanalipwa posho kwenye halmashauri zao husika nchi nzima?

Hata juzi msisitizo wa waziri wa tamisemi kwamba posho za wenyeviti wa mitaa na vijiji zilipwe kwa wakati hukulisikia?

Basi kama hata hili hulijui ni tatizo pia. Nilijua naonhea na mtu ambaye yupo updated na mambo kama haya kumbe siyo.
 
Kwamba hujui wenyeviti wote wa mitaa na vijiji kama wanalipwa posho kwenye halmashauri zao husika nchi nzima?

Hata juzi msisitizo wa waziri wa tamisemi kwamba posho za wenyeviti wa mitaa na vijiji zilipwe kwa wakati hukulisikia?

Basi kama hata hili hulijui ni tatizo pia. Nilijua naonhea na mtu ambaye yupo updated na mambo kama haya kumbe siyo.
Huna unachojua.

Na kibaya zaidi unajifanya UNAJUA.
 
Unakuwa kama mwanamke mswahili kulalamika kila kitu.Tuseme wewe kwa umri wako hujawahi kufanya kazi na mtendaji? Hujui kama kuna hela ya muhuli?
 
Huna unachojua.

Na kibaya zaidi unajifanya UNAJUA.
Ya Leo hii hio, kumbe we ndo hujui kitu unabisha tu uonekane
Screenshot_20220224-201845.jpg
 
Ya Leo hii hio, kumbe we ndo hujui kitu unabisha tu uonekane





View attachment 2130000
Kwamba hujui wenyeviti wote wa mitaa na vijiji kama wanalipwa posho kwenye halmashauri zao husika nchi nzima?

Hata juzi msisitizo wa waziri wa tamisemi kwamba posho za wenyeviti wa mitaa na vijiji zilipwe kwa wakati hukulisikia?

Basi kama hata hili hulijui ni tatizo pia. Nilijua naonhea na mtu ambaye yupo updated na mambo kama haya kumbe siyo.
Unajua kusoma? Kama unajua, hebu rudia tena kusoma maoni ya huyo jamaa yako halafu soma na taarifa ya Bashungwa uone kama ziko sawa.
 
Umeshawahi kufanya kazi na Watendaji Kata na Vijiji hata siku moja?
Nilifanya field mara mbili kama mtendaji wa kata na mtaa kwa hali niliyoiona ofisini ni haki tu kuombwa ela na hao watendaji maana vitendea kaz vingi huwa hawapewi zaidi ya kutoa wao ela zao mfukoni ili kuendesha ofisi
 
Habari za wakati huu wana jamvi,

Billa kupoteza wakati Kuna kitu jana nimekishuhudia nikabaki kinywa wazi. Kuhusu hizi nafasi ambazo serikali imekuwa ikitangaza hivi karibuni Katika halmashauri na wilaya mbali mbali nchini kuhusu kazi ya kukusanya na kuweka vibao vya ANWANI ZA MAKAZI.

Jambo la kusikitisha nililoliona Katika halmashauri ya manispaa ya Tabora ofisi ya kata ya Mpera ni kwamba watu wakipeleka barua zao Ili zisainiwe na watendaji wa kata na mtaa baada ya kusainiwa wanaambiwa watoe shilingi elfu 2000/=.

Kijana mmoja akajaribu kuhoji "mbona kwenye maelekezo ya tangazo hakuna mahali tumeambiwa tulipe hio elfu 2000/=?"

Akaambiwa "hayo ndo maelekezo tuliyopewa" na akaoneshwa orodha ya waliotoa hio pesa idadi ni kubwa kidogo.

Basi yule kijana akamwambia "mimi sina hio pesa maana sikuona maelekezo yake"

Akaambiwa "wewe una kiasi gani hapo ulipo Ili tukusaidie?"

Yule kija akawajibu "Sina kiasi chochote,"

Akaambiwa "haya kama huna basi katoe hio barua yako copy ulete copy ya hio barua."

Nikabaki najiuliza.

1. Ina maana serikali imetoa maelekezo watu walipie pesa kuomba hizo nafasi?

2. Je, waliotoa pesa hizo pesa zinapelekwa wapi?

3. Je, ambao hawajatoa pesa kama huyo kijana atakuwa na ukakika wakupata hio kazi hata kama anakidhi vigezo?

4. Inawezekana waliotoa pesa ndo wakapewa priority kuliko ambao hawajatoa?

5. Ikiwa ajira hii ya siku chache hivi mtu analipishwa je zile kazi za muda mrefu huwa watu wanatozwa kiasi gan?

Maswali ni mengi itoshe kusema inasikitisha sana.

Wasalaam
Kila mtu anakula kulingana na urefu wa kamba yake, ili mradi asivimbewe!
 
Back
Top Bottom