Habari za wakati huu wana jamvi,
Billa kupoteza wakati Kuna kitu jana nimekishuhudia nikabaki kinywa wazi. Kuhusu hizi nafasi ambazo serikali imekuwa ikitangaza hivi karibuni Katika halmashauri na wilaya mbali mbali nchini kuhusu kazi ya kukusanya na kuweka vibao vya ANWANI ZA MAKAZI.
Jambo la kusikitisha nililoliona Katika halmashauri ya manispaa ya Tabora ofisi ya kata ya Mpera ni kwamba watu wakipeleka barua zao Ili zisainiwe na watendaji wa kata na mtaa baada ya kusainiwa wanaambiwa watoe shilingi elfu 2000/=.
Kijana mmoja akajaribu kuhoji "mbona kwenye maelekezo ya tangazo hakuna mahali tumeambiwa tulipe hio elfu 2000/=?"
Akaambiwa "hayo ndo maelekezo tuliyopewa" na akaoneshwa orodha ya waliotoa hio pesa idadi ni kubwa kidogo.
Basi yule kijana akamwambia "mimi sina hio pesa maana sikuona maelekezo yake"
Akaambiwa "wewe una kiasi gani hapo ulipo Ili tukusaidie?"
Yule kija akawajibu "Sina kiasi chochote,"
Akaambiwa "haya kama huna basi katoe hio barua yako copy ulete copy ya hio barua."
Nikabaki najiuliza.
1. Ina maana serikali imetoa maelekezo watu walipie pesa kuomba hizo nafasi?
2. Je, waliotoa pesa hizo pesa zinapelekwa wapi?
3. Je, ambao hawajatoa pesa kama huyo kijana atakuwa na ukakika wakupata hio kazi hata kama anakidhi vigezo?
4. Inawezekana waliotoa pesa ndo wakapewa priority kuliko ambao hawajatoa?
5. Ikiwa ajira hii ya siku chache hivi mtu analipishwa je zile kazi za muda mrefu huwa watu wanatozwa kiasi gan?
Maswali ni mengi itoshe kusema inasikitisha sana.
Wasalaam