Halima Mdee ahamishiwa central police baada ya masaa 72

Halima Mdee ahamishiwa central police baada ya masaa 72

We kilaza sana.
Kama una njaa jiunge ccm au chadema.
Mimi sina njaa hutaona nafanya siasa mpaka nakufa.
Hayo maoni nimetoa mimi kama mtanzania kama unaona kila anayezua hoja dhidi ya chama chako basi naye ni ccm wewe ni mpuuzi tu.

Narudia wewe kama unanjaa jiunge kwenye siasa.
Asante tajiri ila umaskini si kilema but the rich also cries!
 
Wewe nawe mjinga tu. Hii ni hiari ya mtu. Hakuna sheria iliyovunjwa kwa kutumia jina bandia. Cha muhimu ni kuangalia ukweli katika andiko.

Hujavunja sheria ina ni namna yako ya kujificha,kama u jasiri kama Halima Mdee weka jina lako halisi halafu endelea na matusi yako,tuone kama hujalia po.
 
::TAARIFA::

Taarifa kwa Wanachama wa Chadema na Wananchi wa Jimbo la Kawe, Mhe Halima Mdee Mbunge wa Kawe aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Police Kituo cha Osterbay tokea siku ya Jumanne jioni mpaka sasa Amehamishiwa Central Police.

Kwa wale wote mnaotaka kumjulia hali Mbunge kwasasa tuelekee Central Police....

BY HENRY KILEWO
KATIBU CDM DSM
KILEWO- IGP SIYO MANGU TENA OHOOOOOOOOO
 
This is very true, Kawe tuna hasara kubwa, huyu mheshiiwa hata asipokuwa polisi, magereza na mahakamani, hana muda kabisa na jimbo. Kwa bahati mbaya hata chama chake na Mwenyekiti wao ni bogus, trash kabisa ya hali ya juu, hata wangekuwa na akili wange fanya innovation kwa kuomba apumzike walete acting mbunge. Ninajuta sana kumpatia kura yangu huyu mama na chama chake, vituo vye polisi vimefungwa, barabara hazipitiki, mafuriko yasiyo ya lazima kwa kushindwa kuwakabili wapigaji kama bwana Kusaga Mandege wa hapa Zoo, hana muda wa kazi huyo halima yuko busy na mambo yake tu. Pili tabia njema ni silaha, Dr Slaa alikua anasema ukweli sana hata kutaja ile list ya mwembechai lakini hana matusi, dharau na utoto wa namba hii. huyu bibie siku chache tu zilizopita aliomba msamaha mbele ya taifa zima, leo karudia yale yale hata mahakamani kesi yake itakua ngumu sana kumtetea
Acha upuuzi wako
 
Hujavunja sheria ina ni namna yako ya kujificha,kama u jasiri kama Halima Mdee weka jina lako halisi halafu endelea na matusi yako,tuone kama hujalia po.
He we jamaa kiboko. Kwani dikteta uchwara anapingwa na wenye id fake tu?
 
Busara na hekima za watanzania wengi ndio nguzo kuu ya amani na utulivu.
Mungu ibariki Tanzania
 
Asante tajiri ila umaskini si kilema but the rich also cries!
Hujui kwanini nimem-quote huyo jamaa na kumjibu hivyo, yeye alijibu kejeli akiashiria mimi natetea chama flani sasa sikua na haja ya kumjibu vizuri.
Kwanza watu wengi wanafanya siasa hapa kwetu kwa sababu ya kutaka kutuliza njaa ndio maana uongo mwingi, unakuta mtu mzima anaahidi uongo, anaiba pesa za umma alafu useme ndio siasa inapaswa kua hivyo?
Kuna mijitu inatumia ofisi za umma vibaya kisa imepata dhamana, kuna mijitu iko tayari kutetea lolote hata liwe baya kwa sababu linahusu chama chao basi lazima itetee.

Njaaa ukiiendekeza lazima utakua mnafiki na huwezi kusimamia ukweli wala haki.
Mimi siendekezi njaa, napambana na hali yangu, nahakikisha familia yangu haifi njaa, pamoja na changamoto zote za maisha njaa haiwezi kunifanya niingie kwenye siasa (kwa vitendo), sitatetea mwanasiasa kisa nataka pesa, ntasema ukweli kadri akili yangu ilivyopambanua.
 
Kweki akili za upinzani ni kama za watoto. Silaha ya mkononi inaua sana sana watu wasio mzidi 10, lakini silaha ya mdomo, kama midomo ya upinzani hua Taifa lote. Yaliyotokea Rwanda jirani ni mfano tu. Yaliyotokea Ujerumani ya Hitler haisahzuliki.

Wewe na wenzio endeleeni tu na ushabiki lakini hamfiki mbali ila rupango
Hopeless! Unadhani watu wa Kibiti hawakutumia mdomo kuji-organize? Mlikuwa wapi kuwadhibiti wakati wanapanga mipango yao mpaka leo wanasumbua kiasi hiki? Lawama za Kibiti serikali na chama chake haiwezi kukwepa maana mko bize kuchungulia meseji za Mbowe na Tundu Lissu huku watu wenye madhara makubwa mkiwaacha wakijenga mitandao ya uhalifu.

Hakuna mwenye hakimiliki na nchi hii. Kila mtu anawajibu wa kuijenga. Kwahiyo tusipangiane cha kupenda wala kufanya ili mradi sheria haivunjwi.
 
Mzitii mamlaka ndivyo Mungu alivyo amrisha. Ulipokubali kuwa raia wa Tanzania au kuja kuishi ktk ardhi ambayo ina mamlaka na kiongozi mkuu wa hiyo mamlaka ndio head of sovereign state ujue ulikubali kutawaliwa au mamlaka yako ulimkabidhi huyo mkuu wa hilo eneo na umekubali kumtii na kufuata matakwa yake kama mwakilishi wenu. Kimsingi hauko huru kwa kila kitu kama umekubali kuishi chini ya uongozi wa mamlaka fulani, kwa hivyo kuna mipaka ktk uhuru wetu.
Yohana batizaji Hakutii mamlaka kama zuzu,alikubali kukatwa kichwa
 
Hopeless! Unadhani watu wa Kibiti hawakutumia mdomo kuji-organize? Mlikuwa wapi kuwadhibiti wakati wanapanga mipango yao mpaka leo wanasumbua kiasi hiki? Lawama za Kibiti serikali na chama chake haiwezi kukwepa maana mko bize kuchungulia meseji za Mbowe na Tundu Lissu huku watu wenye madhara makubwa mkiwaacha wakijenga mitandao ya uhalifu.

Hakuna mwenye hakimiliki na nchi hii. Kila mtu anawajibu wa kuijenga. Kwahiyo tusipangiane cha kupenda wala kufanya ili mradi sheria haivunjwi.

Nilitoa hoja kakini sikutegemea ungejibu kwa jaziba. Kama Mtanzania, mpenda amani, japo umejibu kwa jaziba na matudi, nashukuru ujumbe wangu umekufikia. Nina uhakika umenielewa ila viongozi wenu wakaidi wataendelea kukamatwa.
 
Wanataka kumkomoa tu!

OvA
Au wanahisi wakimshikilia kwa muda mrefu alostro itamshika! Kumekuwa na tuhuma kuwa hutumia!
Lakini kama mpaka sasa alostro bado, basi tuhuma hizo zitakuwa ni za uongo!
 
Yuko wapi mama Sofia Simba, mama wa vijembe na kejeli?
Dhahabu ili iwe bora shurti ipitie kwenye tanuru. Mheshimiwa sana aliwahi kuitwa mbwa na Manji nasikia, lakini leo Manji anaonja joto ya jiwe.
Tuwe na akiba ya matendo yetu kwa wenzetu kwani hatujui kesh yetu na yao. Kama mtu amevunja sheria mahali sahihi ni mahakamani na sio kumzungusha mahabusu za polisi. Mungu anawaona.
Mkuu kilio cha watu wenye haki mungu anakisikia na kukijibu ni suala la muda tu atalipwa kwa haya anayotutenda
 
Faiza wewe mwanao akijikwaa mimba ya wahuni mitaani unamfanyaje?! Unamtelekeza?! Au unampa nafasi tena ki maisha?! Mwambieni Mzee hawakomoi watu hawa wa kawaida bali wale maskini wa kutupwa wa vijijini !!!
Alhamdulillah wote hawajajikwaa na wapo kwa waume zao.

Mzee hamkomoi mtu hapo. Hizo sera za kimagharibi zitatuangamiza. Akipata akalee mtoto na kama anataka kusoma aende shule za private. Huko ataruhusiwa hata kwenda na mtoto wake.
 
Nilitoa hoja kakini sikutegemea ungejibu kwa jaziba. Kama Mtanzania, mpenda amani, japo umejibu kwa jaziba na matudi, nashukuru ujumbe wangu umekufikia. Nina uhakika umenielewa ila viongozi wenu wakaidi wataendelea kukamatwa.
Ukishaanza kuwapa watu label basi hata hoja yako inapoteza muelekeo. Wewe unadhani kila anayekosoa Jeshi la polisi ni mpinzani? Upinzani ni nini kama mawaziri wakuu wa chama tawala sasa wako 'upinzani'? Una uhakika gani kuwa kesho wewe utakuwa upande uliopo sasa? Ukija kwa hoja, utajibiwa kwa hoja.
 
Au wanahisi wakimshikilia kwa muda mrefu alostro itamshika! Kumekuwa na tuhuma kuwa hutumia!
Lakini kama mpaka sasa alostro bado, basi tuhuma hizo zitakuwa ni za uongo!
Upande wa kijani ndy watumiaji wako

Ova
 
::TAARIFA::

Taarifa kwa Wanachama wa Chadema na Wananchi wa Jimbo la Kawe, Mhe Halima Mdee Mbunge wa Kawe aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Police Kituo cha Osterbay tokea siku ya Jumanne jioni mpaka sasa Amehamishiwa Central Police.

Kwa wale wote mnaotaka kumjulia hali Mbunge kwasasa tuelekee Central Police....

BY HENRY KILEWO
KATIBU CDM DSM
Hivii wale walioitwa WANAUME wa Acaccia wanakuja lini jamani loh!
Mbona wanachelewa
 
Back
Top Bottom