Halima Mdee ahamishiwa central police baada ya masaa 72

Halima Mdee ahamishiwa central police baada ya masaa 72

Ingekuwa ni vijijini hicho kituo wangemuachia wenyewe au kijiji chote kingehamia hapo... umkamate mtu bila kosa mwee!
 
Lkn ni kiongozi gani asiyekubali kukosolewa? Hivi kila anachokisema na kukifanya ni sahihi kwani yy malaika? Demokrasia IPO wapi? Hii awamu ya ajabu kweli kweli daaaaah
 
anasimamia nn? huku kawe Barabara mbovu, Maji shida,

Mkuu wa Wilaya anajua kwamba huko Kawe barabara ni mbovu na maji ni shida? Halima Mdee ndiye Waziri wa Maji? Unaonaje ukimuuliza Kitila Mkumbo kuhusu tatizo la maji huko Kawe? Kitila Mkumbo anaweza kusaidia kwa kuwahimiza DAWASCO kutatua tatizo hilo. Kitila akishindwa, nashauri uwasilishe malalamiko hayo kwa JPM, maana yeye ndiye anayeongoza serikali, ikiwemo matumizi ya kodi za wananchi. Na JPM hashindwi kitu. Ameweza kununua Boeing na Bombardier na kujenga reli ya umeme na kuwachachafya Acacia, atashindwa ishu ndogo tu ya maji huko Kawe kweli? Unamuonea Halima.
 
This is very true, Kawe tuna hasara kubwa, huyu mheshiiwa hata asipokuwa polisi, magereza na mahakamani, hana muda kabisa na jimbo. Kwa bahati mbaya hata chama chake na Mwenyekiti wao ni bogus, trash kabisa ya hali ya juu, hata wangekuwa na akili wange fanya innovation kwa kuomba apumzike walete acting mbunge. Ninajuta sana kumpatia kura yangu huyu mama na chama chake, vituo vye polisi vimefungwa, barabara hazipitiki, mafuriko yasiyo ya lazima kwa kushindwa kuwakabili wapigaji kama bwana Kusaga Mandege wa hapa Zoo, hana muda wa kazi huyo halima yuko busy na mambo yake tu. Pili tabia njema ni silaha, Dr Slaa alikua anasema ukweli sana hata kutaja ile list ya mwembechai lakini hana matusi, dharau na utoto wa namba hii. huyu bibie siku chache tu zilizopita aliomba msamaha mbele ya taifa zima, leo karudia yale yale hata mahakamani kesi yake itakua ngumu sana kumtetea

You sound so stupid and ignorant to the extent that kama ulimpigia Halima Mdee kura, namshauri aikane kura yako. Maana ni fedheha kupigiwa kura na mtu mjinga kama wewe. Naamini Halima Mdee alichaguliwa na watu wenye mitizamo chanya na wanaoona mbali na wanaojua kazi ya mbunge. Halima Mdee amechaguliwa na watu wanaoelewa kuwa si kazi ya Mbunge kufunga vituo vya polisi; si kazi ya Mbunge kujenga barabara; si kazi ya Mbunge kutoa vibali vya ujenzi unaopelekea 'mafuriko yasiyo ya lazima'. Kodi inakusanywa na serikali ya CCM. Serikali ya CCM inayoongozwa na JPM ndiyo inayopaswa kufanya mambo yote unayomtaka Halima afanye. By the way, Halima Mdee akiitisha maandamano ya kuishinikiza serikali kufanyia kazi mambo uliyoyaorodhesha utashiriki?
 
Saafi sana, mamlaka za nchi lazima ziheshimike. Akitoka huko akili itakuwa imemkaa sawa. Hii ndio laana ya kumtukana Spika Ndugai, kakutana na kisiki Mzirankende.

Huu ni uvunjaji wa sheria. Haya siyo mamlaka ya nchi, Huu Sasa unaitwa ni uonevu. . Hakuna sheria inaruhusu mtu kuwekwa ndani bila ya kupelekwa mahakani zaidi ya masaa 48. Pamoja na Rais Magufuli kutenda nazuri, hii inavua uzuri anaotenda. Anavunja sheria ambayo ameapa ataiheshimu wakati anachukuwa uongozi. Kwa kuwa wajinga kama wewe tuko wengi Tanzania, tunashelekea uonevu wa serikali ambayo ilisemekana ni serkali ya watu. TUSIKUBALI kuonewa Nchi hii ni yetu sisi sote. Mtu akikosa apelekwe mahakamani. Dentation without trial haiko kwenye katiba.
 
Acheni kumfariji ujinga, Huwezi kusema ukweli kwa kuhatarisha usalama wa nchi. Mdomo sio wa kuropoka ropoka kila kinachokujia kinywani.
Karopoka nn ,na wapi kavuja sheria mpelekeni mahakamni kama hiyo kesi haitafutwa mara moja maana huwezi toa adhabu mbili kwa mpigo yaani masaa 148 na kesi pia imfinge mika miwili kwa kuwa tayati keahatumikia hakuna keai tena
 
Mpaka Ngosha akimaliza awamu zake za utawala.
Nawasihi wananchi wenzangu mcheze ngoma mkiangalia jua vinginevyo mtaumia zaidi.

Sina chama wala sihitaji siasa, huu ni ushauri wa bure nawapa.
Ushauri wa busara unao endana na reality.
 
Acheni kumfariji ujinga, Huwezi kusema ukweli kwa kuhatarisha usalama wa nchi. Mdomo sio wa kuropoka ropoka kila kinachokujia kinywani.

Nchi inahatarishwa na wavunja sheria, Viongozi wenyewe. Huwezi kumuweka mutu ndani zaidi ya masaa 48 kinyume cha sheria, kwa kudai anahatarisha usalama, hii ni kuwaziba watu midomo. Kama amefanya kosa mahakama zipo apelekwe mahakamani. Serikali ikitaka nchi iwe na amani iache uonevu Watanzania sio watoto wala ng'ombe kuzibwa midomo. Acheni siasa zenu za kuwa fanya Watanzania wajinga.
 
::TAARIFA::

Taarifa kwa Wanachama wa Chadema na Wananchi wa Jimbo la Kawe, Mhe Halima Mdee Mbunge wa Kawe aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Police Kituo cha Osterbay tokea siku ya Jumanne jioni mpaka sasa Amehamishiwa Central Police.

Kwa wale wote mnaotaka kumjulia hali Mbunge kwasasa tuelekee Central Police....

BY HENRY KILEWO
KATIBU CDM DSM


Huu ni uonevu mkubwa na uvunjaji wa sheria Rais aliyoapa ataiheshimu. Watanzania wote wasipige makofi Kushelekea uvunjaji wa haki na sheria. Hii sio kuhusu chama, wala siasa, ni kutetea haki za Watanzania wote ziheshimiwe. Mtu yeyote akikosa apelekwe mahakamani, kumuweka ndani, ni kutumia madaraka vibaya. Mwalim Nyerere kila mala ALISEMA usitumie cheo chako bila ya kufuata sheria. Ukimya wa Watanzania imeifikisha Nchi hii hapa ilipo. Pamoja na Rais kupigana na ufisadi, uonevu kama huu zaidi ya kumuvunjia heshima, unamuchonganisha na watu. Ndiyo pengine Mdee amekosa, serikali iache mahakama iamue na siyo kumuweka ndani kinyume cha sheria, Huu ni unyama. Serikali ikifanya vizuri tuiunge mkono, ikosea lazima tuseme tusipige makofi wala isituzibe midomo kwa kusingizia usalama. Usalama unaletwa na haki sio jela.
 
Saafi sana, mamlaka za nchi lazima ziheshimike. Akitoka huko akili itakuwa imemkaa sawa. Hii ndio laana ya kumtukana Spika Ndugai, kakutana na kisiki Mzirankende.
Laana hii itawarudia wote wenye chuki na visasi wakiongozwa na ngosha
 
Anayeropoka si mwingine, ni wewe. Halima akifa leo historia inaandika jinsi wapumbavu wachache kama wewe wanavyashangilia utawala wa kidikiteta.

Hayawi hayawi, yatakuwa. Watu wapumbavu kama ninyi mnastahili kufungiwa mawe ya kusagia mkatupwe baharini. Lakini nchi inapotumbukia katika lindi la umaskini kwa ajili ya utawala wenye dhuruma mnashangilia, hautaangalia baadaye kuwa wewe ulikuwa unausupport, iko siku itafikia kwako,
Ila mkuu,be sincere kabisa toka moyoni mwako,ungependa kweli Halima afe kwa ajili ya historia kama angekuwa ni dada yako wa damu?Kwa shujaa huenda kilio,kwa muoga huenda kicheko,tusiwe tunawadanganya watu bana.How many times umeshawekwa ndani wewe au unadhani ni rahisi tu,for the sake of history!!?

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
What if they release her? Kuna shida yoyote?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Ujasiri wa kutumia Verified name huna unajifaragua kuondoa Serikali Madarakani? Unadhan hao kina Mbowe hawatamani kuindoa Serikali Madarakani ?
Ukijaribu kulegeza Koki ujiandae kuloweshwa kabla ya kuing'oa hiyo Koki!
...wewe ni verified kwani? Acha ulofa...
Hawa wajinga wanafikiri nchi ya kwao pekee.


Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Bunge kaz yake ni kutetea wananchi bungeni na sio kaz yake kujenga barabara wala maji. Hiyo ni kaz ya serikal
....Mkuu unadhani wanalitambua hilo? Twaweza hoyeee!!

Sent from my CHC-U01 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom