HALI YA MZEE MALECELA: Ninawashukuru Sana JF

Status
Not open for further replies.
Ni habari njema kwa mzee Tingatinga kupata nafuu, Mungu amsaidie apone mapema
 
Mungu aendelee kumlinda kwani bado tunahitaji mchango wake
 
- Wakuu wote heshima mbele sana na SALUTE! Hapa nipo na mama tunasoma ujumbe wote kwa kweli sio siri kuna ya kuchekesha sana na kuhuzunisha pia, lakini one voice Taifa kwanza!

- Mama anawashukuru sana wale wote mnaoomba arudi mjengoni mapema, maana you made her day!

Much Respect People
!

Willie @ NYC, USA.
 
Pole sana kwa kuuguliwa, na tunamtakia mzee Malecela recovery ya haraka ili aweze kuendelea na shughuli zake za kila siku kama kawaida yake.
 

Poleni sana mkuu. Tuko pamoja
 
Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu Mola wa walimwengu wote, amzidishie afya na siha njema mzee wetu Malecela, nawe uwe na subra kwao Insha'Allah.
 
Bwana William nikutakie pole na Mungu amrejeshee afya mzee na mama arejee mjengoni ili akapashe mambo moto japo sina hakika kama hajapunguza mwendo, ila kama anafuatilia kinachoendelea mjengoni basi arejee akiwa amejipanga na kuweka taifa mbele chama pembeni
 
Mmmmmh,kukimbilia kutibiwa nje ya nchi, hasa kwa kiongoz ni kutoiamin sistimu
 


Mkuu poleni sana, naomba mungu aendelee kumpa mzee wetu nguvu na afya. Nakubaliana kwamba kwenye issues za kibinadamu tuweke siasa pembeni.

Tukiwa wazima wa afya tufanye siasa.
 
Mpe salamu Mzee Mwambie apumzike kwa salama kwa kipindi kifupi, na baadae arudi Nyumbani huku Nchi Inayumbaaaa haina Wazee wa Busara wameshakwisha
 

Kujivua gamba na tawi jipya la CCM New York City, USA
by William Malecela on Saturday, April 23, 2011 at 1:12am


@ NEW YORK: Kutokana na kujivua gamba KUJIVUA GAMBA hivi karibuni, Nimeamua kukiunga mkono chama changu CCM kwa KUANZISHA RASMI TAWI LAKE HAPA New York City na vitongoji vyake. NINAWASILIANA NA CCM MAKAO MAKUU DODOMA ili kupata maelekezo ya kanuni za kufungua Tawi nje ya nchi. NINAWAKARIBISHA SANA wale wote wenye nia njema na taifa letu kama mimi, ili tushirikiane kukisaidia mawazo chama chetu NYUMBANI tokea ughaibuni, kwenye kuelekea KUJIVUA GAMBA ZAIDI KWA MANUFAA YA TAIFA LETU.
- NITAENDELEA KUWAFAHAMISHA ZAIDI MAENDELEO YA KUELEKEA KULIFUNGUA TAWI HILI LA CCM, NEW YORK CITY; NITAFANYA KIKAO HIVI KARIBUNI SANA CHA KUWEKA MSINGI WA CHAMA NA KUCHAGUA VIONGOZI WA MUDA, MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

- IDUMU CCM NA KUJIVUA GAMBA; IDUMU TANZANIA!

William Malecela - COMMUNITY ORGANIZER (CO).
 
Mzee Malecela tunamtakia afya njema kabisa na apone arudi aendelee kuwashauri wabinafsi wa ccm. Mama Kilango tunakosa kabisa mchango wake mjengoni,sijui hili la posho angesemaje manake nimpiganaji tunamjua bahati mbaya anachezea timu ya magamba.
 
Hongera sana kwa kumleta mzee nyc usa Baada ya kuugua,lakini huu ndio muda muafaka wa kumuuliza kwanini hawakujenga hospital nzuri nyumbani kipindi wako kwenye power?
Yeye anaweza kuja kwako mzee wa USA akiugua lakini je kwa wale wasiojiweza vp?

alipanga kujenga akiwa raisi bahati mbaya waka mchakachua...lol


Walijenga ya Vichaa Idodomia! Ingawa sijui kama ni majengo tu au ni hospital kamili?
 
Mzee Malecela ni muadilifu..na muungwana sana...yuko fair.. na kama ilivyo kawaida wanyoofu hawapendwi sana ndani ya chama cha magamba...

ndiyo siri ya kutoruhusiwa kuikaribia ikulu...

Tunamwomba Mungu amrejeshee nguvu zake haraka iwezekanavyo!
 
Willy, kwenye ibada ya maombi ya kanisani kwetu leo jioni hii tutamwombe naye pia. Mpe pole mweleze JF wanavyothamini mchango wake. Hajawahi kusaini mkataba kama wa akina "mzee mvi".
 
Shukrani zimrejee muumba hatuna shaka na kazi yake hope tutakua nae tz soon.msalimie mama mwambie
tunamuhitaji sana kabla ya budget ya wizara ya ngereja haijapita naimani anajambo la kutujuza
 
- Well, again ahsante sana kwa wote, leo nilikuwa ninamsomea hii thread amekufa sana na mbaavu maana kwa heshima ya kila mchangiaji nimemsomea mchango wa kila mchangiaji, michango ya Ecoli imemvunja sana mbaavu, infact amesema akiwa fit kabisa ataanza kuingia hapa mwenyewe! ha! ha! ha!

Willie @ NYC, USA.
 
Poleni sana mkuu. Mzee amelazwa hospitali gani hapo NYC? Mungu awatie nguvu na kuwaongoza during this difficulty and trying times. Hope he get well soon
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…